Masterproud
JF-Expert Member
- Sep 14, 2012
- 441
- 118
Alipoulizwa kuhusu walimu na vitendea kazi, Lowassa alisisitiza shule lazima zijengwe. Kukaa benchi kama kunamfanya mtu awe na akili basi kila kiongozi angekaa benchi kama mwaka na kurudi kazini.Huyu huyu Lowassa angekuwa bado serikalini angetetea kwa nguvu zake zote utendaji wa serikali. Ndiye aliyeanzisha shule za kata, ni lini amegundua kuwa kuna haja ya kuwa na waalimu bora kabla ya kuanzisha hizo shule? He is part of the problem, he cannot be part of the solution.
The guy is so desperate.Anaweza kusema ama kufanya chochote.Vitu alivyoshindwa kufanya akiwa PM anataka kutuambia Rais alikua akimzuia?Na vipi hapeleki hoja binafsi au mapendekezo bungeni?
-Hizi ghiliba na ulaghai wanaotaka kupandikiza ni lazima tukabiliane nazo.Kuanzia January tutazunguka vijijini kuwaeleza wananchi ukweli wakati huo huo tukiendelea kuunda mfumo na sera mbadala tutakazotumia baada ya 2015.......
Ndugu Ben naomba mkipita huko vijijini mchukue majina na namba za wanaopenda mabadiliko kwa ajili ya kuwasiliana nao mara kwa mara pindi mtakapokuwa mmeshapita kwa ajili ya kuhamasisha mabadiliko. huu ni wakati wa mabadiliko hatuwezi kukubali kuwa na mfumo wa waziri yule yule toka 1990 mpaka leo yeye ni kubadilisha wizara tu......
Ndugu Ben naomba mkipita huko vijijini mchukue majina na namba za wanaopenda mabadiliko kwa ajili ya kuwasiliana nao mara kwa mara pindi mtakapokuwa mmeshapita kwa ajili ya kuhamasisha mabadiliko. huu ni wakati wa mabadiliko hatuwezi kukubali kuwa na mfumo wa waziri yule yule toka 1990 mpaka leo yeye ni kubadilisha wizara tu........
Viongozi wa TZ ni wa ajabu sana!
(1)LOWASA-Alikuwa PM lkn HAKUTHUBUTU kuyasema mapungufu ya mfumo wetu wa elimu na KUYAPATIA UFUMBUZI alipokuwa madarakani!
(2)SUMAYE-Alikuwa PM na ndiye aliitumbukiza nchi kwenye rushwa ya uchaguzi alipoongoza Bunge litunge sheria ya TAKRIMA lkn sasa analia kuwa Mama Nagu alimuangusha kwa rushwa amesahau kuwa ni YY aliyeiasisi!
(3)Mzee Mangula nae juzi kasema atapambana na rushwa lkn KASAHAU kuwa ndiye yeye aliipamba kwa kutamka kuwa"mgombea kuwahudumia wapiga kura KABLA ya kupiga kupiga kura sio dhambi"lkn baadae akalalamika sana alipoangushwa kwa rushwa na Jah People kule Iringa!
INA MAANA VIONGOZI WETU WANAONA MATATIZO HADI WAKITOKA MADARAKANI?Lowassa na wenzake ni wa kupuuzwa na HAWANA JIPYA!........
Ofcourse akae Pembeni.Kuna mdau kasema kuna vitu unaweza kuona ukiwa pembeni.Yes Namuunga mkono na ndiyo maana tunataka kumshauri na ikibidi kumshinikiza akae pembeni.Hatuko tayari taifa zima kugeuzwa Mradi wa RICHMOND
Ben Richmond unajua ya nani? yeye kama mtanzania kwenye katiba ibara ya 8 ana haki ya kuongea kuhusu nchi au kushauri hivyo siasa isipitilize wakati mwingine." KUNYATA ANYATE KINYONGA AKINYATA KICHECHE ANA VIZIA KUKU"
Anachosema Lowassa ni kuwa sera za chama chake kuhusu elimu zimeshindwa. It is as simple as that. Na anataka Watanzania wawaangalie wao tena kuona kama wanaweza kutengeneza walichobomoa.
Tunakoelekea waTZ siyo kuzuri. Hivi kweli mtu aogope kutoa dukuduku lake moyoni au mawazo yake ya namna ya kuboresha jambo fulani eti kwa sababu tu jambo analoongelea alishindwa kulitekeleza wakati alipokuwa na fursa ya kuwa miongoni mwa viongozi!!!??? Sidhani kama hiyo inaketa mantiki. In fact, kuna mambo ambayo ukiwa nje unayaona vizuri kuliko ukiwa ndani. Kwa hiyo, kwa kuwa nchi inahitaji mawazo ya watu katika kuijenga, lazima turuhusu kila mtu awe na uhuru wa kuchangia mawazo yake whether alikuwa au hajawahi kuwa kiongozi.
