chuma cha mjerumani
JF-Expert Member
- Dec 4, 2013
- 12,180
- 25,417
mawaziri wanapitia kipindi kigumu hamna kitu wanaweza kufanya bila mkuu kusema. awamu tunamawaziri vivuli tuu. wanafanya kazi kwa matukio.
Sasa tunalalamika nini, waende kushatki kesi iende mahakamani maana mahakama hiyo hiyo ndio imewapa wakina lisu ushindi mwingi. Kama ushahidi upo waende mkuu sisi wananchi tunapenda Amani sio unatembea barabarani ukiona jamaa anakuangalia sana unahisi kupigwa mitama anytime. Sasa kulalamika bungeni kwenye Kinga ambapo hata ukisema uongo ufungwi wakati Kuna sehemu nyingi za kuchukulia hatua na sisi tutakuwa hatuwaelewi wenda ni msako wa kiki.Kwani wanaposema kesi ya nyani unampelekea ngedere wewe huwa unaelewa nini?
Haitasaidia kitu, ni mambo mangapi yamefichuliwa kuhusu yule mungu wa Dar na vithibitisho lukuki kuhusu mali za dhuluma anazomiliki na uvamizi dhahiri wa ofisi za watu, lakini bado mwenye nchi kasema hawezi kusikia habari za umbea wa mitandao. 2020 sio mbali inatakiwa kujifunga mkanda na kukaza buti kwa ajili ya kungojea mabadiliko, LAKINI shida yetu wengi ni vichwa vidogo tunasahaulishwa kwa nusu kilo ya sukari na doti ya kanga na kofia kisha tunarudisha shida ileile. KWELI tunahitaji rehma za Mola ili kutooka hapa tulipo.Kama lissu ana ushahidi si autoe hadharani mitandao ya kijamii ipo kwa ajili ya kufichua maovu sio kulalamika bungeni wasiposikilizwa
dawa ni jino kwa jino kwani wao hawana watoto kwanini nao wasitekwe maana utekaji kama umehalalishwa, somalia ilikuwa na vikundi zaidi ya 20 ni wakati wa upinzani kutengeneza vikundi vya kujilinda akitekwa wa uku mnateka wa kule ngoma inakuwa sluu.kulialia basiMna vithibitisho vya mabomu soweto, vithibitisho vya ufisadi wa lowasa, vithibitisho chungu nzima hamjavitoa.
Tutawaamini aje. Nyumbu pekee ndio watawaamini
MUNGU amekupa akili nyingi sana maana yake uonapo mambo yapo kinyume na mapenzi yake basi kwa akili nyingi kabisa tena zenye ubunifu mkubwa alizokupa basi yakupa kuchukua hatua ww ,MUNGU alipo muumba Adam alimpga mamlaka makubwa sana ya ki mungu na ndo maana kila ukionacho hapa duniani jina kiliitwa na Adam lkn pia shetani alikuwepo kwa hiyo yatupasa kuchukua hatua hii c serikali na tuendako c kuzuri na wapinzani kwa ss c muda wa kulia bali ni matendo wasipobadilika as wajue 2020 hawatapata kitu action ni ss.Daaaah Mungu tutetee maana tunapoelekea ni pabaya, Kama alivosema yule mbunge kafumu viongoz ni wanafk
Haitasaidia kitu, ni mambo mangapi yamefichuliwa kuhusu yule mungu wa Dar na vithibitisho lukuki kuhusu mali za dhuluma anazomiliki na uvamizi dhahiri wa ofisi za watu, lakini bado mwenye nchi kasema hawezi kusikia habari za umbea wa mitandao. 2020 sio mbali inatakiwa kujifunga mkanda na kukaza buti kwa ajili ya kungojea mabadiliko, LAKINI shida yetu wengi ni vichwa vidogo tunasahaulishwa kwa nusu kilo ya sukari na doti ya kanga na kofia kisha tunarudisha shida ileile. KWELI tunahitaji rehma za Mola ili kutooka hapa tulipo.
...................................................MUNGU IBARIKI TANGANYIKA.................................................................

hii inanikumbusha miaka ya 90s huko kule kisiwani ukerewe ulitokea ukabaji wa watu kunigwa mpaka wanatoa haja ndogo na kubwa kisha unaachiwa, wananchi wakalalamika sana wilayani lakini wao wakawa wanakanusha hakuna kitu kama hicho, sasa kilichofuata hapo hao jamaa wakaenda kuniga familia nzima ya mkuu 1 huko, kuanzia hapo sasa wao wakaanza kuchukua hatua baada ya wao kukutwa na dhahma hizo, lakini mwanzoni walikataa kabisa kuwa hakuna kitu kama hicho, na waliwezwa kupotezwa kabisa hao wakabaji, mpaka leo watu wanaishi kwa amani na imebaki ni historia, sasa hao wanaopinga isijadiliwe subiri yawakute,Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, alikusudia kutoa Shilingi katika Bajeti ya Waziri Mkuu, akiitaka Serikali na Waziri Mkuu kutoa kauli ya Kuzuia Kikosi Maalumu cha Utesaji, utekaji udhalilishaji na mauaji kinachoratibiwa na Idara ya Usalama wa Taifa, kwa kuwa kikundi kazi hicho kinavunja katiba na sheria za nchi.
