Livingstone Lusinde amewataka CHADEMA Wamuadhibu Joshua Nassari

wacha uongo. toa mifano rais ametukana au amekejeli upinzani zaidi ya kufanya utani tu unaokubalika kwenye siasa zetu. huwezi kulinganisha na matusi kwenye mitandao ambayo ina mikono ya wapinzani. mtu kama lissu na lema wamekua mfano wa lugha ya kejeli na matusi kwa rais wa jamhuri
hivi hii nchi ina raisi kweli??
 
Namshauri huyo Kibajaj asome Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977, Ibara ya 13(1) ambayo inasema hivi ' Watu wote ni sawa mbele ya sheria na wanayo haki bila ya ubaguzi wowote kulindwa na kupata haki sawa mbele ya sheria' mwisho wa kunukuu.
Sasa tujiulize lugha anayotumia Rais wetu mara kwa Mara kuwakejeli na kuwakashifu viongozi wa vyama vya upinzani, na dhahama wanazopata viongozi wa vyama vya upinzani kutoka vyombo vya dola, ni kwa nini huyo Kibajaj asianze kwanza kumtuhumu Mwenyekiti wake wa Chama Cha Majipu, kuwa ndiye yupo mstari wa mbele kuivunja waziwazi hiyo Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?
Hazikutoshi wewe!! Maneno gani ya kashifa aliyoyasema kwa viongozi wa upinzani? Je chadema watamuadhibu Nasari kwa kuingia bungeni akiwa kalewa na akiwa na chupa ya Konyagi akiingianayo ndani ya bunge. Hali hii viroba vimezuiwa je wakati vilipokuwapo hali ilikuwaje?
 
Kama unania ya kumwambia mwenzako ukweli kwa lengo la kutaka kumurekebisha,kitu cha kwanza wewe mwenyewe unatakiwa ufanane na ukweli unaotaka kumwambia mwenzako.

Kwanza yeye mwenyewe ndiye kamdhalilisha mh Rais kwa kumuona kuwa siyo mtu makini katika utendaji wake kwa kumufukuza waziri kazi kwa kuzaniwa tu kalewa.

Wakati picha zipo zinazomuonyesha waziri akiwa amelewa chakari kitu ambacho kinathibitisha kuwa maamuzi ya mh rais ya kumufukuza waziri kazi hayakuwa ya kubahatisha ili kuwa ni halali mh rais kufanya kama alivofanya.

Pia kitendo cha kuambiwa kuwa Nasary alikamatwa na chupa ya konyagi nao ni ubabaishaji ulelule,chupa ya konyagi ni kitu ambacho kinaonekana kwanini Nasary asipigwe picha wakati anakamatwa akiwa na chupa yake watu tukamuona kama tulivyo muona mh Kitwanga akiwa ameusokota ugimbi?.
Kamera za ulinzi zipo za kuthibitisha. Wewe nani katika kudhibiti nidhamu ya mbunge kwa sasa hata upewe vielelezo? Chama chake kimepewa taarifa. Kama kitachukuwa taarifa sawa. Kama Nasari yumo katika kutekeleza malengo ya chadema bungeni sawa watamzawadia. Maana malengo ya chadema nikulifanya bunge kuwa kasino.
Lusinde yupo sawa kusema Kitwanga alidhaniwa kuwa kalewa. Mpaka sasa hakuna kipimo kilichofanywa kuthibitisha kuwa kiwango cha ulevi alichokuwa nacho kitwanga kwa siku ile. Kunakiwango cha ulevi cha kawa huwa hakina madhara.
 
Hivi kitwanga aliwajibishwa na chama?Sitetei suala la Nassari ila naona Lusinde anasema uongo kujenga hoja yake!
Kwa kosa lipi alilofanya Lusinde? Huna sababu za kujihami nyie chadema huenda mnalengo la kulifanya bunge kasino,bar,kilabu.
 
