Liwalo naliwe

Liwalo naliwe

kabiriga

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2012
Posts
1,163
Reaction score
1,213
Siku Ishirini ya kuokoka baada ya kuubiliwa neno la Mungu,tukiwa tumejipumuzisha kitandani mimi na mke wangu mara nikaanza kumuomba msamaha kwakuwa nilitenda mabaya enzi za giza(kabla sijaokoka) "nilitembea nje ya ndoa mke wangu nisamehe nakuhaidi sitarudia tena" "Nimekusamehe mme wangu yametipa hayo" alisema.
Baadae nae akaanza kwa tahadhari akinitaka niseme kweli kama nita msamehe kwa aliyonitendea nikamwambia ondoa shaka mke wangu nitakusamehe tu.Akasema "unajua mme wangu nimepigana sana kukupata na isingekuwa mama mmoja leo tusingekuwa wote,nilikupa dawa unipende sana mme wangu baada ya kuona unataka kuniponyoka,dawa ya mwisho niliyo kulisha niliichanganya na kipande cha nyama na nilikiweka sehemu zangu za siri siku 2 kisha nika kipika na kukiunga na nyama nyingine ndo nkakupa,baada ya kula tu ndo ukaawa wangu nikakutuliza.umenisamehe mme wangu kwa kukulisha dawa za upendo?"
Baada ya hapo nilitafakali sana nikageuka upande wapili wa kitanda nikajifanya kulala usingizi lakini nilkuwa natafakari kamakweli nimsamehe au la!.
sija mwambia kama nimemsamehe au hapana.nimejipa siku tatu za kutoa (kumwambia uamuzi) na maamuzi yangu nikuachana nae kwani kwangu mimi nimeona alifanya makosa yasiosameheka,kwani kama ingelikuwa sumu ningalikwisha kufa.Naombeni ushahuri wenu kama uhamuzi wangu ni haki.
 
Sasa ikiwa yeye kakuzamewe kwa kosa ulilofanya yeye alitaka kukupa ili uekupe na uzinzi na maradhi...kumbuka mwenyezi mungu husamehe ukimuomba kwa nia nzuri kwanini wewe huwezi kumsamehe binadamu mwenzio? ebu fikiri kama angekwambia yeye ndio amefanya kosa kama lako ungemsamehe kweli?..
 
poleni nyote, wewe na mkeo kama kweli.,; kama wewe umesamehewa, kwanini na wewe usisamehe, au unaona wewe dhambi yake ni ndogo kuliko yake? eti ingekua sumu ungeshakufa kwani wewe ingekua UKIMWI huko nje si ungeshamuua? kama upo hai sasa unataka nini zaid? hebu try to think critically bwana, hakuna mwema hapo hata mmoja coz wote mna makosa, so samehaneni hakuna dhambi ndogo wala kubwa...
 
Kwani kutoka nje ya ndoa ni dhambi ndogo sana kwako? Kulishwa dawa utulie badala ya kufurahia unaona balaa?

Mbona yeye alikusamehe? Unaonekana hata huo wokovu wako una mashaka!

Watu tunatafuta tupewe dawa tutulie we unasema nini sijui!
 
Anatakiwa akufanyie ivo tena 7x70 we ni kumsamehe tu, ya 71 unampiga chini.
 
Mkuki kwa Nguruwe kwa binadamu..... Pole kuokoka kumekuletea balaa badala ya baraka.
 
........Endelea kushukuru Mungu kwamba hatakusimulia mambo mengine machafu ya yeye pia kutembea nje ya ndoa... mambo ya kusameheana msameheane tu kwa kuwa sasa mmekuwa viumbe vipya ya kale yamepita.... tazama yamekuwa mapya...
 
Kinachokufanya hasa usimsamehe ni kipi?
kukufanya umwache mwingine uwe nae au kukulisha nyama aloiweka down kwake?
kama ni kumwacha mwingine kwani humpendi mkeo au uliumia kuachishwa na huyo mwingine?
kama ni kulishwa nyama aloweka ustawi wa jamii ndo ishu kwani huendagi uvinza?

Msamehe mkeo kuokoka si kuhudhuria.....ukisamehe ndo haswa ulokole unapoonekana!!!!!!!!
 
... Mkuu kama wewe uwezi samehe'
Natamani kama ingekuwa inawezekana' aje anifanyie mimi hiyo dawa.
 
Siku Ishirini ya kuokoka baada ya kuubiliwa neno la Mungu,tukiwa tumejipumuzisha kitandani mimi na mke wangu mara nikaanza kumuomba msamaha kwakuwa nilitenda mabaya enzi za giza(kabla sijaokoka) "nilitembea nje ya ndoa mke wangu nisamehe nakuhaidi sitarudia tena" "Nimekusamehe mme wangu yametipa hayo" alisema.
Baadae nae akaanza kwa tahadhari akinitaka niseme kweli kama nita msamehe kwa aliyonitendea nikamwambia ondoa shaka mke wangu nitakusamehe tu.Akasema "unajua mme wangu nimepigana sana kukupata na isingekuwa mama mmoja leo tusingekuwa wote,nilikupa dawa unipende sana mme wangu baada ya kuona unataka kuniponyoka,dawa ya mwisho niliyo kulisha niliichanganya na kipande cha nyama na nilikiweka sehemu zangu za siri siku 2 kisha nika kipika na kukiunga na nyama nyingine ndo nkakupa,baada ya kula tu ndo ukaawa wangu nikakutuliza.umenisamehe mme wangu kwa kukulisha dawa za upendo?"
Baada ya hapo nilitafakali sana nikageuka upande wapili wa kitanda nikajifanya kulala usingizi lakini nilkuwa natafakari kamakweli nimsamehe au la!.
sija mwambia kama nimemsamehe au hapana.nimejipa siku tatu za kutoa (kumwambia uamuzi) na maamuzi yangu nikuachana nae kwani kwangu mimi nimeona alifanya makosa yasiosameheka,kwani kama ingelikuwa sumu ningalikwisha kufa.Naombeni ushahuri wenu kama uhamuzi wangu ni haki.

japokuwa hii stori kama imetungwa vile ila mwanaume ameshindwa kukabili kitu kidogo tu.Kweli wanaume ushuzi wengi
 
ubinafsi unakusumbua....haina haja ya kuokoka kama kusamehe huwezi ....wokovu gani wa kutosamehe?
 
"USHUZI" maanake nini? upaswi kutukana hapa kama uoni hoja bora iache ipite,sijaipenda.

Hii sio story ya kutunga! kama uoni ukweli ndani yake ulazimishwi kuamini hivyo.waachie watakaoona inafaa kushahuri wafanye hivyo.
 
Utunzi, na kujidanganya kisaikologia.
Hamna dawa ya mapenzi.
 
kama umeokoka utasamehe lkn km ulijifanya umeokoka kumfurahisha mkeo hutasamehe. Kuwa mwepesi wa kusamehe uishi kwa amani na watu wote baba.
Kwa nn wanaume walio wengi ni wagumu kusamehe?
 
Back
Top Bottom