Loliondo kunani?

Loliondo kunani?

SueIsmael

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2013
Posts
932
Reaction score
1,283
Wandugu,

Kwenye social media fulani nimeona ripoti kuwa kuna oparesheni inaendelea Loliondo ya kuondoa wakazi kwenye "maeneo ya hifadhi". Ripoti hizo zinasema kuna nyumba zilizochomwa moto, watu wameumizwa na wengine wamepoteza vitu.

Kuna yeyote aliyeko kwenye maeneo hayo akathibitisha taarifa hizi? Au mwenye taarifa zaidi?

Natanguliza shukurani.

Updates:
Nyamera:
Bomas are being burned illegally on village land. I wrote a blog post about what happened yesterday.
Illegal Arson Attack in Loliondo – Rangers Say that They Have Started an Operation to Evict the Maasai from the 1,500 km2 Osero
The arson continues today.

Inasemekana kuwa kuna oparesheni imeanzishwa jana Loliondo kuondoa watu na mifugo kwenye eneo lililo na kubwa wa 1,500KM2. Huko Ololosek boma 5-9 zimechomwa moto na watu kuondolewa kwa nguvu na askari wa wanyama pori. Taarifa kutoka chanzo hiki kinasema oparesheni hii imetokana na amri ya Waziri wa Malia Asili na Utalii.
20821387_10154616399265653_932990893_o%2B%25281%2529.jpg


20821394_10154616398010653_494177169_o%2B%25281%2529.jpg


20861472_10154616397055653_1451996190_o%2B%25281%2529.jpg


Kijana Pomoson Ololoso amepigwa risasi na Askari wa wanyama pori tarehe 8/8, Kijijini Oloosek. Inasemekana askari huyo alikuwa anaomba rushwa kwa wachungaji waliokuwa wanachunga eneo la hifadhi ya Serengeti, walipokataa kumuongezea hela alifyatua risasi hovyo na tatu zikampata Pomoson.
Pormoson%2BOloloso.jpg
 
mbona walijazana pale na ofisi wakafunga kwenda kuweka foleni ya kikombe hawakuliona hili wakiwa kwenye mstari?
 
mbona walijazana pale na ofisi wakafunga kwenda kuweka foleni ya kikombe hawakuliona hili wakiwa kwenye mstari?
Walikua wanaumwa upofu baada ya kunywa dawa wamepona ndio maana wanawaondoa.

RubiiKimimi[emoji85]
 
Hii wilaya Ngorongoro ni bora ingetangazwa marufuku kuishi binadamu tangu enzi za mwalimu watu wangeshahama Siku nyingi na kuanza maisha kwingwineko. Sahivi watu wengi nchini sijui hawa wamasai watahamia wapi. Kibaya hawatakiwi kujenga nyumba za kudumu wala kufanya kilimo chenye tija hata ktk maeneo hayo machache waliporuhusiwa kuishi kisheria.
 
Back
Top Bottom