Lowassa aibua mjadala mzito | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lowassa aibua mjadala mzito

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Oct 22, 2011.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Oct 22, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  Mwandishi wetu
  KAULI za Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, kuhusu tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana nchini, imepokelewa kwa hisia na mitazamo tofauti, huku baadhi wakihoji kuhusu sababu za yeye kujitoa katika lawama za utekelezaji mbovu wa mipango ya maendeleo unaofanywa na serikali ya chama chake.

  Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia alisema kuhusu tatizo la ajira, Lowassa ameongea jambo la kweli.Mbatia alisema si jambo la kuficha kuwa nchi sasa imekalia bomu la idadi kubwa ya vijana kukosa ajira.

  Alisema ajira 700,000 kila mwaka zilizoahidiwa na serikali ya Rais Jakaya Kikwete zimegeuka kuwa hewa huku idadi ya vijana wanaoingia katika soko la ajira, ikiwa inaongezeka kila mwaka.

  "Yapo ambayo Lowassa kaongea ukweli, tatizo la ajira kwa vijana ni bomu ambalo kama lisipoangaliwa kwa umakini linaweza kulipuka wakati wowote. Hilo si jambo la kuchezea," alifafanua Mbatia.

  Hata hivyo, Mbatia alimkosoa Lowassa kwa kuzungumza mambo hayo nje ya vikao vya chama wakati yeye ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM.

  Kwa mujibu wa Mbatia, kitendo cha Lowassa kuzungumzia tatizo la ajira nje ya vikao vya chama ni sawa na kuishataki serikali ya chama chake kwa wananchi, ili waamue wanavyotaka.

  Alifafanua kwamba, alichofanya Lowassa ni kuwaambia Watanzania kwamba serikali ya CCM imeshindwa kutimiza ahadi yake ya kuzaisha ajira 700,000 kwa vijana na sasa wananchi wanaweza kuihukumu.

  "Wasianze kutupiana mpira ili huyu aonekani msafi na yule mchafu. Wote ndani ya CCM wameshindwa kuongoza nchi. CCM ni chama dola sasa dude hili limeelemewa na mambo, limeshindwa kutimiza malengo yake, alisema.


  Alisema malumbano hayo ni ishara ya CCM kuelekea kuanguka hata kabla ya uchaguzi mkuu wa 2015, kwani kuna kila dalili chama hicho sasa kiko katika hali mbaya kunakotokana na ukosefu wa utengamano wa kisiasa.

  Mbatia alisema siku zote CCM imekuwa ikijiendesha kwa kutegemea nguvu za dola ikiwemo Idara ya Usalama wa Taifa, lakini sasa hivi kioanekana kuelemewa na mzigo na ndiyo maana, kimeanza kumgeuka na kuongeza:, "ni ishara CCM haifiki 2015'' .

  Wananchi nao walonga

  Kwa upande wake, mkazi wa Mafinga mkoani Iringa, aliyepiga simu katika chumba cha habari cha gazeti hili na kujitambulisha kama Mzee wa Vitabu Tanzania alisema, Lowassa ameshindwa kujibu hoja za msingi za tuhuma zinazomkabili.

  Kwa mujibu wa mzee wa Vitabu, Lowassa alichofanya ni kujiwekea kinga ya kutoguswa na vyombo vya habari na hivyo kufanya Watanzania wasiweze kujua tuhuma zinazomkabili sasa na katika siku za usoni.

  “Lowassa alipaswa kueleza Watanzania kuhusu ukweli wa tuhuma za kuleta kampuni ya mfukoni ya Richmond na si kutishia kushtaki waandishi watakofichua mambo yake,” alisema .


  Mkazi mwingine wa Mafinga aliyepiga simu na kujitambulisha kuwa ni Godson Sanga, alisema Lowassa angefanya jambo la maana sana kama angejibu tuhuma za kuhusika katika kuleta Richmond.

  Kwa mujibu wa Sanga, Lowassa hakuna jambo jipya na la msingi alilowaambia watanzania kwani ameshindwa kujibu tuhuma za msingi badala yake akatangaza vitisho dhidi ya vyombo vya habari na waandishi.

  "Nawasihi msiogope kuandika kama ana maovu, endeleeni kuandika. Sisi jana (juzi) tulikaa tayari tukitegemea angesema jambo kuhusu tuhuma za kuhusika na Richmond. Sasa yeye anakuja kutisha watu akisema wanamchafua kwa nini,” alisema.

  CUF
  Kwa upande wa CUF, chama hicho kimesema matamko mbalimbali ya viongozi wa CCM ni mwendelezo wa mipango na mikakati ya kuandaa kundi litakalosimama na kuhakikisha inarudi madarakani mwaka 2015 kama jinsi walivyomtumia Magufuli kuinadi CCM Igunga.

  ":CCM haiwezi kurekebishika na kuwa chama cha kuwasaidia watanzania kuvuka kutoka kwenye umasikini ,ukosefu wa ajira,mifumuko mikali ya bei, kukosekana umeme wa uhakika na hata kupunguza matatizo mbalimbali yanayoikabili jamii ya kitanzania ikiwemo migomo ya wafanyakazi na wanafunzi nk," alisema Shaweji Mketo Naibu Mkurugenzi wa Oganaizesheni, Uchaguzi na Bunge wa chama hicho.

  Chanzo:Gazeti la Mwananchi
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Oct 22, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,759
  Likes Received: 82,756
  Trophy Points: 280
  Naam Magamba kipo ICU kikisubiri kukata roho tu, itakuwa poa sana kama kitasambaratika kabla ya 2015.
   
 3. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #3
  Oct 22, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Wana JF mtanisamehe.... yani siku hizi nikisikia media inavyowapa promo wanasaisa uchwara najisikia kupasua nyumba kabisa

  the guys are just craps... hivi hoja ya ajira kweli kaibua lowassa??? hata bibi yangu kule kijijini anajua watu hawana kazi... and then wanam-quote Mbatia

  aisee waandishi wamekua wengi ahdi wameamua kuandika tu chochote kinachohusu mtu,

  BASI NIWAUZIE SIRI, MNAWEZA KUUZA MAGAZETI HATA MKIZUNGUMZIA VIUNGO VYA MWILI AU HATA AINA ZA MAUA, NI NAMNA TU MTAKAVHODRAMATIZE
   
Loading...