Live Updates: VPL, Singida United Vs Simba SC Namfua Stadium

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Patashika ya ligi kuu Tanzania Bara VPL, kuendelea leo uwanja wa Namfua Stadium kati ya Singida United na Simba SC.

Katika ligi kuu Tanzania Bara VPL, Singida United wanataka kulipiza kisasi, Huku Simba wanataka kuendelea rekodi yao ya kuchukua ubingwa bila kupoteza mchezo wowote .

Je, Singida United ama Simba SC kuibuka mbabe? Kaa nasi usikose ukaambiwa.. Kumbuka mtanange ni kuanzia saa 10:00 jioni.

IMG_20180512_155917_424.jpg
IMG_20180512_155933_090.jpg
IMG_20180512_155854_895.jpg
IMG_20180512_155835_486.jpg


Mpira umeanza uwanja wa Namfua Stadium ️.. Singida United 0-0 Simba SC

5' Matokea ni bila kwa bila, mpira ni mkali kwa timu zote mbili uwanja wa Namfua Stadium

16' Simba SC wakwenda kwake Mavugo lakini ni Offside ..

18' Kambale anakwenda na mpira kwake Kaseke lakini mpira ni utatoka nje, na unakuwa wa kurushwa kuelekea Singida United

Keni Ali anapiga mbele lakini Mohamad Hussein anazuia na kumpasia Okwii

24' Goo Goo Gooooooaaal Goooooaaaaal Shomari Kapombe anaandika bao la kwanza baada ya kazi nzuri ya Bocco

Pambano ni kali sana uwanja wa Namfua Stadium ️ Singida United 0-1 Simba SC

30' Okwii anapiga mbele lakini anafanyiwa faulo.. Inapigwa lakini haina madhara

31' Batambuzi anapiga shuti kali sana.. Lakini ni goal Kick

33' Ni faulo kuelekea Simba SC.. Inapigwa lakini mpira utatoka nje

Singida United wanashambulia lango la Simba SC.. Lakini mashambulizi yao wanashidwa kuleta matunda

Katikati ya uwanja kwake Mkude, anakwenda kwake Okwii mpira utatoka nje

38' Singida United wanapata kona.. Inapigwa kona lakini inatoka nje na kuwa goal Kick

39' mpira umesimama baada ya mchenzaji Kaseke kupata rabsha.. Ameinuka mpira unaendelea

43' John Bocco yuko chini baada ya kupata rabsha katika mchezo huu wa VPL…

Mpira unaendelea kwake Okwii, kwake Shomari lakini beki wa Singida United anakoa

45+2 ..kuelekea mapumziko katika mchezo huu wa VPL

Naam dakika 45' za kipindi cha kwanza za mchezo wa ligi kuu Tanzania zimemalizika.. Na Simba SC wakiwa mbele kwa goli moja kwa bila.

Singida United 0-1 Simba SC uwanja wa Namfua Stadium

Kipindi cha pili kimeanza uwanja wa Namfua Stadium

46' mpira kama ulivyoanza kipindi cha kwanza.. Ni mashambulizi kwa pande zote mbili.

50' Kaseke anakosa goli la wazi kabisa ilikuwa nafasi nzuri

52' Niyonzima anaingia kuchukua nafasi ya Mavugo upande wa Simba SC

Bocco agonga kichwa lakini golikipa wa Singida United anaokoa

56' Kambale anakwenda kwenye benchi na anaingia Usengimana.. Upande wa Singida United

60' Singida United 0-1 Simba SC, uwanja wa Namfua Stadium

63' Salum, Chuku anakwenda kwenye benchi na anaingia E.Sumbi upande wa Singida United

Miraj anakwenda na mpira.. Lakini anapoteza kwake Niyonzima anapiga mbele lakini mabeki wanaokoa

Batambuzi anakwenda.. Anapiga bunduki lakini golikipa Manula anaweka katika himaya yake

70' Singida United wanapata faulo.. Ni eneo hatari.. Inapigwa lakini inakuwa goal Kick

71' Golikipa Manula anapewa kadi ya njano.. Uwanja wa Namfua Stadium

74' Ni faulo kuelekea Singida United.. Inapigwa na Bukaba lakini mpira utatoka nje ni wa kurushwa

76' Ndemla anaingia kuchukua nafasi ya Kotei.. Upande wa Simba SC

Mpira uko balance kwa pande zote mbili uwanja wa Namfua Stadium ️ Singida United 0-1 Simba SC

Inapigwa faulo kuelekea Simba SC.. Lakini mchenzaji Mlipili anatokea na kuokoa hatari ile

85' Okwii anakwenda kwenye benchi na nafasi yake aningia Kichuya

Kenny anapewa kadi ya njano. Kwa kujirusha eneo la hatari

Kichuya anapiga shuti kali. Lakini ni goal Kick

Ni faulo kuelekea Simba SC..inapigwa lakini haina madhara

90+4 kuelekea kumalizika mtanange huu wa VPL. Uwanja wa Namfua Stadium

Singida United 0-1 Simba SC

90+4' Naam mpira umekwishaaaaaaaaa uwanja wa Namfua Stadium ️. Simba wakitoka kifua mbele kwa goli moja kwa bila dhidi ya Singida United

Singida United 0-1 Simba SC

Asanteni ..Ghazwat
 
Pambano ni kali kwa timu zote mbili uwanja wa Namfua Stadium

Singida United 0-0 Simba SC
 
Back
Top Bottom