Livingstone Lusinde amewataka CHADEMA Wamuadhibu Joshua Nassari | Page 2 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Livingstone Lusinde amewataka CHADEMA Wamuadhibu Joshua Nassari

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Msororo69, Apr 21, 2017.

 1. M

  Msororo69 JF-Expert Member

  #1
  Apr 21, 2017
  Joined: Feb 27, 2016
  Messages: 2,046
  Likes Received: 588
  Trophy Points: 280
  MBUNGE wa Jimbo la Mtera, Livingstone Lusinde amewataka wabunge kujiheshimu na kuheshimu wenzao, kama kweli wanataka kuheshimika huku akilaani kitendo cha mbunge wa chama hicho, Dk Godwin Mollel kupuuza hatua zinazochukuliwa dhidi ya watu wanaochukuliwa hatua kwa kumtukana Rais John Magufuli kupitia mitandao.

  Alisema inashangaza kuona mbunge huyo akitaka Serikali iache kushughulika na mambo yanayoitwa madogo, yakiwemo kama ya kumtukana Rais. Awali, akichangia hotuba za bajeti za wizara mbili zilizopo Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) na ile ya Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dk Mollel ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Siha, aliwataka Watanzania kubadilisha fikra, huku upande serikalii akiisihi iache kushughulika na mambo madogo, akitolea mfano wanaoshughulikiwa kwa kumtusi Rais.

  Lakini Lusinde, alikemea hilo, akisema; “Haiwezekani Rais atukanwe, halafu Mbowe aheshimiwe…Rais anafanya kazi kubwa sana ya kubadilisha mfumo wa uongozi wa nchi hii… Dokta (Mollel) hapa amezungumzia suala la kubadilisha fikra, na huu ni mchango wake wa pili wa aina hii, anasisitiza hilo, kwanza tuwe na mtazamo mpya ili tusonge mbele….

  “Anasema tuache kushughulika na watu wadogo wanaomtukana Rais na badala yake tuhangaike na mambo makubwa…aah, ila dokta huyo huyo anayetutaka tubadilishe fikra anasema kiongozi wa kambi ya upinzani aheshimiwe, ni mtu mkubwa. Yaani Rais atukanwe, Mbowe aheshimiwe? Hatuwezi kwenda hivyo, kama tunataka heshima. Tukiheshimiana hapo tutaona kuendesha nchi ni kazi rahisi.”

  Alisisitiza suala la kutukanwa si dogo, hivyo viongozi wa vyama vingine vya upinzan wasilee matukio ya aina hiyo, bali waungane kumuunga mkono Rais na serikali yake kwa ajili ya ustawi wa nchi. “Mimi naamini Rais anafanya kazi nzuri kabisa ya kuubadilisha mfumo wa nchi hii. Kazi yetu kubwa isiwe kumrudisha nyuma, tumpe moyo, tumtie nguvu Rais wetu, tuwatie nguvu mawaziri wasukume mbele gurudumu la maendeleo.

  “Hivyo naomba tunapozungumzia heshima tuzungumzie pande zote mbili,” alisema na kuimwagia sifa serikali kuwa inafanya kazi kubwa kiutendaji, akitolea mfano Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Kazi inavyozikabili kero za ardhi. Akikazia suala la heshima, alisema anasikia kuna mbunge wa upinzani (Joshua Nassari wa Chadema) juzi aliingia maeneo ya Bunge akiwa na pombe aina ya Konyagi, hivyo kutaka awajibishwe na chama chake.

  “Sisi juzi juzi tu hapa Serikali imemwajibisha Kitwanga (Charles, aliyevuliwa Uwaziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi) kwa kudhaniwa tu amelewa, lakini leo mbunge anaingia na konyagi maeneo ya bunge na anakamatwa. “Sasa leo hii tunataka kuona meno yenu yako wapi, kwa kumwajibisha huyo mbunge, kama mtaweza maana kazi yenu ni kusema tu siyo kutenda. Tunataka kuona mtakuwa wakali kwa kiwango gani kwa mbunge anayekuja bungeni amelewa halafu ana chupa ya konyagi. Sisi tumeshaonesha njia, waziri amekuja amelewa amewajibishwa, sasa ninyi mtachukua hatua gani? alihoji.

