Livingstone Lusinde amewataka CHADEMA Wamuadhibu Joshua Nassari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Livingstone Lusinde amewataka CHADEMA Wamuadhibu Joshua Nassari

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Msororo69, Apr 21, 2017.

 1. M

  Msororo69 JF-Expert Member

  #1
  Apr 21, 2017
  Joined: Feb 27, 2016
  Messages: 2,046
  Likes Received: 588
  Trophy Points: 280
  MBUNGE wa Jimbo la Mtera, Livingstone Lusinde amewataka wabunge kujiheshimu na kuheshimu wenzao, kama kweli wanataka kuheshimika huku akilaani kitendo cha mbunge wa chama hicho, Dk Godwin Mollel kupuuza hatua zinazochukuliwa dhidi ya watu wanaochukuliwa hatua kwa kumtukana Rais John Magufuli kupitia mitandao.

  Alisema inashangaza kuona mbunge huyo akitaka Serikali iache kushughulika na mambo yanayoitwa madogo, yakiwemo kama ya kumtukana Rais. Awali, akichangia hotuba za bajeti za wizara mbili zilizopo Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) na ile ya Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dk Mollel ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Siha, aliwataka Watanzania kubadilisha fikra, huku upande serikalii akiisihi iache kushughulika na mambo madogo, akitolea mfano wanaoshughulikiwa kwa kumtusi Rais.

  Lakini Lusinde, alikemea hilo, akisema; “Haiwezekani Rais atukanwe, halafu Mbowe aheshimiwe…Rais anafanya kazi kubwa sana ya kubadilisha mfumo wa uongozi wa nchi hii… Dokta (Mollel) hapa amezungumzia suala la kubadilisha fikra, na huu ni mchango wake wa pili wa aina hii, anasisitiza hilo, kwanza tuwe na mtazamo mpya ili tusonge mbele….

  “Anasema tuache kushughulika na watu wadogo wanaomtukana Rais na badala yake tuhangaike na mambo makubwa…aah, ila dokta huyo huyo anayetutaka tubadilishe fikra anasema kiongozi wa kambi ya upinzani aheshimiwe, ni mtu mkubwa. Yaani Rais atukanwe, Mbowe aheshimiwe? Hatuwezi kwenda hivyo, kama tunataka heshima. Tukiheshimiana hapo tutaona kuendesha nchi ni kazi rahisi.”

  Alisisitiza suala la kutukanwa si dogo, hivyo viongozi wa vyama vingine vya upinzan wasilee matukio ya aina hiyo, bali waungane kumuunga mkono Rais na serikali yake kwa ajili ya ustawi wa nchi. “Mimi naamini Rais anafanya kazi nzuri kabisa ya kuubadilisha mfumo wa nchi hii. Kazi yetu kubwa isiwe kumrudisha nyuma, tumpe moyo, tumtie nguvu Rais wetu, tuwatie nguvu mawaziri wasukume mbele gurudumu la maendeleo.

  “Hivyo naomba tunapozungumzia heshima tuzungumzie pande zote mbili,” alisema na kuimwagia sifa serikali kuwa inafanya kazi kubwa kiutendaji, akitolea mfano Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Kazi inavyozikabili kero za ardhi. Akikazia suala la heshima, alisema anasikia kuna mbunge wa upinzani (Joshua Nassari wa Chadema) juzi aliingia maeneo ya Bunge akiwa na pombe aina ya Konyagi, hivyo kutaka awajibishwe na chama chake.

  “Sisi juzi juzi tu hapa Serikali imemwajibisha Kitwanga (Charles, aliyevuliwa Uwaziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi) kwa kudhaniwa tu amelewa, lakini leo mbunge anaingia na konyagi maeneo ya bunge na anakamatwa. “Sasa leo hii tunataka kuona meno yenu yako wapi, kwa kumwajibisha huyo mbunge, kama mtaweza maana kazi yenu ni kusema tu siyo kutenda. Tunataka kuona mtakuwa wakali kwa kiwango gani kwa mbunge anayekuja bungeni amelewa halafu ana chupa ya konyagi. Sisi tumeshaonesha njia, waziri amekuja amelewa amewajibishwa, sasa ninyi mtachukua hatua gani? alihoji.

  Source Habarileo online
   
 2. Mystery

  Mystery JF Gold Member

  #2
  Apr 21, 2017
  Joined: Mar 8, 2012
  Messages: 7,994
  Likes Received: 6,776
  Trophy Points: 280
  Namshauri huyo Kibajaj asome Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977, Ibara ya 13(1) ambayo inasema hivi ' Watu wote ni sawa mbele ya sheria na wanayo haki bila ya ubaguzi wowote kulindwa na kupata haki sawa mbele ya sheria' mwisho wa kunukuu.

