Love stories

Love stories

tawfiq

Member
Joined
Aug 9, 2014
Posts
16
Reaction score
7
Hi! Guys mimi ni mtunzi wa story mbalimbali zinazohusu masuala ya mapenzi na maisha kwa ujumla!! Je mko tayari niporomoshe kitu cha uhakika?? Na je mtanipa support ya kutosha??
 
K then! Nawaonjesha mautamu kidogo..

The magic ring (introduction)

Ni safari ya msakatonge mimi niliyeamka bila kujua ni kitu gani
nitaingiza kinywani kwa siku hiyo. Nilimuomba Mungu wa viumbe
wote ili anijaalie niweze kupata chakula kwa siku hiyo kwakua siku
zote yeye ndie aliyekua ananipangie nile nini.
Nilitoka mapema sana kwenda kutafuta riziki. Kwakua maskani
kwangu kulikua mbali kidogo na nainapoishi, ilinichukua mwendo kama
lisaa hivi nikikatisha vichochoro vya tandale ili niibukie manzese na
baadae mburahati ambapo ndio kilinge chetu kilikuwepo hapo.
Nikiwa kwenye mwendo wa haraka, nilishtushwa na mlio wa gari
uliokuwa unalia karibu na nilipokuwepo. Nilijua kua ile gari labda
ilikua inataka kukatiza njia, niliamua kusimama ili niipishe ipite.
Lakini cha ajabu haikupita, zaidi ile gari ilisimama na kioo chake
kilianza kushuka taratibu.
Niliona sura ngeni ya malaika ikiachia tabasamu baada ya kuniona.
Sikuweza kumgundua alikua na asili gani kutokana na uweupe wake na
rangi ya nywele zake. Kabla sijachukua hatua yoyote kutokana na
kupigwa na bumbuwazi, yule msichana alifunga kioo cha gari yake na
kuondoka.
Kusema ukweli sikumuelewa zaidi nilijawa tu mawazo juu ya kitendo
kile. Baada ya kufika kilingeni, nilipokea taarifa kutoka kwa marafiki
zangu kuwa kulikua na mgeni wa kizungu alikuja kuniulizia pale
dakika kadhaa zilizopita.
Kabla hata sijajua ni nani, marafiki zangu walinionyesha msichana
aliyekua amesimama mbali kidogo na pale kuwa ndie aliyekua
ananiita.
Nilimfuata kiuoga na nilipomfikia nilimsalimia, aligeuka na kunitazama.
Uzuri wa macho yake ya blue ndio ulionifanya nishindwe kuongea
chochote.
Ghafla nilimuona yule msichana akinikonyeza na baada ya hapo macho
yake yalibadilika na kuwa kama ya paka. Nilishtuka na nilipotaka
kupiga kelele nilijikuta sauti haitoki. Hata nilijaribu kukimbia
haikuwezekana hata kunyanyua unyayo wangu.
“NAITAKA PETE YANGU”
Aliongea maneno hayo huku akiwa ananitisha kwa kuikunja kunja sura
yake na kuwa sura ambayo sikuweza kuvumilia kuiangalia. Ilinitisha
mno…….
NI PETE GANI ANAYOITAKA KUTOKA KWANGU?
ALINIPA LINI HIYO PETE WAKATI NDIO KWANZA NAMUONA
SIKU HIYO?
 
Wow that waz a very gud start..go on go buddy hahah cant wait 4 the next episode
 
mwanzo niliiong kama zali la mentali ya prof jay, safi!
 
mwanzo niliiona kama zali la mentali ya prof jay, safi!
 
Back
Top Bottom