Long distance relationship

utakimbia wangapi dunia hii na mapenzi ya siku hizi yanatuchanjia kichizi kutokana haya matumizi ya mtandao.Wenzio(gents) huwa wanajaribu kurepair mwanamke kabla ya kuchukua uamuzi wa kukimbia
 
Haya makitu upuuzi sana. I lost a lot of my time collecting stones while leaving diamonds. Imenisababishia kutokuwa na interest kabisa na wanawake mpaka dada zangu.
Pole sana ila hayo mawazo pia siyo mazuri kwasababu wapo wanawake/wanaume ambao ni wanamapenzi ya dhati kwa wenzao sema tu hujampata ndo maana nakwambia hayo mawazo sio mazuri coz hata akitokea mzuri hutamwamini kwahyo usikate tamaa ndugu na usihakishe kuingia kwenye uhusiano kwanza kabla ya kuchunguza,tunachokosea ni pale umetoka kuachana na huyu maumivu hayajapoa unaanzisha mapya ukitarajia yatapoza maumivu kumbe ndo balaa zaidi matokeo yake unajikuta umekutana na watu wengi kwa muda mfupi lkn wote hawana afadhali.
 
kazi kweri kweri
 
Long distance inatoa mazingira makubwa ya kutokuwa na uaminifu kwa wahusika. Unakuta binti anafuatiliwa na mtu, kutokana na upweke mkuu anaouhisi kila mara anajiingiza katika urafiki ili kupato ridhio la moyo ambalo aghalabu huishia katika uhusiano mpya na kwakuwa mhusika wake yuko mbali huwa huru na kujinafasi haswa.

Mara nyingi mtu huyu huendelea kuweka mahasuiano kwa simu, skype n.k na mwezie kama kawaida ilihali akiendelea kujipooza nafsi na mtu alienae karibu.

Kutokana na hali hii ambayo husababishwa na umbali wa kimazingira na mhusika wake ni vema ikiwa hujaoana na mtu na ikiwa si lazima basi usiingie kwenye mahusiano na mtu aliembali.....wahenga walinena..fimbo ya mbali haiui nyoka...
 
mimi nimeona hapo kwenye RED tu
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…