  Source Habarileo online
   
 2. mbikagani

  mbikagani JF-Expert Member

  #21
  Apr 21, 2017
  Joined: Dec 5, 2014
  Messages: 2,241
  Likes Received: 851
  Trophy Points: 280
  WEWE UNAFIKIRI KILA ANAYEPINGA UPUUZI UNOFANYWA NA WAPINZANI NI KIJANI?
  USHAHIDI ANAO ALIYETUAMINISHA.
  NA HAKUNA ALIYEPINGA.
   
 3. O

  Ohooo JF-Expert Member

  #22
  Apr 21, 2017
  Joined: Jul 8, 2015
  Messages: 804
  Likes Received: 996
  Trophy Points: 180
  Chama ndo kinamiliki bunge? Sema awajibishwe na bunge na sio chama. Kitwanga hakuwajibishwa na chama chake na hatuwezi kulaumu wala hakuna aliyekilaumu chama chake bali alilaumiwa yeye kitwanga na rais akamuondoa uwaziri. Nasari kama alikuwa hivyo bunge lina kanuni zake za kuweka kumwajibisha. Hakuna chama kinachofundisha ulevi hiyo ni hulika ya mtu mwenyewe
   
 4. M

  Msengapavi JF-Expert Member

  #23
  Apr 21, 2017
  Joined: Oct 23, 2008
  Messages: 4,802
  Likes Received: 2,748
  Trophy Points: 280
  Kitwanga alikuwa au ni mwanachama wa Chadema?
   
 5. M

  Msengapavi JF-Expert Member

  #24
  Apr 21, 2017
  Joined: Oct 23, 2008
  Messages: 4,802
  Likes Received: 2,748
  Trophy Points: 280
  Wewe na yeye na Bashite wot Bashite!
   
 6. Mkaruka

  Mkaruka JF-Expert Member

  #25
  Apr 21, 2017
  Joined: Feb 5, 2013
  Messages: 8,609
  Likes Received: 4,752
  Trophy Points: 280
  Wanywa pombe na mbege tu hao
   
 7. k

  kabombe JF-Expert Member

  #26
  Apr 21, 2017
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 15,575
  Likes Received: 8,517
  Trophy Points: 280
  Si umeona alivyotumbuliwa fasta?kwa sababu ccm sio chama cha wanywa viroba.Hivi lema au sugu wanaweza kumuadhibu Nasari?
   
 8. L

  LuSilk JF-Expert Member

  #27
  Apr 21, 2017
  Joined: Sep 14, 2016
  Messages: 785
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 80
  Duh ! Nashangaa walevi wanavyo mtetea mlevi mwenzao. Angekuwa si CDM ungesikia makelele yao,wakianzia na ' mwongozo mh.spika' !
   
 9. M

  Msengapavi JF-Expert Member

  #28
  Apr 21, 2017
  Joined: Oct 23, 2008
  Messages: 4,802
  Likes Received: 2,748
  Trophy Points: 280
  Hiyo ndo kazi aliyopewa na chama chake. Kwahiyo hiyo ni kazi ya sisiem. Once upon a time someone uttered an 'f' word na hakuwajibishwa. So you see, kibajaji is not alone.
   
 10. Mystery

  Mystery JF Gold Member

  #29
  Apr 21, 2017
  Joined: Mar 8, 2012
  Messages: 7,949
  Likes Received: 6,706
  Trophy Points: 280
  Kwa hao jamaa........

  Matusi, kashfa na kejeli ni 'official' language yao!
   
 11. flagship

  flagship JF-Expert Member

  #30
  Apr 21, 2017
  Joined: Jul 29, 2015
  Messages: 1,192
  Likes Received: 686
  Trophy Points: 280
  Duh!Kumbe la saba?
   
 12. MUSSA ALLAN

  MUSSA ALLAN JF-Expert Member

  #31
  Apr 21, 2017
  Joined: Oct 13, 2013
  Messages: 18,964
  Likes Received: 7,718
  Trophy Points: 280
  Kwahiyo LUSINDE ameingia kingi kwenye zile Propaganda za kitoto za Mwakyembe?

