TataMadiba
JF-Expert Member
- Feb 7, 2014
- 9,866
- 5,742
Ibara ya 18 ya Katiba
Tundu Lissu anajifanya kutumia Ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kumjibu Waziri wa Mambo ya nchi za Nje, P. Kabudi , mbobezi wa Sheria kuwa ana haki na wajibu wa kulichafua Taifa kwa kisingizio kuwa anaichafua Serikali. Lakini kwanini Lissu anajitoa ufahamu kwa kutosoma mipaka ya haki na wajibu huo katika Ibara ya 30? Ibara inayolinda uhuru wa watu wengine, Maslahi ya Umma , Usalama wa afya na Maadili visiiingiliwe na watu wanaotumia vibaya haki na wajibu huo kama akina TUNDU LISSU?
Maslahi ya Taifa mbele, Uhuru binafsi wa Tundu Lissu Baadaye, Ibara ya 30 ya Katiba inatulinda. Lissu wewe endelea kubwabwaja huko Uzunguni.