Lissu na Mbowe wanastahili pongezi

Lissu na Mbowe wanastahili pongezi

Katika sayansi,mwanasayansi anaegundua kitu hupewa pongezi au tuzo maalamu zikiwemo tuzo za Nobel na wakati mwingine kile kitu anachokigundua hupewa jina lake.

Kwa misingi ile ile na sababu zilezile, hapa kwetu tuna mwanasiasa anaeitwa Tundu Lissu ambae ndio alikuwa mtanzania wa kwanza kugundua kuwa kuna "udikteta uchwara" kipindi hicho watu wengi walikuwa bado hawaelewi wakiwamo hata viongozo wa dini waliokuwa wako kimya kabisa huku baadhi yao wakiwa wanamwaga sifa na pongezi kibao.

Hivi majuzi,kama ilivyo katika sayansi, ambapo mwanasayansi anaweza kuendelea kuufanyia utafiti ugunduzi wa mwanasayansi wa awali kwa lengo la kuuboresha au kutoa majibu ya maswali yanayozua utata kutokana na ugunduzi wa awali kitu ambcho hata Mbowe kakifanya majuzi kwa kuboresha ugunduzi/wazo la Lissu na kututangazia kuwa uliopo sasa ni udikteta kamili akimanisha Lissu alikuwa sahihi katika ugunduzi wake wa awali.

Kwa ugunduzi huu,naamini hawa watu wawili wanastahili pongezi(na laba tuzo) hasa Lissu ambae ndio alikuwa mgunduzi wa awali na ambae ugunduzi wake uliwaamsha wengi ambapo leo hii karibu kila mtu anakubaliana na wazo /ugunduzi wake.

Kugundua tatizo mapema ni njia mojawapo muhimu ya kulikabali au kulitatua tatizo hivyo wengi wangegundua tuna tatizo tangu awali, basi ingetusaidia sana kulikabili tangu mapema.

Napozunguzia maswa ya ugundzi wa kisayansi, wale mliosoma arts mnaweza msinielewa sana ila kwa waliosoma sayansi nadhani wengi wataniunga mkono.

Pumbavu
 
Back
Top Bottom