kwa mujibu wa TBC ni shule ya kiislamu ipo kigamboni ila imepewa jina la kikristo yani EDWARD LOWASSA ISLAMIC SCHOOL kweli pesa si mchezo..
kwa mujibu wa TBC ni shule ya kiislamu ipo kigamboni ila imepewa jina la kikristo yani EDWARD LOWASSA ISLAMIC SCHOOL kweli pesa si mchezo..
Mbunge wa Monduli, Mh. Edward Lowasa amemchangia Mufti Mkuu wa Tanzania sh 13 mil kwaajili ya kukamilisha ujenzi wa kituo na shule ya watoto yatima kilichopo Kigamboni jijini DSM. Mbunge huyo amemkabidhi Mufti fedha hizo leo akisema amezipata kutoka kwenye michango mbalimbali ya marafiki zake ili kukamilisha ujenzi wa kituo na shule hiyo itakayojulikana kwa jina la Edward Lowasa.
Source ni TBC1
Mkuu siku hizi mimi nasema "uvivu na uzembe havina adabu". Kwanini? Matukio mengi yanayoitwa "shida" hapa Tanzania ni matokeo ya uvivu na uzembe.Mkuu shida haina adabu.
Kweli pesa sio mchezo, fikiria unakutana na...Rostam Aziz Catholic High School au Bin Laden Anglican Teachers College
Nafikiri hii inawezekana kwa Tanzania tu
Mh! Ni akina nani hao marafiki?Mbunge wa Monduli, Mh. Edward Lowasa amemchangia Mufti Mkuu wa Tanzania sh 13 mil kwaajili ya kukamilisha ujenzi wa kituo na shule ya watoto yatima kilichopo Kigamboni jijini DSM. Mbunge huyo amemkabidhi Mufti fedha hizo leo akisema amezipata kutoka kwenye michango mbalimbali ya marafiki zake ili kukamilisha ujenzi wa kituo na shule hiyo itakayojulikana kwa jina la Edward Lowasa.
Source ni TBC1
Yote tisa, kumi ajivue gamba. Nchi hii iko hivi ilivyo kwa ajili yake. Umeme huoooooooooooooooooooooooooooo kwa ajili yake. Pokeeni lakini mjiulize fedha hizo alizipata wapi wakati alikuwa mwajiliwa wa serikali. Mufti usipokee hela za mashaka au (wizi) !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Shule hiyo ilianza kujengwa mwaka 2006 na ilipewa jina hilo akiwa waziri mkuu. Tangu wakati huo wameshindwa kuimalizia na Mufti anasema walikuwa wanahijati sh 13mil tu kumalizia. Baada ya msaada huo, wataweza kuikamilisha na wanatarijia kuanza kazi mwakani!
Mimi binafsi sina tatizo na msaada uliotolewa na Mhe. EL, hofu yangu ni jinsi fedha hizo zilivyopatikana. Tunahitaji maelezo ya kutosha marafiki zake wapi waliotoa hizo fedha vinginevyo tutaendelea kuamini kuwa fedha hizo ni mazao ya fisadi mablimbali ambazo Mhe. EL anatuhumiwa nazo. Tukumbuke kuwa Tsh. 13m/- sio mchezo kuzipata hivi hivi tu, kuna watu huwa wanafanya harambee kisha wanaambulia milioni 1 taslimu na ahadi milioni 2!
Hili la jina naona amekwenda mbali; waisilamu walivyo 'sensitive', Mufti asipoangalia hiyo shule anaweza akasusiwa na waumini wake.
Mh! Ni akina nani hao marafiki?
Your are out of your mind to support this donation, this is a guy who is holding this country in ransome.Huo ndio uungwana, ulichonacho unagawana na wengine.
Big up Ole Lowassa!