Siasa za upinzani bila kujitoa ufahamu na kujiona upo juu ya sheria za nchi huwezi kupata kick kirahisi. Ukivunja sheria za nchi kwa kufanya fujo, ukakamatwa na polisi, ukaswekwa rumande na kufungulia mashtaka mahakamani ndo unakuwa umehitimu shahada ya juu ya siasa za upinzani.
Baada ya kupambana na jeshi la polisi na mahakamani ataibuka yule jamaa mwenye mdomo mkubwa kama chapat toka singida au yule jamaa mwenye jicho la kengeza toka hai kuhalalisha uvunjaji huo wa sheria kwa neno la kawaida tu ‘viongozi wa upinzani wanahujumiwa na serikali kwa kuwasweka rumande’ na ‘demokrasia inaminywa’.
Juzi Lowassa nae kaanza kujitoa ufahamu, kaanza kuvunja sheria na taratibu za nchi yetu, anafanya mikutano holela na bado yeye na chama chake wanataka wasikamatwe wala wasihojiwe kwa uhuni wanaoufanya.
Binafsi nawapongeza sana jeshi la polisi kwa kusimamia vema sheria za nchi yetu na kutekeleza kwa vitendo bila hofu wala uwoga misingi ya taifa letu na katiba yetu “binadamu wote ni sawa na hakuna mtu aliye juu ya sheria”. Ila siku juzi mlinikera sana jeshi la polisi mkoa wa Geita kwa kumwachia yule jamaa bila kumweka ndani hata siku moja ili kumkumbusha misingi ya sheria ya nchi yetu.
Jana nimemsikia mbowe akilaani vikali kukamatwa kwa lowassa, hee!!!!, ivi Lowassa au mbowe au chadema wana hatimiliki ya kuvunja sheria za nchi?.
Jeshi la polisi endeleeni kuhakikisha nchi yetu inaongozwa kwa misingi ya kisheria, msiogope makelele ya makengeza wala domo chapatti, watanzania wanyonge mnaotulinda kila siku tupo nyuma yenu na kuwaombea sana.
Chapeni kazi naowaombeni mkimkamata tena Lowassa anavunja sheria mpelekeni kisongo wakatiane moyo na yule nabii hewa.