Lost mandate to govern: Cameron to Labour; CDM to CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lost mandate to govern: Cameron to Labour; CDM to CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ishalua, Mar 1, 2011.

 1. i

  ishalua Member

  #1
  Mar 1, 2011
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Wakati Waziri Mkuu wa Uingereza wakati akifanya kampeni za uchaguzi wa Uingereza uliopita (mwaka jana) na hata siku ya matokeo ya awali ya ubunge yalipotoka, alisema (na alikuwa akisema kwa kurudiarudia) kuwa serikali ya Labour imekosa uhalali wa kuongoza nchi...Hii ni kutokana na mambo mengi ambayo serikali ya Labour haikuyafanyia kazi sawasawa na matarajio ya waingereza. Usemi wake pamoja na uhalali wa kauli hiyo, ulimwezesha Cameron kupata ushindi (aghalabu) kwa kuunda serikali ya mseto na wenzao wa Lib Dems!

  Maneno yake "The Labour government has lost its mandate to govern our country"

  Mimi nadhani, kwa udhaifu wa kiuongozi uliojionesha dhahiri kwenye hotuba ya mheshimiwa Rais, ni wazi kwamba kuna mambo mengi yanayodhihirisha kwamba serikali ya CCM haiko karibu kabisa na wananchi, sina haja ya kuyaorodhesha, yanafahamika na wanajamvi wengi wameshayaainisha! Kuna ulinganifu mkubwa mno wa kauli hii ya Bwana Cameron aliyoitoa kwa serikali ya Labour ilipokuwa bado madarakani kwamba kauli hiyo inaweza kabisa (kwa uhalali pamoja na ushahidi mwingi) kutumiwa na wanaCDM kwamba serikali ya CCM imekosa uhalali wa kugovern nchi yetu!

  Kama ni halali ya CDM kuandamana kikatiba, wakienda nchi nzima kwa lengo la kupinga serikali ya CCM kutaka kuilipa kampuni ya Dowans mabilioni ya shilingi pamoja na kuuambia umma wa watanzania ugumu wa hali ya maisha uliosababishwa na sera na utendaji kazi wa serikali ya CCM, sidhani kama hili linaweza kuchukuliwa kama kuchafua hali ya usalama wa nchi. Wanaandamana kwa amani, wanasema hali halisi iliyopo...majibu ya ufumbuzi wa matatizo ya watanzania hayapo! Kama CCM waliahidi kutatua jambo moja tu kati ya haya mengi, hili la umeme, nearly 5 years ago wakituambia kuna short term plans, midterm na long terms kutatuta kabisa tatizo la umeme nchini, iweje leo tuanze kuambiwa "it takes long time to set up things, put things in place, etc..." hizo short term plans kumbe zilikuwa ni za miaka mingapi???
   
Loading...