Simu ya android ndio simu gan?
android ni operating system inayotumika kwenye mobile devices, ile ideos uliyoikosa kwa elfu hamsini inatumia android os!
kale kasimu sijui nikafate! Kwahiyo najuaje kama simu yangu operating system yake ni android.
unaweza weka model ya cm yako ktk mtandao huu www.gsmarena.com na utapata specification zake ikiwa ni pamoja na kujua operating system inayotumia
Inawezekana sana tu kwa internet hii ya tz mbona mm naitumia kwa kutumia voda internet na haina shida sema uktaka faidi jiunge unlimited package coz inakula bundles si mchezo
nimeingi hapo, nimesearch simu yangu ila katika specifications walizotoa sijaona sehemu waliyoelezea OS
samsung,sony ericsson,google nexus,htc,ideos ndo mostly zinatumia android os,hasa hizi za sasa
Minimum connection speed ni bite ngapi.
nimeingi hapo, nimesearch simu yangu ila katika specifications walizotoa sijaona sehemu waliyoelezea OS
kumbe ningekesha kuitafuta nokia. Ahsante.
basi wewe haumo kwenye list ya lizzy hivyo live tv imekupitia pembeni, kwanza mpwapwa kuna 3g?
Kama una tablet au simu ya android , bila kusahau internet inayoeleweka unaweza ukafurahia kuangalia TV online.
Uzuri wa hii app (tofauti na nyingine nyingi) haikupeleki kwenye website za kizushi, unabadili tu channel kulingana na interest yako.
Baadhi ya channel zilizopo ni NRJ (Paris, Pure, Pop/Rock, Urban na dance) + MTV kwaajili ya music, Eurosport na ESPN kwaajili ya michezo, CNN + BBC + Aljazeera kwaajili ya taarifa ya habari, Star Tv hii naona ina makorokoro ya kila aina, Fox Crime + National Geography + History channel, NASA tv, CINE(+) + Fox movies + Movies kwaajili ya movies pia Cartoon Network na Disney Channel.
Hizo ni baadhi tu (zile zinazonivutia mimi) kwahiyo kama na wewe unataka kufaidi na nyumbani huna king'amuzi nenda tu kwenye Android market utafute LIVE TV (sio zaidi wala pungufu) alafu udownload.
Hamna malipo ya aina yoyote ile.
Nilimaanisha malipo ya ziada (kulipia app, channel zenyewe).Hapo kwenye red, nadhani malipo yake ni makubwa sana kuliko tunavyodhani. Just imagine MBs zinazokwenda wakati wa streaming, umejaribu ku calculate unatumia MB ngapi kwa saa moja? Kimsingi malipo yapo tena sana tu japo si kwa tv stations zenyewe ila kiasi kinachotozwa na hii mitandao yetu najua hata wewe unafahamu mkuu.
Lakini fine, kwa kuwa vipato vyetu vinatofauriana labda kwa wengine inaweza isiwe shida sana.Mimi mwanzo nilidhani hii ni bora kuliko DSTV maana unapata channels nyingi sana lkn nilipoanza kutumia ndipo nilipogundua uzito wake.
But it's fine, watu wajaribu watatoa majibu yao.