Lissu anaweza kupewa nchi ila utawala wake utafananaje?

Lissu anaweza kupewa nchi ila utawala wake utafananaje?

Keynez

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2007
Posts
3,777
Reaction score
6,907
Kuna nguvu kubwa sana inatumika na imekuwa inatumika miezi 12 iliyopita kuzima ushawishi na nguvu ya Mhe. Tundu Lissu, hamahama ya CHADEMA ikiwa mojawapo. Kuna uwezekano Mhe. Lissu atakaporudi ataikuta CHADEMA iko juu ya mawe. Niliwahi kusema huko nyuma, baada tu ya uchaguzi wa 2015 kwamba tofauti na fikra za wengi, Madiwani wana umuhimu mkubwa kwa CHADEMA kuliko hata Wabunge lakini kama chama inaonyesha wanashituka zaidi wakisikia mbunge amejiuzulu kuliko mamia ya madiwani waliorudi CCM.

Sasa ikatokea Mhe. Lissu akagombea Urais na niseme ukweli, bado ana ushawishi mkubwa ila afanye marekebisho madogo sana katika uwasilishaji wake wa hoja, wengi tunajua ni mfumo ndiyo unateua Rais kabla hata hajapitishwa na chama au hajachaguliwa na wananchi.

Naona uwezekano mfumo huu huu ukamkabidhi Mhe. Lissu nchi ila majority ya Wabunge wakiwa wa CCM. Hali hiyo itampa wakati mgumu sana wa kuongoza nchi, matokeo yake itabidi aongoze nchi kwa style ile ile aliyokuwa anaipigia kelele, kama vile kumuaibisha au kumfundisha adabu. Kwa bahati mbaya sana CCM imeamua kufuata siasa zisizo safi.

Hili tumeshalishuhudia mfano kwenye uongozi wa jiji la Dar es Salaam. Upinzani umepewa jiji na halmashauri nyingi nchi nzima ila CCM imeamua kutumia turufu yao iliyokuwa hatarini kuondolewa na Warioba ya maRC na maDC kuvuruga utendaji wao. Wanashindwa hata kuupa mtaa jina bila kuwa overruled!

Ni muhimu sana kwa upinzani kujitafakari. Nimesema mara nyingi tu humu, upinzani kuna watu smart na wengi wenye nia njema na nchi ila wajue kusoma siasa za nchi zinavyoendeshwa kwa sasa na wafanye mabadiliko stahiki. Hivi hivi mtapewa nchi lakini mkaivuruga kuliko hata mlivyoikuta kwa sababu mlishindwa kujipanga ipasavyo.
 
Alafu jana niliota lissu kawa rais wa JMT.

Miaka fulani ya nyuma nilikuwa na rafiki yangu mmoja Mkenya. Wakati huo Uhuru Kenyatta alikuwa anashika nafasi za nne huko kwenye chaguzi za Uraisi Kenya. Nikawa namwambia huyu jamaa kuna siku atakuja kuwa Rais alikuwa ananibishia sana. Kuna 'VITU' nilikuwa najua ndiyo maana nikawa nampa utabiri huo. Na hilo nililiona kwa Obama mapema sana. Hivyo hivyo kwa Lissu, yeye kuwa Raisi wa JMT siyo jambo lisilowezekana kama wengi mnavyofikiri. Kuna 'vitu' najua.
 
Lissu is the chosen one ☝️ that’s why he survived the assassination attempt.
 
Kama mfumo ndo unateua raisi basi ufanye the needful haraka sana kwenye uchaguzi wa 2020, la sivyo hii nchi inakwenda kwa acceleration kubwa sana towards the negative direction!, Lissu apewe nchi ajenge taasisi imara, tatizo la nchi yetu ni ukosefu wa Taasisi imara!. Asimamie mchakato wa katiba bora, hii ya sasa ni sababu mojawapo ya sisi kupiga marktime bila kusonga mbele!. Hakuna Continuity, Kila Raisi anayekuja anakuja na plan zake tofauti!
 
Basi kwa mara ya kwanza, upo wrong, time will tell.
 
Chadema wenyewe hawawezi kumpa lisu agombee kiti cha uraisi coz si wa kanda yao pandwa, sad sasa huo uraisi ataupataje!!!???
 
Uko sahihi kuwa Lissu atakuwa raisi wa Tz 2020, mengine hujaeleweka, mara cdm itakuwa juu ya mawe, lissu abadili style ya kuongea, ccm itakuwa na majority wabunge, system ndo inachagua raisi, etc. Next time be precise
 
Kama mfumo ndo unateua raisi basi ufanye the needful haraka sana kwenye uchaguzi wa 2020, la sivyo hii nchi inakwenda kwa acceleration kubwa sana towards the negative direction!, Lissu apewe nchi ajenge taasisi imara, tatizo la nchi yetu ni ukosefu wa Taasisi imara!. Asimamie mchakato wa katiba bora, hii ya sasa ni sababu mojawapo ya sisi kupiga marktime bila kusonga mbele!. Hakuna Continuity, Kila Raisi anayekuja anakuja na plan zake tofauti!
"Lissu apewe nchi", kumbe watu wanapewaga nchi? [emoji15] [emoji15] [emoji15]
 
Lissu is the chosen one ☝️ that’s why he survived the assassination attempt.
Not only he survived to tell the tale but also it is the same reason of becoming future president he was assalted.
 
Huu ni uzi wangu wa tatu na mwisho nilioamua kuufufua kwa leo. Soma kwa makini na chukua hatua.

Wengine hatuongei kabla hatujafanya tafakuri kubwa.
 
Back
Top Bottom