Mtini
JF-Expert Member
- Apr 28, 2011
- 1,487
- 2,344
Hakuna njia nzuri ya kufahamu una marafiki kiasi gani au una maadui kiasi gani kama ukiwa na shida na hasa ukiwa na shida ambayo si ya bahati mbaya.
Kuna shida ambazo ni za bahati mbaya na kuna nyingine ni za kutengenezwa kabisa. Watu wanakaa wanapanga wakutengenezee shida fulani. Kwangu mimi somo kubwa la hii miezi 16 ni hilo.
Nimeweza kufahamu nimegusa maisha ya watu kiasi gani. Nimeendelea kujifunza kuna watu kiasi gani ambao wangefurahi sana kama nisingekuwa kwenye dunia hii. Na hii story bado ina unflod.
Nimegundua kuna mahali nimefanya vitu sawa sawa na pengine kuna mahali nimefanya vitu sio sawa sawa. Nimepigwa risasi ambazo nisingemaliza nusu saa katika hali ya kawaida.
Ukiniangalia hivi unaniona kama Lissu yule wa Bungeni na hakuna namna ya kuwaonesha nyuma ya nguo hizi nikoje lakini ni makovu matupu ya risasi na visu vya hospitalini. Huu mwili umechanwa chanwa sana.
Kushambuliwa kwangu haikuwa ajali, haikuwa bahati mbaya. Kuna watu walikaa mahali wakaamua huyu Tundu Lissu stahili yake afe na afe kwa namna ambayo itatoa fundisho kwa akina Lissu wengine na wanaofikiria kuwa yeye.
Walipanga nife saa 7 mchana katikati ya vipindi vya Bunge. Wakatuma watu wa kuja kutekeleza hivyo ndio maana nasema haya si mazingira ya kawaida.
Baada ya kutengeneza huo mpango wao kelele ilikuwa kubwa sana juu ya matibabu yangu na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu alisema Dada Alice(mke wangu) tunaomba uandike barua ya maombi na Spika naye akasema tunawasiliana na familia tunahitaji tu waandike maombi ili utaratibu wa sisi kulipa gharama ufanyike.
Tuna barua 5 toka Bungeni kuhusu matibabu. Ya mwisho inasema Bunge haliwezi kulipa gharama sababu kwanza hakuna barua ya kibali cha madaktari watatu toka Muhimbili, hakuna kibali cha K/Mkuu Afya na tatu hakuna kibali cha Rais cha kuidhinisha malipo.
Bunge lililipia gharama za matibabu ya Samwel Sitta ambaye hakuwa Mbunge kwa wakati ule lakini alituma email ya maombi ya kutibiwa na akalipiwa. Mimi niliyepigwa risasi nikiwa natoka kuchangia Bungeni nimepewa majibu kama hayo.
Eneo nililopigiwa risasi ile siku hakukuwa na ulinzi. Ni mtu mwenye nguvu kiasi gani anaweza kutoa amri ya ulinzi kutolewa mahali wanapoishi viongozi wa juu ikiwemo Mawaziri? Someone very powerful wanted me dead.
Rais Magufuli anavyopenda Televisheni lakini tangu 07.09.2019 hajawahi kutaja hata jina Tundu Lissu. Kuna katweet kamoja kanatembea sana ila siamini kama ni ya Magufuli. Ile ni ya Gerson Msigwa.
Someone ambaye sitilii shaka maneno yake aliniambia the order was akifa, hakuna shughuli Bungeni na msimlete Dar mkimbizeni kijijini mkamzike as soon as possible. Nahofia kutaja majina ila kuna siku nitayataja. Itakapokuwa salama kwao, si kwangu maana mimi ni survivor wa 16 bullets.