Vijana wengi bado hatujampokea yesu xo kunywa divai ni kawaida kupunguza mastress fulan xo kulewa n matokeo ya kunywa kupita kiasi chadema hatumwajibishi nasari tunamwonya.ixhu ya kitwanga ilikua ni kiki tu kuipotezea lugumi lkn watanzania tulidanganywa ni kujibu maswali kilevi watanzania tushaamka wala la Joshua Nassari halimpotezei heshima yake nayo pia ni kiki ya kumwanzishia mjadala
 
Kwa kosa lipi alilofanya Lusinde? Huna sababu za kujihami nyie chadema huenda mnalengo la kulifanya bunge kasino,bar,kilabu.
Hebu rudia ulichoandika!Nani kasema lusinde kafanya kosa?Ukurupukaji tu kama ngosha
 
MBUNGE wa Jimbo la Mtera, Livingstone Lusinde amewataka wabunge kujiheshimu na kuheshimu wenzao, kama kweli wanataka kuheshimika huku akilaani kitendo cha mbunge wa chama hicho, Dk Godwin Mollel kupuuza hatua zinazochukuliwa dhidi ya watu wanaochukuliwa hatua kwa kumtukana Rais John Magufuli kupitia mitandao.

Alisema inashangaza kuona mbunge huyo akitaka Serikali iache kushughulika na mambo yanayoitwa madogo, yakiwemo kama ya kumtukana Rais. Awali, akichangia hotuba za bajeti za wizara mbili zilizopo Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) na ile ya Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dk Mollel ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Siha, aliwataka Watanzania kubadilisha fikra, huku upande serikalii akiisihi iache kushughulika na mambo madogo, akitolea mfano wanaoshughulikiwa kwa kumtusi Rais.

Lakini Lusinde, alikemea hilo, akisema; “Haiwezekani Rais atukanwe, halafu Mbowe aheshimiwe…Rais anafanya kazi kubwa sana ya kubadilisha mfumo wa uongozi wa nchi hii… Dokta (Mollel) hapa amezungumzia suala la kubadilisha fikra, na huu ni mchango wake wa pili wa aina hii, anasisitiza hilo, kwanza tuwe na mtazamo mpya ili tusonge mbele….

“Anasema tuache kushughulika na watu wadogo wanaomtukana Rais na badala yake tuhangaike na mambo makubwa…aah, ila dokta huyo huyo anayetutaka tubadilishe fikra anasema kiongozi wa kambi ya upinzani aheshimiwe, ni mtu mkubwa. Yaani Rais atukanwe, Mbowe aheshimiwe? Hatuwezi kwenda hivyo, kama tunataka heshima. Tukiheshimiana hapo tutaona kuendesha nchi ni kazi rahisi.”

Alisisitiza suala la kutukanwa si dogo, hivyo viongozi wa vyama vingine vya upinzan wasilee matukio ya aina hiyo, bali waungane kumuunga mkono Rais na serikali yake kwa ajili ya ustawi wa nchi. “Mimi naamini Rais anafanya kazi nzuri kabisa ya kuubadilisha mfumo wa nchi hii. Kazi yetu kubwa isiwe kumrudisha nyuma, tumpe moyo, tumtie nguvu Rais wetu, tuwatie nguvu mawaziri wasukume mbele gurudumu la maendeleo.

“Hivyo naomba tunapozungumzia heshima tuzungumzie pande zote mbili,” alisema na kuimwagia sifa serikali kuwa inafanya kazi kubwa kiutendaji, akitolea mfano Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Kazi inavyozikabili kero za ardhi. Akikazia suala la heshima, alisema anasikia kuna mbunge wa upinzani (Joshua Nassari wa Chadema) juzi aliingia maeneo ya Bunge akiwa na pombe aina ya Konyagi, hivyo kutaka awajibishwe na chama chake.

“Sisi juzi juzi tu hapa Serikali imemwajibisha Kitwanga (Charles, aliyevuliwa Uwaziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi) kwa kudhaniwa tu amelewa, lakini leo mbunge anaingia na konyagi maeneo ya bunge na anakamatwa. “Sasa leo hii tunataka kuona meno yenu yako wapi, kwa kumwajibisha huyo mbunge, kama mtaweza maana kazi yenu ni kusema tu siyo kutenda. Tunataka kuona mtakuwa wakali kwa kiwango gani kwa mbunge anayekuja bungeni amelewa halafu ana chupa ya konyagi. Sisi tumeshaonesha njia, waziri amekuja amelewa amewajibishwa, sasa ninyi mtachukua hatua gani? alihoji.

Source Habarileo online
Huyo lusinde hajawahi kua na akili pia upeo wake wa kufikiri ni mdogo kma punje ya mchele
 
Hebu rudia ulichoandika!Nani kasema lusinde kafanya kosa?Ukurupukaji tu kama ngosha
Niliona nikupe jibu lenye hadhi kwa swali lako la kipuuzi. Kwa kuwa Kitwanga hakuadhibiwa na chama Nasari hana wa kumuadhibu. Kila mbunge anayo mamlaka yake ya nidhamu ikiwamo chama chake.
 