Viongozi wa TZ ni wa ajabu sana!
(1)LOWASA-Alikuwa PM lkn HAKUTHUBUTU kuyasema mapungufu ya mfumo wetu wa elimu na KUYAPATIA UFUMBUZI alipokuwa madarakani!
(2)SUMAYE-Alikuwa PM na ndiye aliitumbukiza nchi kwenye rushwa ya uchaguzi alipoongoza Bunge litunge sheria ya TAKRIMA lkn sasa analia kuwa Mama Nagu alimuangusha kwa rushwa amesahau kuwa ni YY aliyeiasisi!
(3)Mzee Mangula nae juzi kasema atapambana na rushwa lkn KASAHAU kuwa ndiye yeye aliipamba kwa kutamka kuwa"mgombea kuwahudumia wapiga kura KABLA ya kupiga kupiga kura sio dhambi"lkn baadae akalalamika sana alipoangushwa kwa rushwa na Jah People kule Iringa!
INA MAANA VIONGOZI WETU WANAONA MATATIZO HADI WAKITOKA MADARAKANI?Lowassa na wenzake ni wa kupuuzwa na HAWANA JIPYA!
LEO KATIKA GAZETI LA MWANANCHI:WAZIRI Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa amesema kuna haja ya kutathmini upya mfumo wa elimu nchini, ili kuona kama bado unafaa au la.Alisema hatua hiyo inapaswa kufanywa sasa kabla mambo hayajaharibika zaidi na kwamba anaamini kuwa tangu mfumo uliopowekwe enzi za Mwalimu Nyerere, kuna mabadiliko mengi yamejitokeza.
Lowassa alisema hayo jana alipokuwa akizungumza na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) ofisini kwake jijini Dar es slaam.Mimi nasema kuwa sasa wakati umefika kama taifa. kuunda tume ya elimu, ili kuangalia na kupitia mfumo wote wa elimu, kuangalia mitalaa yetu kuanzia elimu ya awali mpaka vyuo vikuu, kuangalia ubora wa elimu hiyo, vitabu gani vitumike, maslahi ya walimu, yaani kwa ujumla tuangalie upya kuhusu mfumo wa elimu yetu.alisisitiza Lowassa.Lowassa alipendekeza kuundwa kwa tume ya elimu kwa ajili ya kufanya kazi hiyo, ili kwenda na wakati. Tume hiyo iundwe kuchunguza, kutathmini na kuona, endapo mfumo wa elimu wa sasa unaendana na wakati,Lowassa alisema nchi zote zilizoendelea duniani, zimekuwa zikifanya hivyo.Marekani hivi sasa kuna mchakato wa kuangalia elimu inayotolewa kama inaendana na changamoto za karne ya 21, alisema.Kumekuwa na malalamiko mengi miongoni mwa wadau wa sekta ya elimu kwamba mitalaa ya elimu nchini, haimwandai mwanafunzi kukabiliana na changamoto za maisha ya karne hii ikiwa ni pamoja na kujiajiri.
Lowassa ambaye pia ni Mbunge wa Monduli, amesema Serikali ya CCM imefanya mambo makubwa sana katika sekta ya elimu, hususan awamu hii ya nne ambayo kwa mafanikio makubwa, imeweza kujenga shule za sekondari katika kata zote nchini.Katika mkutano wake mkuu wa nane hivi karibuni mjini Dodoma, CCM ilitoa mapendekezo kadhaa miongoni mwao likiwa la kuboresha elimu nchini.Mimi nilipata bahati ya kuongoza juhudi hizo za Serikali kwa mafanikio makubwa kujenga shule hizo, lakini mafanikio hayo yamekuja na changamoto zakealisema.Alisema changamoto kubwa zilizojitokeza katika mafanikio hayo ni ubora wa elimu inayotolewa na shule hizo, uhaba wa walimu na vitendea kazi vikiwemo vitabu na masilahi kwa walimu.
Alisema Tanzania ina bahati ya kuwa na wasomi waliobobea ambao wanaweza kazi hii ya kuangalia mitalaa inayotumika ili kuona kama inakidhi haja na matakwa ya karne ya sasa.My Take- Hivi Lowassa anapochukua muda mwingi kuongea haya na vyombo vya Habari ni sehemu sahihi?.
Lowassa ni Mbunge kama wabunge wengine kwa nini haya anayoyasema asingeyaongea Bungeni ambayo ni sehemu muafaka na Bajeti ya serikali ndiko inakopitia?