WABHEJASANA
JF-Expert Member
- Jun 22, 2011
- 4,225
- 869
Mi najua yupo mwanza kwa mwaliko maalum na wazee wa mila.
Siasa zinazochochea udini ni hatari na tutaendelea kuzikemea Accordingly.Hivi kuna haja gani ya kuhusisha kampeni, mitandao ya kampeni za urais/ubunge/udiwani na nyumba za ibada bila kujali dini? wakuu hili jambo ni double trafficking tuweni makini.Naona dalili mbaya mbele ya safari.Siwataji kwamba ni viongozi gani ambao washaanza kukatumia haka kamchezo kuelekea 2015 ila kwa kuwa wanajijua nawasihi waache.Watazua mgogoro usio wa lazma.WAKUU,
Nimepata taarifa kutoka huko Mkoani Geita Kwamba Aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa ameanza kuvamia kanda ya ziwa na harambee zake na anatarajiwa kufanya Harambee kubwa ya kuchangia kanisa la AICT Mjini Geita kwa ajili ya ujenzi wa Kanisa hilo Juni 16 mwaka huu.
Hata hivyo baadhi ya watu wanaoshughulikia ziara hiyo kwa ukaribu wamenidokeza kwamba pamoja na Harambee hiyo lakini ED anakwenda huko kwa kazi maalum ya kupanga safu yake ya Kanda ya Ziwa katika uchaguzi Mkuu ujao 2015!
Atawaambia wamchague yeye kwasababu anachangia kanisa. Bongo bwana akishinda uchaguzi kwa mfano, kanisa lina haki ya kusema lilimsaidia!
hamchelewi kumpa Utemi wa usukumani nyie!
Tuwe na Mtemi wa Kimeru???
Yeye awanunue hao wanaofanya naye maigizo mbele ya TV ili akarushwe kwenye TBC yake
Wewee... wasukuma ni watu makini na wenye kujitosheleza kiuongozi na kila kitu! Huyu mzee wa watu kaja na mambo yake ya kanisa tu....!hamchelewi kumpa Utemi wa usukumani nyie!
Ndg,wanaweza kumpa...si juzi walimpa Pindaa..huyu kidogo mizimu ya kisukuma itamsaidia kupunguza kulia lia kwake...kuna mwingine baada ya kuiba na kuliingizia taifa hasara kubwa(chenge) wasukuma wakamtunuku UTEMI kwa kazi Nzuri na nzito ya uizi....
Lakini kiboko yao ni yule aliyewaambia pale Bujora kuwa"wanafunzi wanaopata mimba ni vihere hele" baada ya kazi hiyo nzito wakamtunuku UTEMI na kumuita MASANJA huku kabla ya hapo akiwa amepewa kiti kama hicho sehemu tofauti tofauti na kubeba mizimu ya makabila tofauti matokeo yake mizimu inapambana kweli kweli na kusababisha kila akaapo anaishia kujiinamia na kusinzia.....mizimu ya kimasai,kikurya,kiha,kihaya,kihehe,kisukuma,kinyakyusa,kifipa ikibebwa na mtu mmoja anaweza kuishia kuwa zezeta.. Kosa jingine jina la Masanja,hili jina si la kupewa mtu hovyo hovyo,wasukama wametuharibia rais wetu kiasi kwamba kichwani mwake anawaza kuwa MASANJA kweli kwa kutumia mda mwingi kuizunguka Dunia.