Waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa amehudhuria kusimikwa wakufu kwa Askofu mkuu wa kanisa Anglikana la Kenya Arch Bishop Jakson Ole Sapit leo jijini Nairobi. Ibada hiyo imehudhuriwa pia na rais wa Kenya Kenyatta na makamu wa rais wa nchi hiyo Wiliam Rutto.
Kutoka Tanzania kanisa Anglikana limewakilishwa na baba Askofu wa dayosisi ya Mpwapwa ambaye pia ndiye aliongoza mahubiri. Lowassa amekutana na viongozi wakuu wa Kenya na kufanya mazungumzo ambayo hata hivyo hayajawekwa wazi.