kalulukalunde
JF-Expert Member
- May 27, 2016
- 1,056
- 1,083
Waziri Mkuu aliyeshinikizwa kujiuzulu kwa kashfa ya RICHMOND, Edward Ngoyai Lowassa ana hali mbaya kutokana na tishio la mali zake kuanza kunyang'anywa huku pia akiwa ameshauza nyumba yake moja ya kifahari , iliyoko Masaki Dar es Salaam.
Mali za Lowassa ambazo zinaanza kunyang'anywa ili kuerejeshwa serikalini ni ambazo inadaiwa kiongozi huo alizimiliki bila kufuata sheria.
Hili halimhusu Lowassa peke yake, kila mtu ambaye anamiliki mali ambayo hakuipata kihalali lazima irejeshwe, alisema mjumbe mmoja wa Baraza la Mawaziri ambaye aliomba jina lake kutotajwa.
Habari zinasema kuwa kati ya misukosuko ya kisiasa ambayo amekutana nayo katika mwaka uliopita ni pamoja na kuuza nyumba yake ya kifahari , iliyoko Masaki, Dar es Salaam.
Tishio la kuanza kunyang'anywa mali , limefuatia baada ya hotuba ya Katibu Mkuu mstaafu wa CCM , Luteni Yusuf Rajab Makamba kuwa Lowassa anamiliki mali nyingi za Umma.
Makamba alisema wakati wa Kampeni za mwaka jana kuwa zipo ranchi nyingi zilizokuwa za taifa, Lowassa alizigeuza na kuzifanya mali zake binafsi.
Huyu Lowassa tatizo lake kubwa ni mtu asiyeaminika. Hata wakati wa Mwalimu Nyerere , tatizo la Lowassa lilionekana na kuwa na mali ambazo siyo halali, alisema Makamba.
Chanzo: Mwana Habari
Siasa siasa siasa, ukiwa unapenda kulazimisha mambo katika mchezo huu, utajikuta upo hoi bin taabani . Na mwisho wa siku utajikuta ukiwa umechanganyikiwa, Hakika urais hutoka kwa Mungu.