Lowassa akirudi CCM, Dkt. Slaa atasemaje?

Lowassa akirudi CCM, Dkt. Slaa atasemaje?

Wakuu habari za asubuhi,

Nimejiuliza swali hilohapo juu, sababu wote tunafahamu kilicho muondoa Dr. Slaa CHADEMA.

Kwa kauli yake Dr. Slaa ni kwamba yeye alijitoa CHADEMA sababu alikuwa ndie aliemtangaza Lowassa katika list of shame, na hakuwa na jinsi ya kumsafisha. Sasa ikitokea akakarudi CCM ningependa kusikia Dr. Slaa anamzungumziaje Lowassa.

Ngoja nisubiri kuona kuna kitu kingine nataka kujifunza hapa.
DR. Slaa atasema chumba cha kulala kumesafishwa na sio choo tena
 
Kuna uwezekano mkubwa Dr. Slaa akakutana tena na Lowassa na kipindi hiki wote wakiwa makada wa CCM. Ninajiuliza Dr. Slaa atakimbia tena?

Na je ufisadi Lowassa bado upo?

Rais Magufuli anaamini Lowassa ni msafi kuliko yeye kwenye siasa, amekiri mwenyewe, je huu ndio wakati wa kukiri makosa yetu?

Je, CHADEMA walikuwa sahihi kuwa wa kwanza kumsafisha Lowassa?

Kwenye mtandao msimamo utabadilika na kuanza kuimba wimbo wa Rais Magufuli kuwa Lowassa ni msafi?

Karibuni
 
Yote yanawezekana maana wote hao walikuwa wanaccm kwa hiyo kurudi tena huko sio jambo geni na usishangae Zitto kurudi Chadema Siasa ya Afrika ni ya kinafiki.
 
Ufisadi unabakia chadema ndiko kunako mto yordani...ukichafuka unaenda kuoga.
 
kwanini mnamgeukia Dr. Slaa hivi mmesahau matusi mliyomtukana wakati anaondoka Chadema leo yeye na Lipumba anawaumbua kwa mtu yoyote mwenye akili anajua kuwa Lowassa hakwenda Chadema kwa sababu yeye ni muumini wa mageuzi bali alienda huko kwa sababu ya hasira za kukatwa na ccm sasa picha yake inaanza kujionyesha na huu ndio mwanzo wa kuporomoka upinzani kwani hivi vyama vimepoteza imani kwa wananchi
 
Kwani Dr Slaa anaenda kufanya kazi na Lowasa ama Magufuli.?

Makanda bwana gia ya angani itawatesa sana.
Magufuli hana kazi kama mtu binafsi kazi zipo za serikali ya CCM ama za CCM. Hata Dr Slaa hana ugonvi na Mbowe alikuwa na ugonvi na CHADEMA kama taasisi kumpokea Lowasa.
 
Wakuu habari za asubuhi,

Nimejiuliza swali hilohapo juu, sababu wote tunafahamu kilicho muondoa Dr. Slaa CHADEMA.

Kwa kauli yake Dr. Slaa ni kwamba yeye alijitoa CHADEMA sababu alikuwa ndie aliemtangaza Lowassa katika list of shame, na hakuwa na jinsi ya kumsafisha. Sasa ikitokea akakarudi CCM ningependa kusikia Dr. Slaa anamzungumziaje Lowassa.

Ngoja nisubiri kuona kuna kitu kingine nataka kujifunza hapa.
atasema kinyesi kimerudi chooni, kutoka sebuleni
 
Wakuu habari za asubuhi,

Nimejiuliza swali hilohapo juu, sababu wote tunafahamu kilicho muondoa Dr. Slaa CHADEMA.

Kwa kauli yake Dr. Slaa ni kwamba yeye alijitoa CHADEMA sababu alikuwa ndie aliemtangaza Lowassa katika list of shame, na hakuwa na jinsi ya kumsafisha. Sasa ikitokea akakarudi CCM ningependa kusikia Dr. Slaa anamzungumziaje Lowassa.

Ngoja nisubiri kuona kuna kitu kingine nataka kujifunza hapa.
Hana cha kufanya kwa7bu yy kwa sasa c mwana siasa bali ni mtumishi wa serikali nje ya Tanzania
 
Back
Top Bottom