LOWASSA hana sifa za uongozi, ni mwanasiasa mwenye uchu wa madaraka.
Nimefuatilia mahojiano kadhaa ya Ndg.Lowassa kabla na baada ya uchaguzi mkuu (2015) kila mara akihojiwa akekuwa akiongelea kuhusu azma yake ya kugombea uraisi na jinsi gani anaweka mikakati kabambe ya yeye kuhakikisha anashinda au chama chake kinashinda bila ya kutoa mikakati ya kuondoa umasikini,rushwa nk.
Safari ya Matumaini (akiwa CCM);
Kipindi hiki alikuwa akiomba ridhaa ya kupeperusha bendera ya CCM, kila alipopita maneno aliyoyazungumza ni ‘’mafuriko hayazuiliwi kwa mikono’’..hii ilitokana na kwamba alikuwa na uhakika kawanunua wajumbe wengi ndani ya CCM na upande mwingine alitengeneza maigizo ya ’wachungaji’,’masheikh’,’wanafunzi’ nk ambao walijenga taswira ya kuwa ‘wametumwa na watanzania wengine’..hiki ndicho kipindi kabla hajaikodi CHADEMA rasmi, wanaCHADEMA walimpinga kwenye mitandao yote ya kijamii wakionyesha ni jinsi gani ananunua uongozi kwa kurubuni wananchi…..mara nyingi alizunguka na wapiga ramli na ‘’manabii’ ili kufanya propaganda huku akiacha kuzungumzia mambo muhimu ya kitaifa hasa kansa ya ufisadi.Mara nyingi kila mkoa aliopita alizungumza kwa hofu ‘’ mafuriko hayazuiliwi kwa mkono,Mzee Mangula hatanikata niungeni mkono’’…dhahiri alijua anakiuka masharti na kumhadaa Mzee Mangula ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya nidhamu na Makamu mwenyekiti CCM Bara.
Safari ya Mabadiliko (CHADEMA)
Ghafla baada ya ‘kukatwa’ CCM akaikodisha CHADEMA na vyama vitatu (NCCR,CUF na NLD) na kuuziwa nafasi ya kugombea urais sasa kwa kutumia wapiga ramli, masheikh na ‘manabii’ waliendelea kutengeneza mazingira na propaganda kuwa bila yeye kuwa Raisin chi ingeangamia na watu wangekufa sera yake kuu ikawa ‘sitafukua makaburi’…tafsiri rahisi ni kuwa kama uliiba hatajishugulisha na wewe kila mtu afanye yake…akaendelea ‘siatfuatilia mtu,nitahakikisha kila mtu anakuwa tajiri’…fanya yako yeye hatojishughulisha, kimjini wanasema ‘’kila mbuzi ale urefu wa kamba yake.
Baada ya Uchaguzi (wananchi wamemkataa kwenye kura)
Kwa sasa kila napoenda kuhojiwa na waandishi wa habari na mkutano wa CHADEMA yeye akili yake ni uchaguzi wa 2020; yeye anaangali mazingira yoyote yale ili awe raisi, mipango ya kuhakikisha kizazi kijacho wananufaika na rasilimali sio kipaumbele chake,amejawa ubinafsi. Kila akihojiwa hupenda neno ‘’tirany of numbers’’ yaani kinachomsumbua ni jinsi gani atakuwa na idadi ya kura za kutosha awe raisi mwaka 2020 au 2025, hajishughulishi na chochote,yeye anafanya kampeni tu,wahariri wa magazeti wananufaika naye kwani anataka naye kila siku gazeti linukuu kauli yake. Mtaalamu mmoja marekani aliwahi kusema,nanukuu kwa umeombo ; ‘A politician thinks of the next election; a statesman thinks of the next generation’. ~James Freeman Clarke, Sermon.