mwengeso
JF-Expert Member
- Nov 27, 2014
- 9,219
- 6,650
Nakubaliana na wewe kuwa maendeleo ya vitu yaendane na mahitaji ya watu kwa maendeleo yao.Kunatakiwa kuwe na BALANCE kati ya maendeleo ya watu na maendeleo ya vitu.
Pia maendeleo ya vitu yazingatie mahitaji ya watu, na yawe shirikishi.
Kwa mfano, huwezi kuwajengea wananchi wa Chato uwanja wa ndege wa kimataifa wakati hitaji lao ni maji, zahanati, madawati,na pembejeo.
Huwezi kuleta maendeleo ya vitu huku ukinyima wananchi / walipakodi haki zao za msingi kwa mfano, kutowapandisha watumishi wa umma mishahara, kuwadhulumu wakulima korosho zao, kuwatoza wanawake wanaojifungua ada ya kujifungua, kuwalazimisha wamachinga kununua vitambulisho, na dhuluma nyingine nyingi.
Zaidi kuna umuhimu wa kuwapa wananchi mamlaka makubwa zaidi ya waliyonayo sasa hivi ktk kuamua mambo yao ya kimaendeleo. Utaratibu uliopo umempa Raisi madaraka makubwa kupita kiasi na kuwafanya wananchi wawe ombaomba kwa Raisi.
Sikubaliani na wewe ya hiyo mifano uliyotoa kwa kuwa yanakisi mtazamo wako kisiasa zaidi kuliko kiuchumi/maendeleo.
Miradi yote iliyotekelezwa au inaendelea kutekelezwa na Serikali iko kwenye Ilani ya Uchaguzi Mkuu, 2015 ya CCM. Ni Ilani iliyokipa chama ridhaa ya kuunda Serikali. Ni imani kuwa Ilani hiyo, ilivyoboreshwa kwenye Ilani ya Uchaguxi Mkuu, 2020 itakipa CCM ushindi mnono ukilinganisha na Ilani ya CHADEMA ya Uhuru, Haki na Maendeleo ya Watu.