Lowassa apokwa mali zake, Ana hali mbaya sana ameuza nyumba Masaki

Hivi hamjui hata nyumba yake ya Masaki ndio amepangisha ubalozi wa South Africa Ulioko Tz, endeleeni kujifariji eti kafirisika
 
Inasemekana kutoka kwa nani?Nani anasema?Umesikia wapi?

Wewe na huyo mzee nani wa kuhurumiwa?Hivi wakati mwingine mnapoandika hamfanyi self evaluation?Wewe na huyu mzee nani wa kuonewa huruma?mwenzako anakula pensheni ya uwaziri mkuu mpaka anakufa, unajua mafao yao ni kiasi gani?Yaani hata hizo tafiti ndogo unashindwa kufanya?

Endelea kungojea na utangojea kama fisi anavyoungojea mkono uanguke ili haukote

Kila mwezi mzee anapewa 80% ya mshahara wa waziri mkuu wa sasa hivi bado afya wanamhudumia, ulinzi afu anataka kujifananisha nae ye we unaishi manzese kwa mfuga mbwa "bila 7,000 kwa siku hau survive"
 
Siasa zimetuharibu kiasi kwamba ubongo zetu tunazitumia kwa asilimia 2 tu , na tumebaki kusifiana yule jamaa ana bonge la Jumba masaki na mambo kama hayo, habari yenyewe kwanza ni feki hiyo
Mawazo ya kimaskini ndo yanazidi kuligharimu taifa. Imagine mtu anauza nyumba yake basi gazeti linasema ana hali mbaya na watu wanashangilia. Mi sio mfuasi wa Lowasa ila nakereka habari nyepesi kama hizi zinapata wasomaji, inaonesha ni kiasi gani watanzania wengi walivo na akili fupi. Kuna real estate hizi hapa nimezicheki sahiv huko South Africa zote zinapatikana kwa bei below $ 500,000 sasa mfano lowasa ameuza hiyo akaenda kununua huko which economically ni kitu kizuri mno. Ntazidi kulia na watu kuzidi kuwa na mawazo ya kimaskini. Embu ona tu hii mifano. sasa akinunua huku bado kuna habari itasema Lowasa fisadi.. Sad! Ignorance
jf12.jpg
jf11.jpg
jf10.JPG
 
..inasemekana aliuza nyumba apate hela za kampeni ili akishinda urais angezirudisha kwa kupiga dili. Mzee huyu ni wa kuhurumia kwani akina mbowe walijua fika anao mkwanja, wakauvuta na kumpatia matumaini hewa ya ushindi. Sasa wanamvutia kasi tena 2020 walambe tena, mwishowe ataishia kuuza kila kitu, we ngoja tu.

Nami naona hivyo hivyo unavyoona wewe ila utamsubiri sana hadi aje kula kwenu kama una imani ni wa kufilisika.Tatizo hata wewe huna cha kukushibisha na kumsaidia mwingine.Buku saba ni kiasi kidogo mno na ukizingatia ni hadi bandiko likubalike Lumumba.Kufilisika kama kutatokea kwa tajiri hakutafanana na kufilisika kwa kapuku na ndio maana wamekwambia kukonda kwa ngombe hakufananishwi na mbuzi.
 
Lazima aisome namba. Alijifanya jeuri kumbe mali zake amezipata kimagumashi
Kama tunsvyoisoma kwenye sukar!!!
View attachment 352381
Waziri Mkuu aliyeshinikizwa kujiuzulu kwa kashfa ya RICHMOND, Edward Ngoyai Lowassa ana hali mbaya kutokana na tishio la mali zake kuanza kunyang'anywa huku pia akiwa ameshauza nyumba yake moja ya kifahari , iliyoko Masaki Dar es Salaam.
Mali za Lowassa ambazo zinaanza kunyang'anywa ili kuerejeshwa serikalini ni ambazo inadaiwa kiongozi huo alizimiliki bila kufuata sheria.
Hili halimhusu Lowassa peke yake, kila mtu ambaye anamiliki mali ambayo hakuipata kihalali lazima irejeshwe, alisema mjumbe mmoja wa Baraza la Mawaziri ambaye aliomba jina lake kutotajwa.

