Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 59,976
- 135,169
Wanabodi,
Kama kawaida yetu JF, be the first to know, niko hapa Hoteli ya Hyatt Regency, (zamani Kilimanjaro Kempinski), kwenye hafla ya uzinduzi wa malipo kwa njia ya mtandao, kwa kutumia simu ya mkononi, kulipia huduma zote za kibiashara zinazotolewa na Tanzania Chamber of Commerce Industry and Agriculture (TCCIA), zikiwemo certificates of orgin, katika mtindo unaitwa (LIPA FASTA). Mfumo huu, umegharimiwa na taasisi ya TradeMark, East Africa, ambapo kwa sasa Mkurugenzi Mkazi wa TradeMark East Africa kwa Tanzania, John Ulanga, anazungumza.
Taasisi ya Trademark East Africa, imepongezwa kwa kuiwezesha Tanzania, kuwa ndio nchi inayoongoza nchi zote za Afrika ya Mashariki, kwa matumizi ya mifumo ya malipo kwa njia ya Mtandao, kulipia huduma mbalimbali za kibiashara, hivyo kupunguza gharama za kufanya biashara na wakati huo, kuifanya Tanzania kuwa ni nchi ya mfano wa kuingwa na nchi nyingine za Afrika ya Mashariki, katika kuboresha mazingira ya kufanya biashara.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) Mhandisi Raymond Mbilinyi, (katikati) akibonyeza kitufe kuzindua Mfumo wa malipo kwa mtandao, kutumia simu za mkononi Kulipia huduma za TCCIA ujulikanao kwa jina la LIPA FASTA. Mfumo huo umefadhili wa na TradeMark East Africa (TMEA), kwa Chama cha Wafanyabiashara, wenye Viwanda na Kilimo cha Tanzania, TCCIAA
Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi wa TMEA, Tawi la Tanzania, John Ulanga amesema, "Sisi kama TMEA tuna furaha kubwa kusaidia mfumo huu wa LIPA FASTA kufanya kazi kwa lengo la kuboresha mazingira ya kufanya biashara Tanzania, hivyo kukuza biashara na kuleta ufanisi wa biashara kwa Tanzania.
Ulanga amesema TMEA imetumia zaidi ya Dola za Marekani, $ 600,000 katika kufanikisha mradi huu kwa kwa Chama cha Wafanyabiashara, wenye Viwanda na Kilimo cha Tanzania, TCCIA, lakini pia unahusisha Chama cha Wafanyabiashara, wenye Viwanda na Kilimo cha Zanzibar, (ZNCCIA), Fedha za kugharimia mpango huu, zimetolewa na Serikali ya Uingereza kupitia Shirika lake la Maendeleo la kimataifa, (DFID) kupitia TradeMark, East Africa, (TMEA) inayosimamia utekelezaji wa mradi huo.
Ulanga amesema maboresha ya biashara, yanafungua zaidi fursa za Watanzania kufanya biashara, kilichobaki ni kwa Watanzania kuchangamkia fursa hizo, kwa hoja kuwa fursa hazingoji mtu, tukishindwa kuzichangamkia fursa hizi, zitachangamkiwa na wengine.
Kwa upande wake, Rais wa TCCIA Ndibalema Mayanja amesema "Tunaishukuru sana TMEA kwa misaada wa kugharimia mfumo huu, muhimu ambao utaokoa muda na kupunguza gharama, kwani muda ni mali muhimu sana kwa mfanyabiashara yoyote, ukiokoa muda, umeokoa fedha na umeongeza faida”, hivyo LIPA FASTA itaongeza kasi ya usajili wa vyetu vya uasili kuongeza kasi ya kufanya biashara.
Paskali