  Sasa tujiulize lugha anayotumia Rais wetu mara kwa Mara kuwakejeli na kuwakashifu viongozi wa vyama vya upinzani, na dhahama wanazopata viongozi wa vyama vya upinzani kutoka vyombo vya dola, ni kwa nini huyo Kibajaj asianze kwanza kumtuhumu Mwenyekiti wake wa Chama Cha Majipu, kuwa ndiye yupo mstari wa mbele kuivunja waziwazi hiyo Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?
   
 3. mrangi

  mrangi JF-Expert Member

  #3
  Apr 21, 2017
  Joined: Feb 19, 2014
  Messages: 22,020
  Likes Received: 9,311
  Trophy Points: 280
  DarasA la Saba ni shidaa

  Ova
   
 4. mrangi

  mrangi JF-Expert Member

  #4
  Apr 21, 2017
  Joined: Feb 19, 2014
  Messages: 22,020
  Likes Received: 9,311
  Trophy Points: 280
  MUDA wa kusoma autoe wapi Huyu lisinde

  Ova
   
 5. Mystery

  Mystery JF Gold Member

  #5
  Apr 21, 2017
  Joined: Mar 8, 2012
  Messages: 7,994
  Likes Received: 6,776
  Trophy Points: 280
  It is true, huyo jamaa ni semi illiterate!
   
 6. mrangi

  mrangi JF-Expert Member

  #6
  Apr 21, 2017
  Joined: Feb 19, 2014
  Messages: 22,020
  Likes Received: 9,311
  Trophy Points: 280
  Hakuna kitu kabisaaa hyo

  Ova
   
 7. Mystery

  Mystery JF Gold Member

  #7
  Apr 21, 2017
  Joined: Mar 8, 2012
  Messages: 7,994
  Likes Received: 6,776
  Trophy Points: 280
  Shida yote hiyo kwa Bunge letu kuwa na wabunge wa design ya akina Lusinde, ni hao hao wabunge wa CCM ambao kwenye Katiba yao pendekezwa ya Lumumba, wameweka kiwango cha elimu ya Mbunge ni kujua tu kusoma na kuandika lugha ya kiswahili!

  Ama kweli Sisiem ni janga la Taifa......
   
 8. E

  Euphransia JF-Expert Member

  #8
  Apr 21, 2017
  Joined: Jan 26, 2017
  Messages: 941
  Likes Received: 767
  Trophy Points: 180
  Kwani CCM kama Chama kilimwadhibu Charles Kitwanga?
   
 9. Tukundane

  Tukundane JF-Expert Member

  #9
  Apr 21, 2017
  Joined: Apr 17, 2012
  Messages: 8,322
  Likes Received: 2,686
  Trophy Points: 280
  Kama unania ya kumwambia mwenzako ukweli kwa lengo la kutaka kumurekebisha,kitu cha kwanza wewe mwenyewe unatakiwa ufanane na ukweli unaotaka kumwambia mwenzako.

  Kwanza yeye mwenyewe ndiye kamdhalilisha mh Rais kwa kumuona kuwa siyo mtu makini katika utendaji wake kwa kumufukuza waziri kazi kwa kuzaniwa tu kalewa.

  Wakati picha zipo zinazomuonyesha waziri akiwa amelewa chakari kitu ambacho kinathibitisha kuwa maamuzi ya mh rais ya kumufukuza waziri kazi hayakuwa ya kubahatisha ili kuwa ni halali mh rais kufanya kama alivofanya.

  Pia kitendo cha kuambiwa kuwa Nasary alikamatwa na chupa ya konyagi nao ni ubabaishaji ulelule,chupa ya konyagi ni kitu ambacho kinaonekana kwanini Nasary asipigwe picha wakati anakamatwa akiwa na chupa yake watu tukamuona kama tulivyo muona mh Kitwanga akiwa ameusokota ugimbi?.
   
