IGUDUNG'WA
JF-Expert Member
- Oct 22, 2011
- 2,071
- 1,316
Gari aina ya scania lililokuwa likitoka mkoani kuingia jijini Dar es salaam nusura lipate ajali maeneo ya Ubungo maji mchana huu baada ya lori hilo kufeli breki zote.
Gari hilo namba T 9850 ASB lilionekana kupoteza mweleko wakati linateremka kutoka kituo cha Kibo kuja ubungo maji.
Kitu ambacho sielewi ni gari hiyo kuhama kutoka upande wa kushoto wa barabara na kuingia upande wa kulia ambapo nusura igonge ukuta wa TANESCO makao makuu,dereva alijitahidi kuimudu gari hiyo iliyokuwa imesheheni mzigo wa mahindi na kusimama salama kando ya kituo cha zamani cha daladala ubungo.
Jambo hili limesababisha foleni kubwa hapa Ubungo mida hii
Hapo kwenye picha ni raia wakimpongeza dereva