Lissu: Dr. Slaa ni Rais ajaye

Lissu: Dr. Slaa ni Rais ajaye

Magnesium

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2014
Posts
317
Reaction score
185
Kuna kila dalili kwamba Chadema na vyama washirika vina mpango wa kumsimamisha Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa kugombea urais Oktoba mwaka huu.

Dalili hizo zilijitokeza hadharani juzi kutokana na kauli ya Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu aliyoitoa katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Viwanja vya Majengo, Moshi akimtaja Dk Slaa kama ndiye rais ajaye huku akieleza uwezekano wa Ukawa kuchukua nchi.

Lissu alimtaja Dk Slaa na Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo kuwa ndiyo wabunge wa Chadema ambao hawajawahi kushindwa na CCM tangu mwaka 1995.

“Historia hiyo itasema mbunge mmoja kati yao (ambao hawajawahi kushindwa na CCM) ni Mzee Ndesamburo na historia hiyo itasema mbunge wa pili ambaye hajawahi kushindwa na CCM ni Dk Willibrod Slaa, rais wetu ajaye,” alisema Lissu.

Mjumbe huyo wa Kamati Kuu (CC) ya Chadema, alisema katika historia ya Taifa hili kuna uwezekano mkubwa wa Chadema na vyama washirika kuingia Ikulu baada ya Oktoba.

Vyama washirika ambavyo vinaunda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) vya Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD, vimepanga kusimamisha mgombea mmoja katika ngazi zote za uchaguzi kuanzia urais hadi udiwani katika Uchaguzi Mkuu ujao.

Dk Slaa aligombea urais 2010 na kushika nafasi ya pili kwa kupata kura milioni 2.3 sawa na asilimia 26.34 nyuma ya Rais Jakaya Kikwete aliyeshinda kwa kura milioni 5.3 sawa na asilimia 61.17.

Hadi sasa Ukawa haijateua wagombea wake katika ngazi hizo ambazo ni urais, ubunge na udiwani ambao watachuana na wagombea wa vyama vingine.

Chanzo: Mwananchi
 
Sasa wanazunguka mbuyu wa nini? Wenzao wakitaja rais wao wanaambiwa wanataka kuivunja ukawa na huyu kiropoko Lissu anaijenga?
 
Mkipuuza tu ushauri wa NCCR-MAGEUZI mtaangukia pua vibaya sana na huyu Malaya wenu.
 
Hajakosea magamba yote yanyongwe yanahaha sana na yatatajana pindi kitanzi kitapo fika.
 
Hatufai ataifilisi hazina kwa kujikopesha kila siku, then ameshindwa kuidhibiti vhadema katika ubadhirifu ataiweza jamhuri ya muungano wa tanzanai.
 
Slaa akiwa rais atafunga mafisadi wengi mno na kutaifisha mali zao. Mafisadi vyupi vinabana sasa hv hii habari sio njema kwao hata kidogo.
 
Mkipuuza tu ushauri wa NCCR-MAGEUZI mtaangukia pua vibaya sana na huyu Malaya wenu.
Hivi nyie vijana wa chama tawala mtaacha lini matusi? matusi hayajengi hoja sana sana yanaonyesha hulka ya mchangiaji ilivyo, tujirekebishe tujenge nchi yetu sote.
 
Vyovyote iwavyo. Raisi wa Tanzania anatoka UKAWA. Tumechoswa na up.u.mb.avu wa ccm. Mlifukia wizi wa Richmond, mkasoma upepo, mkapotezea.Imekuja Escrow, mmeiba, bila haya mnadiriki kuwasimanga watanzania eti million kumi fedha za mboga!. Mkajidai kuwahadaa Watanzania, na sasa mnaanza kusafishana ikiwa na dharau kubwa kwa Taifa na kuhalalisha ufisaid wa ki firaunni.

Ccm kwendeni mbali mtuachie nchi yetu. Jiandaeni kurudisha mali mlizotuibia. Hatuna mizaha, na hatuna mashara kwa masuala ya uhai wa taifa.
 
Slaa ni kilema wa mkono na mguu hataweza kukabiliana na changamoto za nchi yetu
 
Kuna kila dalili kwamba Chadema na vyama washirika vina mpango wa kumsimamisha Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa kugombea urais Oktoba mwaka huu.

Dalili hizo zilijitokeza hadharani juzi kutokana na kauli ya Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu aliyoitoa katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Viwanja vya Majengo, Moshi akimtaja Dk Slaa kama ndiye rais ajaye huku akieleza uwezekano wa Ukawa kuchukua nchi.

Lissu alimtaja Dk Slaa na Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo kuwa ndiyo wabunge wa Chadema ambao hawajawahi kushindwa na CCM tangu mwaka 1995.

“Historia hiyo itasema mbunge mmoja kati yao (ambao hawajawahi kushindwa na CCM) ni Mzee Ndesamburo na historia hiyo itasema mbunge wa pili ambaye hajawahi kushindwa na CCM ni Dk Willibrod Slaa, rais wetu ajaye,” alisema Lissu.

Mjumbe huyo wa Kamati Kuu (CC) ya Chadema, alisema katika historia ya Taifa hili kuna uwezekano mkubwa wa Chadema na vyama washirika kuingia Ikulu baada ya Oktoba.

Vyama washirika ambavyo vinaunda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) vya Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD, vimepanga kusimamisha mgombea mmoja katika ngazi zote za uchaguzi kuanzia urais hadi udiwani katika Uchaguzi Mkuu ujao.

Dk Slaa aligombea urais 2010 na kushika nafasi ya pili kwa kupata kura milioni 2.3 sawa na asilimia 26.34 nyuma ya Rais Jakaya Kikwete aliyeshinda kwa kura milioni 5.3 sawa na asilimia 61.17.

Hadi sasa Ukawa haijateua wagombea wake katika ngazi hizo ambazo ni urais, ubunge na udiwani ambao watachuana na wagombea wa vyama vingine.

Chanzo: Mwananchi

Tuache mzaha mzee ndesamburo anafaa sana kupeperusha bendera ya ukawa na anajua kujenga hoja kwa wapiga kura, ni mzee pekee asiyekuwa na kashfa yeyote, huyu mwingine huwa nahitaji sabuni kidogo ya mumwosha japo dodoki linaweza lisihitajike.
 
Naona sasa mnataka mtukubmbushe yaliyotokea Zambia.
 
Vyovyote iwavyo. Raisi wa Tanzania anatoka UKAWA. Tumechoswa na up.u.mb.avu wa ccm. Mlifukia wizi wa Richmond, mkasoma upepo, mkapotezea.Imekuja Escrow, mmeiba, bila haya mnadiriki kuwasimanga watanzania eti million kumi fedha za mboga!. Mkajidai kuwahadaa Watanzania, na sasa mnaanza kusafishana ikiwa na dharau kubwa kwa Taifa na kuhalalisha ufisaid wa ki firaunni.

Ccm kwendeni mbali mtuachie nchi yetu. Jiandaeni kurudisha mali mlizotuibia. Hatuna mizaha, na hatuna mashara kwa masuala ya uhai wa taifa.
Nyie endeleeni kuwaabudu SLAA na MBOWE huku wakikifilisi chama, miaka 22 bado makao makuu yako kwenye chumba cha kupanga hamuhoji nuo ufisadi.
 
Back
Top Bottom