Lori laua wanne na kukimbia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lori laua wanne na kukimbia

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Dec 25, 2010.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Dec 25, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  WATU wanne wakiwemo watatu wa familia moja, wamepoteza maisha kwa kugongwa na gari katika ajali ya barabarani iliyotokea juzi katika barabara ya Shinyanga -Nzega katika kijiji cha Usanda, wilaya ya Shinyanga.

  Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Kamanda wa polisi mkoani Shinyanga, Diwani Athumani alisema tukio hilo lilitokea majira ya saa 11 za alfajiri wakati gari aina ya lori lisilofahamika lilipowagonga waendesha baiskeli wawili waliokuwa na abiria watatu.

  Kamanda Athumani alisema watu watatu kati ya wanne waliokufa katika ajali hiyo ni wa familia moja na kwamba walifikwa na mkasa huo wakati wakiwa njiani kuelekea msibani wilayani Nzega mkoani Tabora.

  Aliwataja waliokufa katika ajali hiyo kuwa ni Salum Masesa (36) aliyekuwa akiendesha baiskeli na abiria wake wawili Pili Kimoga (30) na mtoto wake, Winnie Hamisi mwenye umri wa miezi miwili na Tatu Daudi (35) wakazi wa kijiji cha Isela wilaya ya Shinyanga vijijini.

  Alimtaja majeruhi aliyekuwa akiendesha baiskeli ya pili kuwa ni Masunga Nzela (36) mkazi wa kijiji cha Isela amelazwa hospitali ya mkoa. Marehemu watatu, wote wa kike ni wa familia moja.

  Gari kubwa aina ya lori baada ya kutokea kwa ajali hiyo iliyosababisha vifo lilikimbia na kufanikiwa kutoroka bila ya kufahamika na kwamba taarifa za ajali na kutoroka kwa gari hilo lililokuwa lina kwenda kasi imepelekwa mikoa jirani.

  Kamanda huyo wa polisi alisema, uchunguzi wa awali wa polisi umebaini kuwa ajali hiyo ilitokea wakati waendesha baiskeli waliogongwa walikuwa kwenye uelekeo mmoja na gari lililowagonga upande wa kushoto na inadaiwa kuwa lilikuwa kwenye mwendo wa kasi.
   
Loading...