Lissu kawazidi akili Mawakili wa Serikali

Lissu kawazidi akili Mawakili wa Serikali

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
25,136
Reaction score
48,363
Februari 16,2026 Jopo la Majaji watatu Mheshimiwa Jaji Fahamu, J. Mheshimiwa Jaji Chuma, na Mheshimiwa Jaji Kamana, liliamua kuwa kifungu cha 194 cha sheria ya mwenendo wa Makosa ya Jinai (Criminal Procedure Act (CPA) ni kinyume cha Katiba kwa kuwa kinampa Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai haki ya kipekee kuomba ulinzi wa shahidi bila kumpa mshtakiwa haki sawa, na pia kinaruhusu maombi ya kusikilizwa upande mmoja bila kuhakikisha haki ya kusikilizwa kwa upande mwingine.

Soma Mahakama Kuu: Kifungu kinachoruhusu kuficha mashahidi wa kesi ni batili na kinyume na Katiba

Sisi tusiojua Sheria tukashadadia kuwa kesho yake Lissu atapeleka hukumu ile mahakamani ili kwenye kesi yake kusiwepo na mashahidi wa uficho.

Kumbe Lissu angepeleka hukumu ile angefungua mlango kwa mawakili wa Serikali kukata rufani kupinga hukumu hiyo isitumike kwenye kesi ya Lissu.

Maana yake huu mwenendo wa Sasa wa hii kesi ungesimama kusubiri uamuzi juu ya rufani hiyo itakayokuwa imekatwa na Serikali.

Wakati rufani inasubiri kusikilizwa muda waliopangiwa kina Jaji Ndunguru ungekuwa unaisha hivyo baada ya maamuzi ya rufani kutoka ingebidi Lissu asubiri tena Jaji Mkuu awapangie tena hao majaji muda mwingine wa kusikiliza hiyo kesi ya Uhaini inayomkabili.

Kitendo cha Lissu kukaa kimya kimefanya kesi iendelee kusikilizwa huku mawakili wa Serikali wakitafuta mbinu mpya ya kuifanya hiyo kesi isikilizwe kwa muda mrefu.
 
Uko sahihi kabisa, nami nilikuwa na mashaka hayo kwamba ile hukumu ya mwanza kupinga mashahidi wa kificho laiti hoja zake zingehamishiwa kwenye kesi ya Lissu ingepelekea mchezo wa delaying tactics kwa upande wa serikali kama ambavyo walikuwa wanafanya kule kisutu!.
 
Uko sahihi kabisa, nami nilikuwa na mashaka hayo kwamba ile hukumu ya mwanza kupinga mashahidi wa kificho laiti hoja zake zingehamishiwa kwenye kesi ya Lissu ingepelekea mchezo wa delaying tactics kwa upande wa serikali kama ambavyo walikuwa wanafanya kule kisutu!.
Jana si umeona wameanza kuleta mambo ya kusema sijui mitandao ya jamii inafanya nini... Ili waseme mashahidi wanaogopa kwenda kutoa ushahidi mahakamani.
 
Hasa akiwa na madaraka ya kugandamiza wengine...
Inakuwa ni hatari sana.
Leo nani anayemuuliza mwigulu juu ya Yale mabasi anayomiliki
?
Nani anajua kama mwigulu analipa kodi au halipi?
Kwann mwigulu nchemba pamoja na usomi wake wote wa uchumi. Hupokea pesa cash badala ya kupitisha bank?
 
Back
Top Bottom