Live on star TV mtazamo baada ya matokeo ya Arumeru

Live on star TV mtazamo baada ya matokeo ya Arumeru

Yahya Mohamed

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2010
Posts
270
Reaction score
317
Karibuni kwa michango na mezzo yenu Wana JF tukiakisi matokeo ya UCHAGUZI mdogo Arumeru na safari ya demokrasia ya ukweli nchini
 
ushindi wa arumeru pamoja na kata nyingine uliotokea jana ni alama kuwa ELIMU YA URAIA NI SILAHA TOSHA YA KUPAMBANA na ubakaji wa demokrasia na wizi wa kura

pia ni alama kuwa 2015 ambapo kila mbunge atakuwa anapambana na upandde wake CCM itakuwa na hali ngumu....

lakini cha msingi wanaweza kulainisha mambo kwa kucheza fair politiks kama za akina january makamba ili angalau kuwepo sokoni.... na waachane na wahuni kama kina lu....de na waimba taarabu....watu wanataka uwajibikaji tu....not longolongoi.....

tuko pamoja mkuu
 
Nipo nawafuatilia live toka huko Arumeru ila jambo moja tu linanitatanisha kuhusu facial expression yako wewe YAHAYA M. Nahisi kama hujapenda chadema kushinda uchaguzi huu.!!
Sema basi "PEOPLESSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSS...!!!!
 
Tafadhali ndugu Yahaya hapo studio tunaomba jaribuni kutuletea matokeo ya chaguzi ndogo (udiwani) zilizofanyika hapo jana.
Peoplesssss POOOOOOWWWWWWEEEEERRRR..!!!??
 
Kweli Yahya hebu tujuzeni vizuri tujue matokeo halisi ya UDIWANI, nani kaongoza kwa kiwango gani nk
 
magamba chali.chadema huree!nashauri chadema wajipange vizuri vijijini.mijini wawahamsishe sana vijana wajiandikishe ili 2015 tuikomboe tanzania kutoka kwa mafisadi
 
mwanzo wa ngoma ni lele. Afadhali hata CCM dalili za kuanguka mnaziona, kuliko yawapate yaliyotokea kwa UNIP ya Zambia. wananchi wameanza kuichallenge CCM waziwazi. Kampeni za Raisi mstaafu,Waziri Mkuu mstaafu, Wabunge wa chama tawala, zote hazikufua dafu kwa kijana mdogo asiye na mke, anayeishi kwa wazazi wake.
 
Uchache wa wapiga kura Arumeru tatizo elimu ndogo ya uraia. TUME YA UCHAGUZI LAZIMA IWE KAMA TAASISI YENYE WAFANYAKAZI KILA WILAYA AMBAO WATAFANYAKAZI YA KUTOA ELIMU YA URAIA WAKATI WOTE NA ITASAIDIA KURUDISHA IMANI KWA WAPIGA KURA KWANI KUNABAADHI YA WAPIGAKURA HAWAONI UMUHIMU WA KUPIGA KULA KWANI HAWANA IMANI NA TUME YA UCHAGUZI. Siamini kuwa tume haiwezi kuwa na watumishi kwenye kila wilaya badala ya kutumia wakurugenzi ambao wengi wanamajukumu mengi. Kama pcb wameweza kwanini tume ishindwe. Watanzani wengi hawana elimu na wengi tu hawajui kusoma.
 
mkuu wa kaya baada ya kukicost chama kwa kukaa kimya na mijambazi yake kina ngeleja,luhanjo,uttoh,ekelege,mtasiwa,nyoni na mafisadi wengine ambao bado hawajahukumiwa mpk leo pamoja na mitume kibao iliyoundwa na bunge na kutoa mapendekezo ya hukumu dhidi yao,sasa naamini wanatafuta mchawi lkn kwa mtanzania wa leo atatoa hukumu iliyoshindwa kutolewa na serikali kwa kupitia sanduku la kura,hizi ndizo hasira za watanzania kwa serikali inayoshindwa kutimiza wajibu wake, VIVA CDM
 
