Live lectures toka AfroIT | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Live lectures toka AfroIT

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Kilongwe, Jan 16, 2011.

 1. Kilongwe

  Kilongwe JF-Expert Member

  #1
  Jan 16, 2011
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 424
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  [​IMG]

  Katika kepeleka gurudumu la maendeleo mbele,timu nzima ya AfroIT inatarajia kuanza kutoa lactures mbalimbali za fani kedekede live.Kwa kuanzia tutaanza na zile za ICT na Biashara(Economics,management,Leadership nk) bila gharama yoyote.Kwa siku za usoni kutegemeana na walimu tutatanua wigo kwa fani zaidi.


  Hii itakuwa ni kama upo darasani ambapo washiriki wataweza kupata wasaa wa kuuliza maswali,kujibu maswali na mengineyo. Hauitaji programu yoyote zaidi ya internet,browser na microphone(ni muhimu kwakuwa ni dhahiri utataka kuuliza maswali kwakuwa mtindo wa kufundisha ni ule wa ushirikiano zaidi),au webcam(ni option kwa wasikilizaji na ni lazima kwa mtoaji somo(mwalimu).)

  Ratiba ya vipindi na link ya kila kipindi inapatikana HAPA .

  Kama unataka kushiriki kutoa somo basi usisite kuwasiliana na timu ya AfroIT kwa kutuma e mail kwenda podcast@afroit.com

  Muhimu: Kwakuwa tumeanzisha programu mbili kwa pamoja,kuna uwezekano watu wakachanganya ipi ni ipi,Webcast inapatikana kwa wiki mara moja tena kwa idadi maalum ya washiriki ambao wanahitajika kujiandhikisha kwa kutuma e mail kwenda podcast@afroit.com,ndani ya webcast washiriki mbalimbali watakuwa wanajadili hoja husika Live toka pande mbalimbali za dunia,ila Live lactures itakuwa kila siku ambapo kutakuwa na mtoaji somo(mkufunzi) na wengine wote ni wasikilizaji(wanafunzi) ambapo hakuna haja ya kujiandikisha,ingawa kutokana na sababu za kiufanisi na kiuchumi kutakuwa na limit ya namba ya washiriki hivyo wakwanza kuingia ndiye atapata nafasi(FIFS),kila darasa halizidi watu 20.

  Tunahamasisha wanajamii mbalimbali kushiriki kutoa masomo kwa jamii.
   
Loading...