Lowassa akumbukwa

Hakuna anayemkumbuka Huyo Mroho wa madaraka. Nchi imepata nafuu kwa kushindwa kwake! Nchi ingekuwa matatizoni.



Hatimae wananchi wameanza kukiri heri wangemchagua Lowassa kuwa rais huenda angewahurumia katika bomoabomoa inayoendelea.

Wadau hii maana yake nini?

Chanzo: Tanzania Daima
 
John Magufuli anaangalia mbali sana, nadhani hakukosea kutojenga urafiki wa wafanyabiashara kipindi kile CCM inafanya kampeni. Hakutaka kuiangalia Tanzania yenye kuwafaidisha wachache na kuwasahau walio wengi. Hata ile jeuri ya kuwaambia watu hakuna kwenda nje ya nchi, imetokana na yeye mwenyewe kujiamini katika uadilifu alionao. Rais tajiri mwenye hisa nyingi kwenye mabenki na makampuni makubwa ya kimataifa atapata wapi jeuri ya kuwaambia watu wasiende nje ya nchi?. JPM mpaka sasa keshaweza kuzidhibiti tamaa binafsi za utajiri, kwake walio wengi wanaporidhika basi wale wachache hawawezi kumnyima usingizi.
 
Hatimae wananchi wameanza kukiri heri wangemchagua Lowassa kuwa rais huenda angewahurumia katika bomoabomoa inayoendelea.

Wadau hii maana yake nini?

Chanzo: Tanzania Daima
They are very wrong,time is the best judge let's be patient.
 
Ukitaka kujua lowassa anakumbukwa nenda kwenye page ya eatv ucheki comments za watu khs wastara kubomolewa nyumba zake 2,ndo utajua watu wanamkumbuka lowassa kinoma
 
Ukitaka kujua lowassa anakumbukwa nenda kwenye page ya eatv ucheki comments za watu khs wastara kubomolewa nyumba zake 2,ndo utajua watu wanamkumbuka lowassa kinoma
Kweli aisee maana lowasa angewaacha tu wateketee..si jeuri yao wenyewe..ye anaishi masaki..lakini lowasa si kipaumbele chake kuifanya miji ya tz iwe na muonekano wa kuvutia maana yeye tayari ana mji wake ktk jiji la London.
 
Hapa kazi tu ndio habari ya mjini hizo siasa zenu za vyama sijui kusifia sifia watu na kushabikia ujinga tupa kule ......
 



Hivi Magufuli ametaja mali zake?
Mana hatutaki unafiki na visasi tunataka dhamira ya kweli.

Ni jambo baya sana kushangilia udhalimu wanaofanyiwa wazee na watoto wa watanzania wenzetu ambao wengi wao ni maskini wakutupwa wanaobomolewa nyumba zao na kuachwa wakilala nje.
Ni laana kubwa kuwafanyia unyama wazee na akinamama na watoto eti wamejenga mabondeni.
Je ni kwa nini mji mzima wa Dsm usibomolewe kwa kuwa ni maeneo karibu yote yamejengwa bila kupimwa.
Serikali ya CCM ilikua wapi?
Na je CCM wote walikua ni mataaira isipokua Magufuli peke yake ndio amekuja kuwazindua?
Au kwa sababu maeneo mengi ya jiji ccm ilikosa kura mwaka jana?
Ni kwa nini wazee wanaotaabika kwa kuvunjiwa nyumba wasingeheshimiwa kama watu dhaifu?
Ndio maana CCM na serikali yake ilishindwa kudhibiti mauaji ya albino kwa sababu ya kukosa huruma!

Kuna ugumu gani kwa serikali ya CCM kutumia pesa inazokusudia kuinyang'anya CUF ushindi wake kwa kurudia uchaguzi uliofanyika na kumalizika kwa amani kwa kuzitumia kwenye kuwasaidia wazee wetu kwa kuwajengea nyumba hata vyumba viwili kwenye eneo lililopimwa na kisha kuwatoza kodi ndogo ya nyumba,hata sh. 5000 tu kwa mwezi ili waweze kuishi kama hao maprofesa wanaoonekana kuwa ndio binadamu ilihali ndio walitumika miaka nenda rudi kuihujumu nchi?

Je, hao waliojenga mabondeni wangejenga wapo wakati watu wachache waliowahi kushika madaraka kwenye serikali za CCM wamejimilikisha kila eneo zuri na nyumba za umma?
Je,ni kwa nini wasianze na ofisi za CCM ambazo zimejengwa bila kufuata ramani?