Nipo nawafuatilia live toka huko Arumeru ila jambo moja tu linanitatanisha kuhusu facial expression yako wewe YAHAYA M. Nahisi kama hujapenda chadema kushinda uchaguzi huu.!!
Sema basi "PEOPLESSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSS...!!!!
Hii nimeipenda Mkuu usingizi bwana
 
Ni wakati muafaka sasa watawala wa nchi wakatambua kuwa matakwa ya wananchi yaheshimiwe na ghiriba, longolongo na ubabaishaji wa aina yoyote hauna nafasi tena kwa kwa watanzania

Na kubwa zaidi ni kuwa viongozi watambue kuwa haki ni msingi wa amani yetu.
 
Jambo nililijifunza katika uchaguzi huu na ambalo lilijitokeza pia wakati wa uchaguzi mkuu ni kuwa vyombo vya dola vijipange vizuri na viache kuwa na wasiwasi usiokuwa na sababu. vurugu nyingi zimekuwa zikitokea wakati wa kuhesabu kura au kutangaza matokeo ambayo tayari watu wanakuwa wanayo kutokana na mitandao. jana watu walitoka kwenye vituo vyao huko milimani wakashika Usa kuja kushangilia baada ya kutumiana matokeo kwa mitandao. polisi walipawsa kuhakikisha kuwa watu wanakaa mita 100+ kutoka kituoni kama sheria inavyotaka na siyo kuwaamuru waondoke. kwa watu ambao wana imani ndogo na tume na vyombo vya dola tafsiri inakuwa kwamba zenge linataka kupenyezwa na hivyo wanagoma kutoka hatimaye mabomu yanapigwa. ikumbukwe kuwa demokrasia siyo tu kupiga kura kwa utulivu bali pia kuhesabu kura na kutangaza matokeo halisi kama kura zilivyohesabiwa. Nawapongeza Chadema kwa ushindi wa ARUMERU, Mwanza, Mbeya na Songea.
 
Kwanza kabisa! Ushindi wa CDM ni salamu tosha kwa chama tawala kuwa, mambo ya kulindana, kupeana vyeo pamoja na kufanya hii nchi ni ya watu fulani fulani yana mwisho. Haiwezekani ukitoka Arusha mjini kwa gari kuelekea upande wowote, huwezi kuamini kwa namna ambavyo wananchi wanavyoishi bila huduma za msingi, ifike wakati sasa viongozi wetu waone aibu, wajione ni sehemu ya binadamu wengine waishio hapa nchini. Na hii inawezekana kama watu watapewa fursa ya kuchagua viongozi wanaowataka.
 
Hii nimeipenda Mkuu usingizi bwana

Pole sana kwa kuzidiwa na usingizi uliokubana hayo yote ni kudhirisha kuwa wewe nawe umekesha kusubiria saa ya ukombozi.
teh teh teh nimekutania tu bwana schoolmate(SAUT) wangu, endelea kutujuza yanayojiri huko.
 
Kwa waliokuwa mjini jana(arusha)sherehe zilianza mapema kabisa,makundi ya watu yalikuwa yametawanyika kila kona wakisherehekea ushindi wa chadema
 
mkuu wa kaya baada ya kukicost chama kwa kukaa kimya na mijambazi yake kina ngeleja,luhanjo,uttoh,ekelege,mtasiwa,nyoni na mafisadi wengine ambao bado hawajahukumiwa mpk leo pamoja na mitume kibao iliyoundwa na bunge na kutoa mapendekezo ya hukumu dhidi yao,sasa naamini wanatafuta mchawi lkn kwa mtanzania wa leo atatoa hukumu iliyoshindwa kutolewa na serikali kwa kupitia sanduku la kura,hizi ndizo hasira za watanzania kwa serikali inayoshindwa kutimiza wajibu wake, VIVA CDM

Spot on mkuu! I concur!
 
Back
Top Bottom