Lo!,NAPE NNAUYE APOTEZA vs UFISADI = O-2 (ARUMERU MASHARIKI) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lo!,NAPE NNAUYE APOTEZA vs UFISADI = O-2 (ARUMERU MASHARIKI)

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by commonmwananchi, Mar 3, 2012.

 1. commonmwananchi

  commonmwananchi JF-Expert Member

  #1
  Mar 3, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 2,152
  Likes Received: 477
  Trophy Points: 180
  Haiwi haiwi mwisho imekuwa.
  Ni nape nnauye yule katibu mwenezi wa ccm taifa.ambae amekuwa akipinga ufisadi ndani ya chama chake kila siku majukwaani, hatimae amejitokeza rasmi huko arumeru na kumtangaza rasmi Bw sioi sumari kama mgombea wa chama chake kwa nafasi ya ubunge jimboni humo.

  Hatua hii ni sawa na kukubali Rasmi kupoteza mechi baina yake dhidi ya mafisadi,kwani mbali ya sioi kuwa ni mkwe wa hasimu mkuu wa Nape Bw Lowassa lakini pia mchakato mzima wa uteuzi wake ulighubikwa na ufisadi mkubwa wa rushwa na kupelekea malalamiko makubwa ndani ya chama chao.
  Lakini pia imeenda mbali zaidi na kufikia hatua hata ya baadhi ya wana ccm kutiwa mbaroni kwa tuhuma za rushwa wakihusishwa na Sioi huyuhuyu.

  Kitendo cha Nape kutokea na kuwa bega kwa bega na maamuzi hayo ni sawa na kusalimu amri kwa ufisadi sawa na kupoteza mechi kwa kulambwa magoli mawili kwa bila.
   
 2. a

  alpha5 JF-Expert Member

  #2
  Mar 3, 2012
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 209
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  acha unaffik wewe
   
 3. commonmwananchi

  commonmwananchi JF-Expert Member

  #3
  Mar 3, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 2,152
  Likes Received: 477
  Trophy Points: 180
  Mnafiki ni wewe unayetoa jibu la kihuni kwenye hoja inayotaka tafakuri ya kina,tumia bongo kujibu watu makini na kama ulifisadi hadi matokeo ya elimu basi kaa kimya au nenda kale kiroba!
   
 4. LE GAGNANT

  LE GAGNANT JF-Expert Member

  #4
  Mar 3, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 1,247
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Chama tawala kuondoa rushwa na ufisadi ni sawa na kuondoa tatizo la foleni dar. Ufisadi ndio umewaingiza madrakani watauondoaje?
   
 5. commonmwananchi

  commonmwananchi JF-Expert Member

  #5
  Mar 3, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 2,152
  Likes Received: 477
  Trophy Points: 180
  Sasa ndugu yetu Nape,najiuliza binafsi bila kupata jibu la mara moja.hivi anajisikiaje kwa sasa.au ndio kama unavyosema kwamba kiapo chao ni kimoja?
   
 6. PENDING'ULA

  PENDING'ULA JF-Expert Member

  #6
  Mar 3, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 269
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wachunguzi wa mambo tulijua tangu mwanzo kuwa "mechi" hii ataipoteza! Sababu kubwa ni kwamba Nape ni kocha, Kipa, Defender, Kiungo mkabaji na wakati huohuo ni Mshambuliaji! Sijawahi kushuhudia ushindi wa maana katika mechi dizaini hii zaidi ya kuwa kituko cha aina yake! Nape hana uungwaji mkono wa dhati katika vita yake! Atapoteza mapambano mengi!
   
 7. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #7
  Mar 3, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Mnachanganya mambo....!

  kweli vuvuzela linakera sana masikioni hasa likiwa linapuliza bila kukoma nimeamini sasa.
   
 8. commonmwananchi

  commonmwananchi JF-Expert Member

  #8
  Mar 3, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 2,152
  Likes Received: 477
  Trophy Points: 180
  Mimi namshauri angefanya jambo moja tu.nalo ni kumuomba Lowassa msamaha na avunje kambi ya Anti-magamba na kujiunga na Magamba original team,
   
 9. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #9
  Mar 3, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Hata kama lowassa hapendi Nape atabaki kuwa katibu mwenezi wa ccm mwenye wajibu wa kueneza sera za chama chake na kuyanadi maamuzi yote ya chama,hawezi kwenda kinyume na hilo kama sioi ndio mgombea wa ccm kwa sasa basi kambi zote zinavunjika rasmi na kuwa kambi moja ya ccm,huo ndio utamaduni wa chama chetu,naona wengi hamjui,tutawaelewesha mpaka muelewe na kuacha upotoshaji.Kujivua gamba palepale mpaka chama kitakapotangaza vinginevyo,lakini kwa sasa kisu cha kamati kuu ndio kinanolewa kwa ajili ya kulichana chana gamba lililobaki.
   
 10. commonmwananchi

  commonmwananchi JF-Expert Member

  #10
  Mar 3, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 2,152
  Likes Received: 477
  Trophy Points: 180
  Kama ni kisu basi hakifai kwani kinamjeruhi hadi mkataji mwenyewe.nina maana Nape mwenyewe.na kwa tafsiri yangu kutokana na ulichoandika ni kama umesema Nape hata kama hapendi ufisadi,lakini pale ambapo chama kimeamua kuukumbatia,basi ni lazima asimame na kuutangaza msimamo huo na pia ikibidi kuutetea kwa nguvu zote atake asitake,

  Hivi hiyo cc unayoisema ni tofauti na hii iliyompitisha Sioi bila kuyaona madoa ya rushwa yaliyokiacha chama majeruhi ndani ya wodi ya washili?
   
 11. PENDING'ULA

  PENDING'ULA JF-Expert Member

  #11
  Mar 3, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 269
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naam, Hilo kwa wanasiasa linawezekana! Ni mara nyingi tumeshuhudia wakiyaramba matapishi yao mchana wa jua kali!
   
 12. commonmwananchi

  commonmwananchi JF-Expert Member

  #12
  Mar 4, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 2,152
  Likes Received: 477
  Trophy Points: 180
  Tatizo ni kwamba haya matapishi anyolamba sasa Nape,yana madhara kwa jamii ya kitanzania kwa kiasi kikubwa sana.
  Ni lazima ajuwe kwamba tayari alikuwa ana wafuasi ndani ya chama chake waliokuwa wanamuunga mkono na kampeni yake hii dhidi ya magamba. Hivyo kwa muelekeo anaoonyesha kuelekea ni dhahiri anawaacha njia panda wafuasi wa Anti-magamba ndani ya ccm yake.
   
 13. k

  kiponzelo Member

  #13
  Mar 4, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hii nchi inaendeshwa kichifu au kitemi kama mkwawa au?sipati picha kwa nini mkwe apewe ubunge tena?h
   
 14. commonmwananchi

  commonmwananchi JF-Expert Member

  #14
  Mar 4, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 2,152
  Likes Received: 477
  Trophy Points: 180
  Unajua hali jimboni pale kwa wana ccm ni kwamba ilikuwa ni kama kufanya mirathi kwenye siasa.kwani hata angekuwa sio Sioi sumari mtoto wa Marehemu Jeremia sumari.basi angekuwa mwingine ni wa Mirisho sarakikya bila shaka!
   
Loading...