Lissu: Wananchi wanaweza kuwashitaki mawaziri ambao hawajaapa

Kibo10

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
11,277
8,850
Mwanasheria machachari Mh Tundu Lissu amesema Wananchi wana haki ya kuwashtaki mawaziri ambao wanatoa maamuzi wakati bado hawajapishwa kuwa wabunge.

Ukizingatia maamuzi yao mengine yanaathiri wananchi moja kwa moja.
Lissu amesema"Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesema mawaziri watatokana na wabunge na ili kuwa mbunge lazima mtu aape.

Kwa maana hiyo watendaji hao siyo mawaziri kwa kuwa hawajaapa kuwa wabunge.
 
Last edited by a moderator:
ni ukweli huo.....!!!!tatizo watz ni vibaraka wa akili.
Kwani wateule waliopewa ubunge mara ya mwisho na JPM wameshaapishwa na spika?
 
Lissu aisee sasa anaelekea kuwa chizi!!!
Uchizi wake upo wapi?Si kwamba machizi ni hao wanaosigina katiba?
Mbarawa aliapa wapi kuwa mbunge?
Kifungu gani cha sheria kinampa mamlaka kuagiza na kutoa matamko kabla ya kuapa kuwa mbunge?
Jiongeze..Lissu yupo right
 
Lissu angeungana na wenzake watafute kwanza Katibu mkuu wa chama chao (CHADEMA) kabla ya kurukaruka kama chura anayetafuta maji. Anajidai kujua sheria saaana, hebu awaambie Watanzania Katiba ya CHADEMA inasema nini kuhusu muda wa kumpata Katibu wa Chama endapo kiti kiko wazi?
 
ni ukweli huo.....!!!!tatizo watz ni vibaraka wa akili.
Kwani wateule waliopewa ubunge mara ya mwisho na JPM wameshaapishwa na spika?
Katiba inachezewa na mijitu inashangilia kama mazuzu.Tuendapo watajimilikisha nchi na makofi,pongezi watapewa.
Watz sijui tunalaana gani ndio maana majirani wanatudharau
 
Katiba inachezewa na mijitu inashangilia kama mazuzu.Tuendapo watajimilikisha nchi na makofi,pongezi watapewa.
Watz sijui tunalaana gani ndio maana majirani wanatudharau
Mkuu, ni mara ngapi CHADEMA mmechezea katiba yenu na bado mnakaa kimya?
 
Kwa hili walau kwa Mara ya kwanza nimemkubali LISU ,

kwani kufanya kazi ya uwazili kabla ya kiapo cha ubunge nadhani si sawa.
Si vizuri kuvunja utaratibu tulizojiwekea wenyewe.
 
Mkuu, ni mara ngapi CHADEMA mmechezea katiba yenu na bado mnakaa kimya?
Acha vijiswali vepesi.Hapa tunaongelea katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania.Imekanyagwa,Si katiba za vyama
 
Mkuu, ni mara ngapi CHADEMA mmechezea katiba yenu na bado mnakaa kimya?
Chedema kuchezea katiba yao sidhani kama kunahalalisha wengine nao kuvunja sheria,

Heshima yako ni kubwa hapa jf tulia njoo na jibu zuri.
 
Acha vijiswali vepesi.Hapa tunaongelea katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania.Imekanyagwa,Si katiba za vyama
Duh! Mkuu. Yaani ikivunjwa katiba ya CHADEMA unaona poa ila ya nchi! Kwani hao Mawaziri wakifanya kazi bila ya kiapo cha ubunge kuna kitu gani kinapungua? By the way unajua maana ya Separation of power?
 
Eheeee hii ndo Tanzania ya magafuli anakuna kufata sheria yeye atakavyo ona yeye inafaa akuna kuhoji sasa lissu anataka nin
 
Mtazamo wangu:

- Hoja ya msingi anayo, tena sana!

- Ila tusiendeshwe sana na sheria..kama wanatenda sawasawa na majukumu yao basi mimi naona ni vyema. Tuchukue hatua pale tu atakapo-abuse mamlaka yake

- kosa la CHADEMA kuvunja sheria halihalalishi serikali kuvunja sheria.

- kwa mantiki hiyo katiba inatakiwa ifanyiwe marekebisho ili kuepuka kama haya, yaani kuwe na muda mfupi kati ya kuteuliwa waziri na kuapishwa. nadhani hiyo itaondoa malalamiko kwa pande zote. Meanwhile, kama wanafanya mema tuwaunge mkono na kuwasaidia, kama wanakiuka miiko tuchukue hatua stahiki kuwapinga!

#mtazamoWangu
 
Back
Top Bottom