WanaJF,
Lowassa anazidi kuwapeleka mchakamchaka wapinzani wake kuelekea uchaguzi mkuu hapo oktoba!
Ukiachana na kauli aliyoitoa kuhusu kupima afya kwa kila mtangaza nia wa CCM. Hii kauli nyingine ameitoka kwa kamati ya maadili na usalama wa chama pindi waandapo vigezo na masharti kwa upande wa maadili kwa wagombea wa CCM.
Mhe Lowassa alitoa pendekezo kuwa, kamati ya maadili ichunguze mali na raslimali za watangaza nia wote wa chama kwa nafasi ya urais kwa kuwaajili wapelelezi binafsi (private investigator) na hilo liende sambamba na kuchunguza wafadhili na wadhamini wa watangaza nia kwa upande wa nafasi ya urais.
Pendekezo hilo lilipokelewa vizuri na wajumbe wa kamati hiyo muhimu ya chama, ila isipokuwa waziri mkuu mhe Pinda na Membe wao wamelipinga vikali pendekezo hilo kwa madai kuwa alitekelezeki!
Hoja yao waheshimiwa hao wawili ni kwamba, kwa muda uliobaki sasa na taratibu za mchakato wa uchaguzi zilivyo, kamati hiyo ya maadili haiwezi kushughulikia mambo ya upelelezi kwa watangaza nia wa nafasi ya urais.
Rai yangu: Mtanzania, kuwa makini na watu unaoenda kuwapa hazina yako. Kama watu hawapo tayari kuchunguzwa ili kupima uadilifu wao wanapoitumikia serikali katika nafasi zao, je watu wa aina hiyo wanastahili kuaminiwa na kukabidhiwa Ikulu?
Note: Private Investigators ni watu ambao wana nafasi, uwezo na fursa ya kupata taarifa yoyote waitakayo. Hivyo inapaswa kamati ya maadili ya chama iyafanyie kazi mapendekezo ya Lowassa ili tuweze kupata mtu sahihi.
Pia, kwa wale wanaoota UKAWA itaingia Ikulu mwezi novemba nawataka mzinduke kutoka usingizini. Rais ajae atatoka CCM na hilo halina mjadala. Jambo la msingi ni kumchagua yupi bora kati ya watangaza nia tulionao sasa.