 10. kmbwembwe

  kmbwembwe JF-Expert Member

  #10
  Apr 21, 2017
  Joined: Aug 16, 2012
  Messages: 6,425
  Likes Received: 1,394
  Trophy Points: 280
  wacha uongo. toa mifano rais ametukana au amekejeli upinzani zaidi ya kufanya utani tu unaokubalika kwenye siasa zetu. huwezi kulinganisha na matusi kwenye mitandao ambayo ina mikono ya wapinzani. mtu kama lissu na lema wamekua mfano wa lugha ya kejeli na matusi kwa rais wa jamhuri
   
 11. mrangi

  mrangi JF-Expert Member

  #11
  Apr 21, 2017
  Joined: Feb 19, 2014
  Messages: 22,020
  Likes Received: 9,311
  Trophy Points: 280
  Jamaa anastahili apigwe manati TU maana ni shidaaa

  Ova
   
 12. Bome-e

  Bome-e JF-Expert Member

  #12
  Apr 21, 2017
  Joined: Jan 3, 2014
  Messages: 8,605
  Likes Received: 5,439
  Trophy Points: 280
  Hivi kitwanga aliwajibishwa na chama?Sitetei suala la Nassari ila naona Lusinde anasema uongo kujenga hoja yake!
   
 13. mbikagani

  mbikagani JF-Expert Member

  #13
  Apr 21, 2017
  Joined: Dec 5, 2014
  Messages: 2,248
  Likes Received: 853
  Trophy Points: 280
  KIMSINGI MAMBO YANAYOFANYWA NA CCM NI YA AJABU.
  LAKINI KUINGIA BUNGENI UMELEWA, TENA NA CHUPA MKONONI, NI AJABU ZAIDI.
   
 14. Mystery

  Mystery JF Gold Member

  #14
  Apr 21, 2017
  Joined: Mar 8, 2012
  Messages: 7,994
  Likes Received: 6,776
  Trophy Points: 280
  Kule kuwaambia watu wa Kagera kuwa Ukimwi wao.....

  Katerero wao........

  Hata mto ngono upo kwao.......

  Hivi huo tunaweza kuuita utani au ni kashfa na kuwakejeli watu wa Kagera!?
   
 15. BAVARIAN

  BAVARIAN JF-Expert Member

  #15
  Apr 21, 2017
  Joined: Mar 15, 2017
  Messages: 223
  Likes Received: 161
  Trophy Points: 60
  Sidhan kama mtu mwenye akili timamu unaweza kuendelra kuzungumzia habar za akina lusinde,wasitupotezee mda we need bashiiite certificate
   
 16. k

  kabombe JF-Expert Member

  #16
  Apr 21, 2017
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 15,649
  Likes Received: 8,609
  Trophy Points: 280
  Chadema hakuna mwenye uthubutu wa kumuonya Nasari.Wote wanywa viroba
  Tunaposema chadema ni chama cha wanywa viroba tunamaanisha mambo kama haya ya Mbunge mzima kuingia bungeni na konyagi
   
 17. misasa

  misasa JF-Expert Member

  #17
  Apr 21, 2017
  Joined: Feb 5, 2014
  Messages: 5,506
  Likes Received: 2,540
  Trophy Points: 280
  Kama hayo maelezo yametoka kwenye kinywa cha mhe.lusinde basi pongezi zake ametoa point tupu kama mhe. Joshua alionekana na konyagi ajibishwe na chama chake.
   
 18. Mystery

  Mystery JF Gold Member

  #18
  Apr 21, 2017
  Joined: Mar 8, 2012
  Messages: 7,994
  Likes Received: 6,776
  Trophy Points: 280
  Tupe ushahidi kuwa huyo Nassari aliingia na chupa ya konyagi yenye kilevi kule Bungeni.

  Kwa kuwa nyinyi makada wa rangi ya kijani, kwa 'kuwapakazia' wapinzani hamjambo........
   
 19. b

  bibinnaa JF-Expert Member

  #19
  Apr 21, 2017
  Joined: Jan 17, 2017
  Messages: 1,006
  Likes Received: 813
  Trophy Points: 280
  I stand to be corrected....sijawahi kumsikia Mh. Huyu akichangia mambo ya maendeleo...siku zote ni mipasho na maandiko ya kwenye kanga.Nina uhakika watu wa sampuli hii wanamkwamisha Mh Rais kuleta mabadiliko chap chap
   
 20. Tukundane

  Tukundane JF-Expert Member

  #20
  Apr 21, 2017
  Joined: Apr 17, 2012
  Messages: 8,322
  Likes Received: 2,686
  Trophy Points: 280
  Hakuna mtu yeyote ambaye anaweza akafurahi mh Rais kutukanwa kwa kuwa ni Rais wa wote na anatakiwa aheshimiwe na watu wote.

  Tatizo ni pale ambapo hata lisilo kuwa tusi linalazimishwa kubadilishwa kwa nguvu na kuwa tusi kwa kuwa mh Rais kasemwa,kiasi ambacho Kuna mtu alishawahi kupelekwa Mahakamani kwa kumuandika boss Fulani mpumbavu lakini waliishia kushindwa Mahakamani baada ya kuthibitika kuwa upumbavu siyo tusi.
   
Loading...