  Eti Usalama wa Taifa wamemkamata na KONYAGI na bado wakamruhusu aingie bungeni akiwa amelewa.

  haya majinga ya CCM huwa yanaona kila mtu ni mjinga kama wao!
   
 13. s

  stigajemwa JF-Expert Member

  #32
  Apr 21, 2017
  Joined: Nov 12, 2016
  Messages: 373
  Likes Received: 319
  Trophy Points: 80
  Kwani Nasari ana cheo gani huko chadema,tuanzie hapo.Kama ana wadhifa fulani ndani ya chama basi wamwajibishe.Lakini kama hana wadhifa, yapasa awajibishwe na wapiga kura wake.Bahati mbaya kile kipengele cha katiba pendekezwa ya warioba cha kumwajibisha mbunge kabla hata ya miaka mitano kilinyofolewa na wabunge wa ccm
   
 14. S

  Sexless JF-Expert Member

  #33
  Apr 21, 2017
  Joined: Mar 11, 2017
  Messages: 2,940
  Likes Received: 4,270
  Trophy Points: 280
  Swali lako zuri Sana Mkuu. Kibajaji kama yumo humu jukwaani analazimika kulitolea majibu.
   
 15. KIBEHA

  KIBEHA JF-Expert Member

  #34
  Apr 21, 2017
  Joined: Jul 14, 2013
  Messages: 255
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 45
  Haiingii akilini mtu unataka uitwe mheshimiwa kijana unakamatwa na mzinga wa konyagi ukiingia nayo Bungeni jamani Bungeni???? mmh ninamashaka km hiyo masters degree alikua anasoma huku amezimua,kweliiii??? hao wapiga kura wake kazi wanayo, yaani anategemea akili ya pombe ndio aweze kufanya "arguments" haibu gani hii sisi vijana tunaipata.
   
 16. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #35
  Apr 21, 2017
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,483
  Likes Received: 5,562
  Trophy Points: 280
 17. M

  Mkirindi JF-Expert Member

  #36
  Apr 21, 2017
  Joined: Mar 2, 2011
  Messages: 3,335
  Likes Received: 950
  Trophy Points: 280
  Hebu tujiulize Matajiri wakubwa hapa TZ, walio hai NA wali kwenda mbele ya muumba wao , amabao wamewacha biashara kubwa . JEE walikuwa NA elimu ya darasa la ngapi?

  Kwa mfano:

  1. Karimjee Jivanjee (Marehemu)

  2. Bhakresa

  Nk
   
 18. b

  bibinnaa JF-Expert Member

  #37
  Apr 21, 2017
  Joined: Jan 17, 2017
  Messages: 1,004
  Likes Received: 808
  Trophy Points: 280
  Napendekeza tuache kuongea habari zake tusije tujakawa kama yeye...I am afraid.
  Naibu wa Spika ni Daktari ktk Sheria...Spika ni Mwanasheria...why dont they stop him uttering such sentences.PBU inakuwa live wakati wa bunge la Kenya..those guys are serious and all of them talk sense.
   
 19. m

  mtanzania1989 JF-Expert Member

  #38
  Apr 21, 2017
  Joined: May 20, 2010
  Messages: 2,138
  Likes Received: 1,701
  Trophy Points: 280
  Wamuangalie vizuri na Mdee, bila shaka anaingia na bangi bungeni.
   
 20. B

  Batale JF-Expert Member

  #39
  Apr 21, 2017
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 1,064
  Likes Received: 439
  Trophy Points: 180
  Sikubaliani na kutukanwa raisi ,wabuge kwenda mjengoni wakiwa Maji. Mhm heshima huipata anayeheshimu pia, hivo nivyema tukaheshimiana.
   
 21. luginyo

  luginyo JF-Expert Member

  #40
  Apr 21, 2017
  Joined: May 26, 2013
  Messages: 1,158
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Lusinde kweli wewe darasa la saba Jembe la uongooo fyuuuu
   
Loading...