Niliona nikupe jibu lenye hadhi kwa swali lako la kipuuzi. Kwa kuwa Kitwanga hakuadhibiwa na chama Nasari hana wa kumuadhibu. Kila mbunge anayo mamlaka yake ya nidhamu ikiwamo chama chake.
Nani kapinga hilo?Nilichosema ni kuwa Lusinde asitumie uongo kujenga hoja yake,full stop!
 
Nani kapinga hilo?Nilichosema ni kuwa Lusinde asitumie uongo kujenga hoja yake,full stop!
Uongo upi? Nasari kakamatwa na walinzi wa bunge ikiwa amelewa na anachupa ya konyagi. Jamani laana hupati kwa baba na mama tu. Nasari anasumbuliwa na laana ya Mwakyembe.
 
Kamera za ulinzi zipo za kuthibitisha. Wewe nani katika kudhibiti nidhamu ya mbunge kwa sasa hata upewe vielelezo? Chama chake kimepewa taarifa. Kama kitachukuwa taarifa sawa. Kama Nasari yumo katika kutekeleza malengo ya chadema bungeni sawa watamzawadia. Maana malengo ya chadema nikulifanya bunge kuwa kasino.
Lusinde yupo sawa kusema Kitwanga alidhaniwa kuwa kalewa. Mpaka sasa hakuna kipimo kilichofanywa kuthibitisha kuwa kiwango cha ulevi alichokuwa nacho kitwanga kwa siku ile. Kunakiwango cha ulevi cha kawa huwa hakina madhara.
Walioleta picha za kitwanga zilizonashwa na kamera za ulinzi za bunge akiwa amelewa wananijua mimi nina ndiomaana wakanionyesha hizo picha,na tunachokijua ni kwamba Kitwanga alitumbuliwa na mh rais kwa kosa la kuingia bungeni akiwa amelewa,sasa kama alikuwa anazaniwa kuwa alikuwa kalewa kwa sababu hakuna kipimo kilichothibitisha ulevi wake na kama ulevi wake ulikuwa ni wa kawaida usiokuwa na madhara yoyote,hayo ni ya kwenu,tunachokijua ni kwamba mh rais ni kipimo sahihi tosha cha kutosha kuthibitisha kuwa Kitwanga alikuwa amelewa na mh rais ni mtu makini ndio maana kachukua maamuzi makini kwa kumtumbua Kitwanga kwa ulevi.

Mnadai kuwa Nassary aliingia bungeni akiwaameshika chupa ya konyagi,na kwamba kamera za bunge za usalama ziliweza kumunasa akiwa ameshika chupa ya konyagi na kwamba picha hizo zimekabidhiwa kwenye chama chake,mkisubiri hatua zitakazochukuliwa na chama chake.

Kwa Kitwanga mnahitaji kipimo ambacho kingeweza kuthibitisha kuwa ni kweli Kitwanga alikuwa amelewa pamoja na kuonyesha kiasi cha ulevi alichokuwa nacho.Je kwa Nassary mulitumia kipimo gani kuthibitisha kuwa chupa ya konyagi aliyokuwa amebeba na Nassary ilikuwa na kilevi ndani?.
 
wacha uongo. toa mifano rais ametukana au amekejeli upinzani zaidi ya kufanya utani tu unaokubalika kwenye siasa zetu. huwezi kulinganisha na matusi kwenye mitandao ambayo ina mikono ya wapinzani. mtu kama lissu na lema wamekua mfano wa lugha ya kejeli na matusi kwa rais wa jamhuri
Duh, kweli ukipenda chongo huitwa kengeza. Weww kebehi, dharau na majivuno yote anayotamka mkulu unasema ni utani!! Uko serious kweli au ubongo wako wa kupamabanua mambo umekreck?
 
Ukiona chipa ya Dawa usidhani ni Dawa yaweza kuwa dumu na ukiona chipa ya Maji usidhani kuna Maji .
Ili ikubaliwe kuwa ni konyagi Lusinde anajua taratibu(mkemia)
 
Ni uzezeta kusema umpe nguvu kiongozi wakati analipwa mshahara na marupurupu kibao. Kila kiongozi atimize wajibu wake,sio rais,waziri au kiongozi yoyote anze kulalamika watu awamsapoti wakati mwisho wa mwezi anapata mshahara.
 
Back
Top Bottom