Ushahidi wa Utekaji,udhalilishaji , Utesaji na mauaji yanayofanywa na kikundi hicho ulitolewa na Tundu Lissu ambapo alisisima bungeni kuelezea kuwa wapo watu 18 anaowatetea Mahakamani ambao wapo tayari kutoa ushahidi huo, dhidi ya kikundi hicho kinachotumia nyumba iliyopo Mikocheni na Oysterbay ambapo watu mbalimbali wamekuwa wakisafirishwa kutoka mikoani mpaka kwenye nyumba hizo kuteswa kinyama bila jamii kujua.Mbali na ushahidi wa wazi wa Nape kutishiwa bastola hadharani, Bashe kutishiwa maisha na usalama wa Taifa kuwa yupo kwenye orodha ya wabunge 11 wanaotakiwa kufanyiwa mabaya, Godbless Lema na Lissu mwenyewe kukamatwa na polisi bila kibali cha ukamataji kuwekwa rumande na kunyimwa dhamana, Ben Saanane kupotea, Ney wa Mitego kukamatwa, Roma Mkatoliki kutekwa na kuteswa, Clouds Media Group kuvamiwa na mtu ambaye Watanzania wote wanamjua na nashangaa kwanini bado ni Kiongozi wa Serikali na serikali imekaa kimya?Je,kuna baraka za Ikulu?
Jambo hilo limepingwa sana na Mawaziri wa CCM, Jenister Mhagama na Angela Kairuki kwa kuwa wamesema hakuna habari zozote za namna hiyo, wakidai kuwa hakuna utekaji nyara hapa nchini kuwa ni maneno ya baadhi ya watu wa mitandaoni wanoataka kuichafua Serikali .Walimuomba Waziri Mkuu asitoe kauli yoyote kwa kuwa jambo hilo ni uchochezi. Mawaziri hao wameona matukio yote hayo si kitu wala si chochote katika nchi kana kwamba walioteswa si watu wanaowahusu, wala hao hawastahili kulindwa utu wao na kana kwamba si Watanzania. Mawaziri hao wameitetea Serikali na kumwomba Spika kuwa Hoja hiyo isijadiliwe Bungeni.
Jambo hilo lilimpelekea Spika kutaka kura ipigwe na ndipo Wabunge walio wengi wakaomba kujadili kwa kina na serikali itoe kauli. Spika kwa mamlaka yake ameamua jambo hilo lisijadiliwe kabisa ndani Bunge.
*#MyTake katika hili*
Kama Mawaziri na baadhi ya wabunge wa CCM wasiotaka jambo hilo lijadiliwe Bungeni kwa mustakabali wa amani ya Taifa letu, wanadhani kuwa wanaweza kumzuia Mungu asilete wokovu wa Taifa hili kwa njia ya Bunge basi wajue kuwa Mungu ataleta wokovu wa Taifa hili kwa njia nyingine.
Haitasaidia kitu, ni mambo mangapi yamefichuliwa kuhusu yule mungu wa Dar na vithibitisho lukuki kuhusu mali za dhuluma anazomiliki na uvamizi dhahiri wa ofisi za watu, lakini bado mwenye nchi kasema hawezi kusikia habari za umbea wa mitandao. 2020 sio mbali inatakiwa kujifunga mkanda na kukaza buti kwa ajili ya kungojea mabadiliko, LAKINI shida yetu wengi ni vichwa vidogo tunasahaulishwa kwa nusu kilo ya sukari na doti ya kanga na kofia kisha tunarudisha shida ileile. KWELI tunahitaji rehma za Mola ili kutooka hapa tulipo.
...................................................MUNGU IBARIKI TANGANYIKA.................................................................
*#MyTake katika hili*
Kama Mawaziri na baadhi ya wabunge wa CCM wasiotaka jambo hilo lijadiliwe Bungeni kwa mustakabali wa amani ya Taifa letu, wanadhani kuwa wanaweza kumzuia Mungu asilete wokovu wa Taifa hili kwa njia ya Bunge basi wajue kuwa Mungu ataleta wokovu wa Taifa hili kwa njia nyingine
Acha kujitoa ufahamu wewe. Unajua richmond ilikuwa wakati wa uongozi wa nani na huu ni uongozi wa nani? hapa hakuna cha bunge, mahakama, wala polisi. sembuse mtandao? Huu ni mchezo wa mtu mbili.Kwani ya Richmond yaliibuliwa kanisani?njia zilizotumika kuibua zile kashfa zingetumika pia kwa mambo yanayoendelea saiv sio kutegemea masuala kuibuliwa kanisani tena kwa kashfa kubwa.
Mmekata tamaa ya kusikilizwa kisha bado mnalalamika kutaka kusikilizwa aisee tena na mtu mnayemtukana kila siku
Mbona walisema wana ushahidi wa Lowssa fisadi na hawakutoa , hawa tumewazoeaKama lissu ana ushahidi si autoe hadharani mitandao ya kijamii ipo kwa ajili ya kufichua maovu sio kulalamika bungeni wasiposikilizwa