Hivi Serikali imeshindwa nini kutumia majeshi yetu, makuruta wa JKT na wafungwa kujenga nyumba hata laki moja kwa gharama ndogo sana kwa ajili ya wazee na wakina mama na watoto walioko mabondeni? Kisha wakalipa kodi ya sh. 5000 - 10,000/-?
Je, pangekua na vita ni sh.ngapi zingetumika?
Iweje tushindwe kutumia majeshi yetu kuhudumia jamii kwenye nchi ya amani kama TZ?
Au CCM inataka kinuke kule Zanzibar itumie mamilioni ya pesa kupeleka majeshi kule kuweka serikali kwa udhalimu wa kuua demokrisia. Je,itasaidia nini kumwona Shein yuko Madarakani kwa gharama za watanganyika wakati baba zetu na mama zetu na watoto wetu wanalala nje kwa ku unjiwa vijumba vyao tena kwa uzembe wa serikali wa kushindwa kutimiza wajibu wake wa kupima viwanja na kuweka wazi matumizi ya ardhi?

Kila sheria inayotungwa inapaswa kutekelezwa kwa kujali kwanza ustawi wa watu wake sio kuufanya wengine wafe kwa makosa na uzembe wa watawala na chama kile kile kilichosababisha uzembe huo.

CCM na Serikali yake walipaswa kwanza kuwaomba watanzania msamaha kwanza ndipo waanze kuwabomolea nyumba zao?

Kama Serikali ya Magufuli na CCM yake wameamua kuwaadhibu wote waliovunja sheria basi isiishie kwa wazee na akina mama na watoto waliojenga mabondeni kwa umaskini wao bali wawaadhibu wote mpaka wale waliofoji vyeti ambao wako kwenye ajira na wanaendelea kuhurumiwa na kutumbua mishahara ilihali masikini hawahurumiwi. Hatusikii mtu ndani ya CCM akiseme au kushauri kwamba wote waliodanganya kwenye ajira wavunjiwe ajira zao kama wazee wetu wa mabondeni!!

Hii inakuaje kujipatia umaarufu kwa kuwaadhibu na kutesa walalahoi na kuwaacha watu wanaokaa kwenye maofisi yenye viyoyozi kwa vyeti batili wakiendelea kutanua?

Kama busara inatumika basi itumike kwa wote.
 

yaan umeandika mengiii ila pumba tupu, hiv umesoma kwanza kabla ya kupost?? umekuwa kama una kimbizwa,,,
 
Kwa kweli wewe ni mzalendo unayependa kuona mabadiliko ya ukweli nakupa big up. Watanzania wengi tuna ugonjwa wa siasa hata kwenye mambo ya msingi. Congratulations comrade
 
yaan umeandika mengiii ila pumba tupu, hiv umesoma kwanza kabla ya kupost?? umekuwa kama una kimbizwa,,,
Umenena. Hivi magufuli kutaja mali zake kuna uhusiano gn na watu kuvunja sheria? Watu wanaharibu mazingira . Wamejenga kwenye vyanzo/mikondo ya maji mafuriko yakiwakumba lawama kwa serikali. Watanzania tuna matatizo. Mji hauleweki ni wp duniani watu wsnaruhusiwa kujenga mabondeni? Ubishi mwingine hauna tija. Mara ngp watoto/watu wanaopolewa kwenye mafuriko. Jamani siasa mbuzi ndio zimetufikisha hapa.
 
Lakini kweli jamani viongozi wetu wamehodhi ardhi kubwa sana
 
We chukulia zile za sumaye za magwepande walisema ni hekali30
 
Magufuli hawezi kuleta nafuu yoyote ya kimaisha kwa wananchi, msoto utaendelea kama kawa na watu watajuta kumchagua na baadhi wameshaanza kuona madhara ya kukurupuka kwake. Hana uwezo wa kuisogeza nchi mbele kimaendeleo, muda utaongea. Mpaka sasa hakuna chochote cha maana alichofanya zaidi ya kuvunja nyumba za wananchi wake na kufukuza kazi watumishi bila kufuata sheria, mambo ambayo hayamsaidii mwananchi wa kawaida anayeumizwa na mfumuko wa bei.
 
1000digits kuna wimbo mmoja Bushoke Junior anasema wanayataka mapinduzi na mapinduzi hawayawezi....tafuta hiyo nyimbo, ujumbe wake ni mmoja tu, hakuna mabadiliko yasiyokuwa na gharama. Umeandika meeengi sana lakini tambua ukweli mmoja tu, haiwezekani watu waishi kwa kuzingatia taratibu za kizamani halafu wakapata maendeleo ya kisasa. Mtanzania hawezi kuishi kwa tamaduni zake, kwa hulka zake halafu akayafikia maendeleo waliyonayo wengine. Hakuna kitu kama hicho, machungu lazima yatukute ili tuweze kuvuka kipindi hiki. Inauma mtu anabomolewa nyumba aliyoijenga kwa jasho, lakini ni lazima tufike mahali kwa ujumla wetu tukubali kurudi katika njia iliyonyooka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…