Lowasa na Sumaye wanapewa vitu vifuatavyo maisha yao yote ( Na Serikali ya CCM ) :-
1. Usafiri
2. Ulinzi ( mkali )
3. Wafanyakazi
4. Malazi
5. Chakula
6. Mshahara ( 80 %)
7. Mavazi
8. Mawasiliano
Tuchane na siasa za 2015, siasa za kufuata upepo na zilizokwisha pita na wakati.
Wewe upo huko Naliendeli, Ngudu na huko kwingineko unajivunia ukamanda wako eti upo na Lowasa , Sumaye kwenye safari ya mabadiliko.
Huna mbele wala nyuma unafuata mkumbo ( hasa huku mitandaoni). Unajua Mbowe anavyoramba ruzuku ya CHADEMA ?
Ukapimwe akili.
Kuendesha Chama kihuni chenye wapiga kura mil. 6 ni tatizo kubwa sana.
Huoni bahati kubwa kwa chama kuwa na watu wa hadhi na wenye maana kama Lowasa na Sumaye?
Sumaye hata akiwa jukwaani unatamani kumsikiliza?
Ngoja niwafundishe hekima ,maarifa na busara za siasa mana naona kuna uhaba mkubwa sana kwenye vyama vya upinzani!
Ukiwatoa wazee wenye Busara kama Prof. Baregu,Prof. Safari, Lowassa, Sumaye, Mahanga, na wazee wengine Chadema kitakua kama kikundi cha waendesha Bodaboda wanaomvamia dereva wa VX V8 baadae ya dereva mwenzao kuendesha bila kufuata sheria kutokana na kutokujua sheria na kugonga VX la watu kisha maderva wa boda boda kukusanyika na kumzonga dereva mahiri wa VX huku wakiona wao wanaonewa.
Hivi huoni kuwa Mtu kama Kadinali Pengo au Askofu Shoo kiwa na jambo la kuzungumza au kuwashauri Chadema ni rahisi kabisa kumtafuta Sumaye au Lowasa na sio wahuni huni wengine wenye jaziba hata kwa mambo yanayohitaji maarifa na busara.
Nyerere alikuwa alisomeshwa na serikali ya mkoloni ,akawa mtumishi wa serikali ya mkoloni, akawa waziri mkuu wa serikali ya Mkoloni lakini alikuja kuungana na watanganyika wenzake kudai Uhuru na Uhuru ukapatikana ,sasa kama waafrika wangembagua kwa sababu tu aliwahi kuitumikia serikali ya mkoloni ingekua sio jambo la busara na maarifa.
Sitaki kuwafundisha namna ya kuwatumia Akina Lowasa na Sumaye kujenga chama tena kwa kasi sana. Ngoja nikae kimya ili zoezi la kumwachia Lema na Mbowe Chama liendelee kwa ufanisi.