Lissu pole sana, ila wanaCHADEMA bado tunakudai

Countrywide

JF-Expert Member
Mar 2, 2015
18,173
27,223
Habari wanaJF,

Leo kuna jambo nataka kulizungumzia, issue ya matokeo ninapenda kumpa pole Lissu.

Lakini kuna hili jambo lingine ambalo sijalipenda hata kidogo. Lissu kwa sasa anaishi kwenye ubalozi wa ujerumani kwa kile alichosema kutishiwa maisha yake.

Yupo sahihi kwa hilo, lakini akumbuke sisi tulikuwa tunamtegemea kiongozi wetu huyu kutuvusha na sio kukata tamaa.

Ninasema hayo kwa kuwa Lissu alisema mwenyewe kuwa yupo tayari kwa lolote na haogopi tena vitisho, iweje leo aseme ametishiwa hivyo kuamua kwenda kujihifadhi ubalozini?

Na ameenda mbali kwa kusema muda si mrefu anarudi ubelgiji kwa kuwa huku usalama wake ni mdogo.

Lissu kumbuka sisi wafuasi wako tulisema "Lissu sio Lowassa" tukimaanisha wewe sio muoga na upo tayari kwa lolote na ndio maana hata ulipofunga barabara siku ile kwenye kampeni tulishangilia sana kwa kukuona shujaa, sasa leo imekuwaje tena?

Ok, pia umekua ukisema kuwa wananchi wananyanyasika sana wengine wanakufa kwa uonevu, sasa na sisi wananchi tunaoumizwa tukimbilie wapi?? Tupe mbinu, usijiokoe mwenyewe tu.

Wote tunaonyanyasika na sisi tuje tuishi huko ubalozini?

Wanachadema bado tunakudai sana, kwa kuwa uliahidi kutuvusha.
Nawasilisha
 
Tatzo na nyinyi mlimsaliti kwenye maandamano yake, all in all lissu Sasa anasema Kila mtu apambane na hali yake sasa
 
Rais wa Tanzania anaongoza maiti,Lissu nenda zako kaishi maisha yako kwa furaha na tunakutakia kila la kheri!Hizi maiti za bongo achana nazo,ni kupoteza muda wako!

Maisha mema mh Lissu!Labda huko mbele maiti zitafufuka,hapo ndio urejee!
 
alafu pia hta kama alisalitiwa kwenye maandamano mbona alivotoka police hakuendelea tena kuhamasisha kuandamana badala yake akaa kimya na hakutoa upadate yoyote kuhusu maandamano
 
Hapana, yeye mwenyewe amekiri nguvu kubwa ilitumika. Hivyo hatuna kosa, arudi tupambane upya
Tatzo na nyinyi mlimsaliti kwenye maandamano yake, all in all lissu Sasa anasema Kila mtu apambane na hali yake sasa
 
Badala ya kujivusha mwenyewe unasubiri lisu aje akuvushe.
Wewe kirungu tu unaogopa mwenzio alipigwa risasi 30 na HAJAFA .huyu ndo stering wa kweli.
Sio Yule anayetegemea NEC na polisi wamlinde.
"Lisu ni mshindi"
"Maalim ni mshindi"
HAO NDO MARAIS WANGU.
 
Kumbuka tulisema lissu sio lowassa, tukiamaanisha ni ama zetu ama zao. Na tukasema sasa basi, iweje leo akate tamaa?
Rais wa Tanzania anaongoza maiti,Lissu nenda zako kaishi maisha yako kwa furaha na tunakutakia kila la kheri!Hizi maiti za bongo achana nazo,ni kupoteza muda wako!
Maisha mema mh Lissu!Labda huko mbele maiti zitafufuka,hapo ndio urejee!
 
We jamaa bwana,

Kwaiyo kwa vile sio muoga ndio abaki tu hapa, akamatwe, awekwe segerea, wakati huo yy anateseka ww uko na familia yako kwenye kochi unasoma tu Habari za JF au sio

Muwe mnawaza na upande wa pili pia
 
Maumivu ya risasi aliyopata lissu ulimsaidia? Ungekuwa ww unatishiwa maisha ungefanya nn? kuna mtu anapenda kufa kizembe? Anaowapambania hawataki kujipambania,watu walidhani kadhia za miaka 5 atapata lissu kumbe ni wa,nenda lissu kale maisha
 
Lakini tulisema "sasa basi"
Na tukasema lissu sio lowassa, na ana wakili amsterdam, sasa anakamatwaje? Au yule wakili kazi yake nini?
We jamaa bwana,

Kwaiyo kwa vile sio muoga ndio abaki tu hapa, akamatwe, awekwe segerea, wakati huo yy anateseka ww uko na familia yako kwenye kochi unasoma tu Habari za jf au sio

Muwe mnawaza na upande wa pili pia
 
Rais wa Tanzania anaongoza maiti,Lissu nenda zako kaishi maisha yako kwa furaha na tunakutakia kila la kheri!Hizi maiti za bongo achana nazo,ni kupoteza muda wako!
Maisha mema mh Lissu!Labda huko mbele maiti zitafufuka,hapo ndio urejee!
Hahahahahahahaa
 
Tulisema lissu sio muoga, tulisema lissu amejitolea maisha yake kwa ajili yetu

Back
Top Bottom