Jamaa>naomba lift
Lodilofa>mimi sina lift ningekuwa nayo ningekupa
Jamaa>sina maana hiyo yaani naomba nipande gari yako..
Lodilofa>pumbaf...umeona gari yangu ni mahindi au maharage mpaka upande shambani..!?HUKU AKIWASHA GARI NA KUONDOKA SPEED AKIMUACHIA JAMAA VUMBI.
nilikuwa namkubali sana Ndondocha wa tabasamu kama kuna anayekumbuka kituko chake akitoe jamani.
Kituko cha ndondocha kwenye mazishi.
Msemaji: Poleni sana ndugu wafiwa, sasa kama ilivyo kwa utamaduni wetu mtu akifa lazima apatikane mtu wa kumsindikiza (Akimaanisha azikwe pamoja na marehemu)
Waombolezaji: Ndio..
Ndondocha: Kweli kabisaaa, lazima tudumishe mila, sasa tutampataje huyo mtu?
Msemaji: Wanandugu watapiga kura.
Waombolezaji: Uamuzi wa busara. (Wakapiga kura)
Msemaji: Nashukuru sana, tumeshampata msindikizaji, mtu aliyepigiwa kura nyingi ni Ndugu Ndondocha, hivyo tunaomba usogee karibu na kaburi hapa ili tumalize haraka.
Ndondocha: (Huku akiwa na hasira..) Jamani basi naombeni mniruhusu nikaage familia yangu, nipeni dakika 15 tu tena na ulinzi kama hamniamini.
Waombolezaji: Sawaaa
Ndondocha kaenda nyumbani akakusanya jeshi lake (Mwanae
KIOKOTE na mbwa kama laki mbili hivi pamoja na Anko wake
KAISI jamaa anapiga vichwa balaa)
Kilichotokea nafikiri msomaji unaweza malizia..
I miss NDONDOCHA