Siku Ishirini ya kuokoka baada ya kuubiliwa neno la Mungu,tukiwa tumejipumuzisha kitandani mimi na mke wangu mara nikaanza kumuomba msamaha kwakuwa nilitenda mabaya enzi za giza(kabla sijaokoka) "nilitembea nje ya ndoa mke wangu nisamehe nakuhaidi sitarudia tena" "Nimekusamehe mme wangu yametipa hayo" alisema.
Baadae nae akaanza kwa tahadhari akinitaka niseme kweli kama nita msamehe kwa aliyonitendea nikamwambia ondoa shaka mke wangu nitakusamehe tu.Akasema "unajua mme wangu nimepigana sana kukupata na isingekuwa mama mmoja leo tusingekuwa wote,nilikupa dawa unipende sana mme wangu baada ya kuona unataka kuniponyoka,dawa ya mwisho niliyo kulisha niliichanganya na kipande cha nyama na nilikiweka sehemu zangu za siri siku 2 kisha nika kipika na kukiunga na nyama nyingine ndo nkakupa,baada ya kula tu ndo ukaawa wangu nikakutuliza.umenisamehe mme wangu kwa kukulisha dawa za upendo?"
Baada ya hapo nilitafakali sana nikageuka upande wapili wa kitanda nikajifanya kulala usingizi lakini nilkuwa natafakari kamakweli nimsamehe au la!.
sija mwambia kama nimemsamehe au hapana.nimejipa siku tatu za kutoa (kumwambia uamuzi) na maamuzi yangu nikuachana nae kwani kwangu mimi nimeona alifanya makosa yasiosameheka,kwani kama ingelikuwa sumu ningalikwisha kufa.Naombeni ushahuri wenu kama uhamuzi wangu ni haki.
Yaani ndugu yangu nadhani hujaelewa maana ya Wokovu(kuokoka).
Kuokoka ni kujisalimisha kwa Yesu, Kumkiri Yeye kwa kinywa chako kuwa ni Bwana. Kuyaacha yale yote zamani ulifanya(Kuwa kiumbe kipya ya kale yote yamepita) Kubadilika kutoka katika hatua moja kwenda katika hatua nyingine nzuri zaidi. Kiafya, kimazingira, kiuchumi na kielimu. Sasa wewe naona unataka urudi Misri wakati uko safarini kuelekea kanani.
Sikuzote ndani ya wokovu jifunze kusamehe na kusahau,Mkeo huyo ametubu kwa kile alichokutendea kama wewe ulivyotubu uliyoyafanya kinyume na mpango wa Mungu.Kwani usipo samehe Umeuacha wokovu maana maandiko yanatuamuru "NINYI KILA MSIMAMAPO NA KUSALI, SAMEHENI, mkiwa na neno juu ya mtu; ili na Baba yenu aliye mbinguni awasamehe na ninyi makosa yenu. Lakini kama ninyi hamsamehi, wala Baba yenu aliye mbinguni hatawasamehe ninyi makosa yenu" (Marko 11, 25, 26 ).
Maana yake, kutokusamehe kunahesabiwa kuwa ni kosa mbele za Mungu, na ni dhambi inayotutenga na uso wa Mungu, ili tusijibiwe maombi yetu toka kwa Mungu. Kutokusamehe ni uasi, Dhambi ni uasi (1 Yohana 3:4) Dhambi ni kuasi maagizo ya Mungu.
Lakini kama ulimpokea Kristo kuwa Bwana na Mwokozi wako unatabia ya kusamehe ndani yako.Maana maandiko yanasema "Bali wote waliompokea (Kristo) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake; waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu." (Yohana 1:12,13)
Sasa nakuomba ndugu yangu kama uliokoka kwa kumaanisha unatabia hii ndani yako:
Kuyafuta makosa na kutoyakumbuka tena ni tabia ya Mungu ambayo imo ndani yako sasa.Ulipompokea Kristo moyoni mwako na kumkiri kuwa ni Bwana wa maisha yako, pia ulipokea ndani ya moyo wako tabia hii ya Mungu ya kufuta makosa na kutoyakumbuka.Hii ndiyo tabia inayotakiwa ionekane katika maisha yako unapokosewa na mtu.