Habari zinasema kuwa kati ya misukosuko ya kisiasa ambayo amekutana nayo katika mwaka uliopita ni pamoja na kuuza nyumba yake ya kifahari , iliyoko Masaki, Dar es Salaam.

Tishio la kuanza kunyang'anywa mali , limefuatia baada ya hotuba ya Katibu Mkuu mstaafu wa CCM , Luteni Yusuf Rajab Makamba kuwa Lowassa anamiliki mali nyingi za Umma.
Makamba alisema wakati wa Kampeni za mwaka jana kuwa zipo ranchi nyingi zilizokuwa za taifa, Lowassa alizigeuza na kuzifanya mali zake binafsi. Huyu Lowassa tatizo lake kubwa ni mtu asiyeaminika. Hata wakati wa Mwalimu Nyerere , tatizo la Lowassa lilionekana na kuwa na mali ambazo siyo halali, alisema Makamba.


Source: Mwana Habari

HIzo mali zake hazina majina?
 
Mwalimu Nyerere alisema hivi: Mtu akikwambia kitu cha kijinga huku akitambua kwamba anakwambia ujinga na wewe ukaukubali kuwa ni ukweli anakudharau sana. Kataeni kuambiwa na kukubali ujinga.
 
Sishangai kuona Tz ni nchi pekee inayofanya biashara vizuri sana ktk vyombo vya habari na mitandao ya jamii coz watu wanapenda sana umbea . Tz let's change jamani yapo mengi ya kufanya ktk hii nchi na dunia kwa ujumla...........it's so sad
 
Kuna kigogo mmoja mkubwa kwenye Idara fulani tuliambiwa ana miliki nyumba 40 Dsm pekee na shamba zaidi ya heka mil. 1.
Hata huvyo bado anadunda ofisini bila hata kuchunguzwa. Nadhani huu utumbuaji wa majipu umelenga baadhi ya watu kulingana na maeneo wanapotoka. Double standard kwenye kutumbua majipu itasababisha zoezi lishindikane kutekelezeka.
 
Si mlisema ametenga bilioni 200 kupanga mkakat wa 2020...mbona hamueleweki?
Kwani habari zote zinatoka chanzo kimoja? Kama unaubongo taarifa hizi hazikupi shida. Wasiawsi wangu ni kwa wewe uliye na uti wa mgongo pekee. Maana mchango wako waonyesha hofu uliyonayo.
 
Nami naona hivyo hivyo unavyoona wewe ila utamsubiri sana hadi aje kula kwenu kama una imani ni wa kufilisika.Tatizo hata wewe huna cha kukushibisha na kumsaidia mwingine.Buku saba ni kiasi kidogo mno na ukizingatia ni hadi bandiko likubalike Lumumba.Kufilisika kama kutatokea kwa tajiri hakutafanana na kufilisika kwa kapuku na ndio maana wamekwambia kukonda kwa ngombe hakufananishwi na mbuzi.
Mipasho kibaooo, ila hali ya mzee wetu ni tete, sasa hatujui mkwanja wa kusuuza roho za wana chadema 2020 zitatoka wapi? Maana kila penye ufisadi tinga tinga limebomoa na kujenga upya, kila penye mfereji tinga tinga limesomba kokoto na kujaza na kuzuia kabisa wizi, sasa ataponea wapi?
 
Lazima aisome namba. Alijifanya jeuri kumbe mali zake amezipata kimagumashi
Hiyo jeuri ya kuchukua nyumba ya lowasa ni hekaya za abunuwasi hakuna mwenye jeuri hiyo maana hizo nyumba hii mibabu yetu mijizi yote inazimiliki
 
Back
Top Bottom