Live Update: Azam FC v Oljoro JKT FC

Live Update: Azam FC v Oljoro JKT FC

Makoye Matale

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2011
Posts
6,490
Reaction score
2,104
Leo, pamoja na kuwa na mechi nyingine katika viwanja vya Manungu na Mkwakwani, mechi inayovuta hisia za mashabiki wa soka ni ile ya Chamazi kati ya Azam FC na Oljoro JKT. Azam yenye point 21 inaweza kuiporomosha Simba kutoka nafasi ya 2 hadi ya 3 endapo itashinda na kufikisha point 24. Kwa sasa Simba ina point 23.

Mlioko Chamazi tunaomba Live Update.
 
Mimi siko Chamazi, wewe huwezi kufanya maarifa tukapata updates?
 
Azam wanaongoza kwa goli moja.
Goli limefungwa na Kipre Tchetche dakika ya 3 kwa penalti.
 
game over ujoro kala 1 bila mpka sasa ni nafasi ya 2..
 
full time/ azam 1 orjoro 0....jahazi la rage linazidi kuzama maskini:nimekataa
 
ndetichia unatonesha vidonda vya watu .wenyewe [simba] wakipata matokeo wtapigana tena

La kuvunda halina ubani. Kaseja kafanya mengi Msimbazi lakini leo anashutumiwa vibaya, hakika shukrani ya punda ni mateke.
 
La kuvunda halina ubani. Kaseja kafanya mengi Msimbazi lakini leo anashutumiwa vibaya, hakika shukrani ya punda ni mateke.

[h=5]KASEJA ABWAGA MANYANGA SIMBA SC
NAHODHA wa Simba, Juma Kaseja amewaaga wachezaji wenzake na kuwaambia yeye na klabu hiyo basi.
BIN ZUBEIRY amefika kwenye mazoezi ya Simba jioni ya leo Uwanja wa Kinesi, Urafiki, Dar es Salaam na kukuta wachezaji wote wakiendelea na mazoezi kujiandaa na mechi ya Toto African mwishoni mwa wiki, kasoro Kaseja na Amir Maftah.
Alipoulizwa Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga alisema kwamba Maftah ana ruhusa maalum kwa sababu ameoa hivi karibuni, lakini Kaseja hawana taarifa zake, ila; "Nadhani hatakuwa vizuri kisaikolojia baada ya kufanyiwa fujo Jumamosi,"alisema Kamwaga.
Lakini BIN ZUBEIRY ilipozungumza na wachezaji wenzake, walisema Nahodha wao amewaaga kwamba yeye na Simba basi, kwani ameumia sana kwa jinsi alivyodhalilishwa na mashabiki Jumamosi Morogoro.
"Juma hapa ndio basi kaka, Kasema yeye na Simba basi, amesononeshwa mno na jinsi alivyodhalilishwa baada ya mechi ya Morogoro,"alisema mchezaji mmoja wa Simba baada ya mazoezi Kinesi leo.
Kaseja alitukanwa na kutishiwa maisha na mashabiki wa Simba baada ya mechi dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro wakimtuhumu kufungwa mabao ya kizembe.
Lakini tayari uongozi wa Simba umelaani vikali vurugu na vitisho alivyotolewa kipa wao huyo namba moja, na kusema wanafikiria kuwachukulia hatua kali watu waliomfanyia hivyo Nahodha wao huyo.
Juhudi za kumpata Kaseja mwenyewe kuzungumzia suala hilo, hazikuweza kufanikiwa kwani simu yake ilikuwa haipatikani.
[/h]
 
bado mechi 14 kitaeleweka tu nani champions ni mnyama,lambalamba au yebo2
 
Back
Top Bottom