Lowassa atoboa siri ugonjwa wake

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,322
33,128
reglowassa.jpg
Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa, akiungumza na waandishi wa habari kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam jana, baada ya kurejea akitokea nchini Ujerumani alikokwenda kwa matibabu ya macho. Kulia ni Mkewe, Regina. Picha na Emmanuel Herman​

Boniface Meena
WAZIRI Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa amerejea nchini kutoka Ujerumani alikokwenda kwa matibabu na kuzungumzia afya yake akisema anasumbuliwa na ugonjwa wa macho,na kujitutumua kwa kukunja ngumi huku akitamba kuwa yuko tayari kwa mapambano.

Tangu mwanasiasa huyo alipondoka nchini kimya kimya wiki kadhaa zilizopita kwenda Ujerumani kwa matibabu, suala la afya yake limezua gumzo na kuibua mijadala kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii, huku baadhi ikidai hali ni mbaya.

Machi 7 mwaka huu, Lowassa alilitihibitishia Mwananchi kwamba alikuwa hospitalini nje ya nchi lakini, hakuwa tayari kufafanua alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa gani wala kutaja hospitali aliyolazwa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), jijini Dar es Salaam, Lowassa alisema alikwenda Ujerumani kuchunguzwa tatizo la macho ambalo lilikuwa likimsumbua.

"Kumekuwa na maneno mengi kuwa naumwa na wengine wakisema ni mgonjwa sana lakini, yote hayo ni uongo,"alisema Lowassa na kuongeza:

"Nilikuwa Ujerumani kwa ajili ya kuchunguzwa macho kama yana matatizo. Profesa wangu aliniambia niende ili kuangalia kama nahitajika kufanyiwa operation (upasuaji) lakini, ameniambia sina tatizo na afya yangu ni nzuri na pia mapigo yangu ya moyo yako 120/40 niko vizuri na sina presha."

Lowassa alisema alichokuwa akikifanya huko ni kuangalia afya yake, na kuwaomba watu wajue kuwa hana tatizo lolote.

Katika kuthibitisha kwamba hana tatizo lolote, Lowassa alikunja ngumi mbele ya waandishi wa habari na kunyosha mikono yake huku akicheka , kuthibitisha kuwa yu buheri wa afya.

Alifanya hivyo baada ya kuombwa na mmoja wa waandishi wa habari athibitishe kama yuko mzima wa afya. "Niko vizuri, niko tayari kwa mapambano yaliyoko mbele yetu," alisema Lowassa bila kufafanua ni mapambano gani.

Ingawa hakutaka kufafanua mapambano yake hayo, Lowassa amekuwa akitajwa kutaka kuwania urais mwaka 2015, kumrithi Rais Jakaya Kikwete atakapomaliza muda wake kikatiba.

Lowassa alikataa kujibu maswali mengine ikiwemo kampeni za ubunge Arumeru Mashariki kwa mgombea wa CCM, Sioi Sumari kuhusishwa na yeye.

Alisema hawezi kuzungumzia suala hilo kwa kuwa mkutano huo ulikuwa maalumu kuzungumzia suala la afya yake.

Regina Lowassa

Kwa upande wa mke wake, Regina, aliyekuwa amefuatana naye, alisema mumewe ni mzima na yuko imara kwa kuwa hana tatizo lolote.

"Mume wangu hajambo, yuko imara kabisa na hana tatizo lolote,"alisema Regina.

Hata hivyo, mkutano huo ulikuwa na mazingira magumu kwa waandishi wa habari kuuliza maswali mengine baada ya baadhi ya wenzao kuwazui.
"Mheshimiwa alitaka kuzungumzia tu afya yake na si kitu kingine."Zilizikika baadhi ya kauli zikisisitiza.

Utata wa afya yake

Wakati Lowassa anazungumza na gazeti hili Machi 7 mwaka huu, alijibu kama ifuatavyo:

Swali: Asalaam alaykum Mheshimiwa Lowassa.
Jibu: Waalaykum Salaam.

Swali: Mimi naitwa... (jina la mwandishi) kutoka gazeti la Mwananchi. Kwanza pole kwa matatizo ya kiafya yanayokusumbua.
Jibu: Ahsante.

Swali: Nimekupigia pamoja na kukupa pole, nilitaka kujua unaendeleaje na matibabu?
Jibu: Niko hospitalini kwa sasa naomba niache mambo mengine tutaongea baadaye.

Swali: Lakini, ni matibabu gani hasa unayopata?
Jibu: ... (akimtaja mwandishi) naomba niache niko hospitalini sasa hivi mambo mengine tuongee baadaye.

Lowassa alitoa majibu hayo majira ya saa nane mchana na alipopigiwa tena saa 10.20 jioni, alijibu kama ifuatavyo:

Swali: Naam, Mheshimiwa Lowassa nimekupigia tena mimi... (mwandishi akajitambulisha).
Jibu: ... Unataka nikuambie nini tena? Nilishakwambia niko hospitalini niache!

Swali: Sawa, natambua uko hospitalini, lakini wewe ni kiongozi ambaye umewahi kuwa Waziri Mkuu, hivyo Watanzania wangependa kujua maendeleo ya afya yako kutokana na utata ulioibuka na kama je, umelazwa hapo hospitalini au uko katika matibabu ya kawaida?
Jibu Niache, ninachokwambia niko hospitalini sasa unataka nini tena? Nisingependa kuzungumzia afya yangu kwa undani.

chanzo.
Lowassa atoboa siri ugonjwa wake
 
Kama mapigo ya moyo wake ni 120/80 basi ana matatizo makubwa sana. Au yule profesa wake ni maji marefu
 
Anajitutumua tu... Mbona habari za kuaminika kutoka vyanzo nyeti vya serikali vinasema jamaa afya yake mbovu. Politicians sio wakweli anajua akisema hali halisi atapoteza mashabiki na itakua advantage kwa opponents wake. Naskia pia kapoteza vision kabisa aseme ukweli tu ila najua hafiki 2015.
 
hakuna mtu wa umri wake anayeweza kuwa na presha ya 120/80 labda kama anaumwa low presha!!!
 
Do you need to go to German to find out your blood pressure is 120/80 ??
 
Back
Top Bottom