Hope mistari hii itakusaidia;
Unajua nakuthamini zaidi ya rushwa na posho, bila ya wewe mimi siwezi kuishi ni sawa na kukosa bunduki eneo la tukio, nakuheshimu kama LINDO, wewe ndio IGP wa moyo wangu... mbona uko kimya? nina RB ya penzi lako, nijibu nifungue jarada lako ndani ya moyo wangu. Usifanye moyo wangu ukaenda mbio kama DIFENDA MPYA, nakuhakikishia nitakuwekea usalama kama MSAFARA WA RAIS, usiniweke roho juu kama MAANDAMANO YA CHADEMA!