Lowasa amefanya nini kwa wanaMonduli?

Lowasa amefanya nini kwa wanaMonduli?

Dopas

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2010
Posts
1,151
Reaction score
392
Sipingani na nia yake ya kutaka kuingia Ikulu kwani ni haki yake ya kikatiba, lakini najiuliza tu kwa muda wote alipokuwa mbunge wa Monduli, kwa nafasi zote alizotumikia serikalini kuna cha pekee ambacho wananchi wa Monduli wanaweza kujivunia nayo? Umaskini anaotaka kuumaliza Tanzania atakapokuwa Rais, amejitahidi kiasi gani kuumaliza kwa wapiga kura wake wa Monduli?

Maswali yanaweza kuwa mengi, ila inafaa kusoma katikati ya mistari. Kama kwa miaka yote aliyokuwa Mbunge wa Monduli hakuonesha jitihada za kumaliza umaskini wa wapiga kura wake wa Monduli, ndiyo tujiaminishe kuwa kwa miaka kumi atakayokuwa Rais atafuta umaskini wa Tanzania?

Baadhi ya viashiria ya umaskini wa hali ya juu wa jimbo la Monduli ni tatizo la maji. Sijasikia jitihada zake kumaliza tatizo hilo, wala kulipatia ufumbuzi wa kudumu. Alikuwa hata waziri wa maji, lakini pita leo barabara ya Arusha -Karatu, utaona akina mama na punda wakisaka maji kwa umbali mrefu.

Nguvu kubwa ya hela inayotumika isingehitajika ikiwa kuna kitu cha wazi alichofanya huko jimboni kwake.

Kama kuna anayefahamu hatua kwa hatua jinsi alivyowatoa wapiga kura wake kutoka dimbwi la umaskini anaweza kulisemea, vinginevyo ni hadithi ile ile ya kuigeuza Kigoma kuwa Dubai, ambazo hadi leo ni ndoto za alinacha.
 
mtoa post umeuliza swali zuri sana Ritz Pasco pitieni mskize hii maneno
 
Last edited by a moderator:
Njoo monduli jionee mwenyewe kazi nzuri iliyotukuka ya Mhe EL Raisi mtarajiwa, then compare to mtama
Mbushunoti ni vizuri tu ukaeleza machache tukafahamu.
Binafsi sipingi kama kuna kitu cha wazi alichopigania kwaajili ya wapiga kura wake wa Monduli. Kwa kifupi tu Lowasa tangu ajiuzulu uwaziri mkuu alibaki bubu bungeni kwa miaka takriban 8, sasa sijui ni wapi aliyasemea mahitaji ya watu wake, walau kwa ndani ya miaka hii 8, bila hata kurudi nyuma sana.

Ninachofahamu ni mali zake binafsi: mahoteli ya kifahari, majumba ya kifahari, na biashara mbalimbali kuanzia Mondoli juu hadi kwingineko.

Kama Mbunge wa Monduli, tukisimamia ukweli nina mashaka kama kuna kitu wapiga kura wake watajivunia nayo, ingawa kwa bahati mbaya kwa miaka yote hawakuona mwingine aliye afadhali.

Monduli naifahamu kwa kiasi kikubwa, japo sio kila kijiji. Naifahamu pia kuwa ni baadhi ya wilaya katika mkoa wa Arusha ambazo watu wake wanaishi kwa dhiki na umaskini wa kutupwa. Ikulu aende tu, sina shida naye. Ila ninachojua ni kuwa hakuna kipya atakacholeta Tanzania, kama ambavyo hakuna kipya alichofanya kwa watu wa Monduli.

Jambo lingine ni Lowasa wa zamani sio wa sasa. Lowasa wa zamani walau alikuwa na nguvu na afya. Ila Lowasa wa sasa amechoka kimwili, japo nia yake ya kwenda Ikulu ni ile ile. Namtakia kila la heri.
 
katika juhudi zangu za kufuatilia na kusikiliza bunge sijamsikia Lowasa kuongea au kuuliza lolote bungeni tangu alipojiuzulu. kama kuna mtu aliyemsikia akiuliza au kuunga hoja mkono atukumbushe ili tuone kama alikuwa anatoa hoja kwa faida ya wananchi au kwa faida yake, ni njia mojawapo ya kumpima kama anaatufaa
 
Yaani siamini macho yangu


Huyu madabida ameisha ua ndugu zetu kibao kwa kuwauzia vidonge feki huku akifurahia mihela wao wakifa. Leo anajua Lowasa akiwa Rais kesi yake itafutwa hivyo anamfananisha na mtume wetu kipindi hiki cha mfungo?


Kweli hela ina nguvu, yaani na sisi waislamu tunaamini kabisa kuwa Lowasa ndio Mtume wetu?


TAKBIIIIR!
 
umewahi kufika monduli....JIBU lako itakuwa hapana, ndo maana ujui...miuondo mbinu safi na maanisha lami,shule za secondari na msingi za kutosha,sehemu kama monduli ni ya jamii ya wafugaji,wanaitaji sana elimu bora na huduma madhubuti za afya zao na mifugo,na hayo kwa monduli yana patikana....Kama kipimo chako cha umasiki ni magorofa na mavogue,basi hata uingereza kuna masikini sawa na monduli..asante...
 
Hakuna kitu mkuu ni utapeli tu ndugu yangu kama ule Wa 2005 maisha bora kila mtanzania...
Yaani siamini macho yangu

Huyu madabida ameisha ua ndugu zetu kibao kwa kuwauzia vidonge feki huku akifurahia mihela wao wakifa. Leo anajua Lowasa akiwa Rais kesi yake itafutwa hivyo anamfananisha na mtume wetu kipindi hiki cha mfungo?

Kweli hela ina nguvu, yaani na sisi waislamu tunaamini kabisa kuwa Lowasa ndio Mtume wetu?

TAKBIIIIR!
 
Njoo monduli jionee mwenyewe kazi nzuri iliyotukuka ya Mhe EL Raisi mtarajiwa, then compare to mtama

Acha uongo hamna kitu. Wapiga kura wake ni wafugaji. Malambo ya kunyweshea mifugo aliyoacha marehemu kipenzi chetu Edward Moribge Sokoine yako wapi? Kwa teknolojia ya sasa na hizo fedha za marafiki zake angeweza kuchimba visima vya maji kila kijiji. Yeye binafsi ni mfugaji mkubwa lkn kiko wapi kiwanda cha nyama au maziwa ili viajiri vijana? Badala yake kiwanda chetu cha maziwa cha Arusha kimeuzwavkwa Uhuru Kenyata na amekigeuza bohari la kiwanda chake cha Brookside! Kuleni pesa yake lkn hamna kitu hapo!
 
Amewaletea mafuriko ama hilo haulioni mkuu?
 
Back
Top Bottom