Uchaguzi 2020 Lissu anaongelea tu Serikali za Majimbo kujiamulia mambo ila haelezi gharama za uendeshaji zitatoka wapi

Sera ya majimbo ni ya kibepari.

Tanzania limekua katika misingi ya kijamaa, hatutaiweza.

Hii ilipaswa kuanza wakati tunapata uhuru sio leo.
 
Hii hoja ya majimbo ccm imewakamata pabaya sana.Kila siku wanatapa tapa bila kuwa na point mtambuka.
Ukweli ni kwamba mfumo wa majimbo ni mzuri tunataka tuchague gavana ili akizingua tunampiga chini.

Sent from my SM-J730GM using JamiiForums mobile app
 
Mfumo wa majimbo unategemeza Utawala wa Sheria ambao ni takwa muhimu kwa wananchi kuweza kujiletea maendeleo.

Ni wazi kuwa mfumo wa serikali kuu, mikoa na wilaya uliasisiwa na unaungwa mkono na watawala ambao wanaishi na kunufaika na utawala kiimla wa kutoka juu kwenda chini.
 
Lisu anaongelea tu majimbo kujiamulia mambo ila haelezi gharama za uendeshaji jimbo litatoa wapi.

Anaeleza kijanja janja huku akificha kuwa uendeshaji jimbo unatakiwa uendeshwe kwa pesa za ndani ya jimbo ikiwemo miradi ya maendeleo.

Chukulia Singida tegemeo lake kuu la uchumi ni kuuza vidumu vya mafuta ya alizeti. Hivyo vyaweza jenga barabara za lami? Kilomita moja tu ya lami inasoma Gharama ya bilioni moja. Hivyo vidumu vya alizeti vyaweza jenga barabara na kulipa mishahara ya wafayakazi wa jimbo?

Afafanue pia kuhusu gharama za kuendesha jimbo asilaghai tu ohh mujiamulie wenyewe.

Ukimsikiliza uaona kabisa mlaghai kwenye gharama za uendeshaji na za miradi ya maendeleo zitakako toka hagusi anahamia hoja nyingine mbio.
Wewe pimbi sikiliza soma kwanza USA wanaendeshaje majimbo usiongee ujinga wako hapa
 
Wewe pimbi sikiliza soma kwanza USA wanaendeshaje majimbo usiongee ujinga wako hapa
Kila Jimbo linajitegemea ndio maana Kuna majimbo Marekani yenye umaskini wa kufa mtu na yako mengine matajiri kupita maelezo
 
Mkuu, katiba ya Warioba haikupigwa chini bungeni. Kilichofanyika CCM walibadili baadhi ya vipengere ... Wapinzani wakasusia. Pamoja na CCM kuikamilisha wao wenyewe bado wameshindwa kuileta kwa Wananchi waamue!!
Suala la majimbo ni cha “kike”, litauvunja nchi vipande vipande.
 
1600856024112.png
 
Jiulize ni kwanini jimbo la Bwege na mengine ya upinzani yanaonekana “mzigo”, tafakari kwa undani usiitazame taswira ya juu juu ukajenga hoja potofu.

Sera ya majimbo inakwenda kujenga hulka ya watu kujitambulisha kwa maeneo wanayotoka, jambo ambalo ni bata sana linaloua moyo wa utaifa.
Kwahiyo majimbo ya wapinzani hamna raslimali ndiyo maana ayaendelei?
Mbona ata kwasasa tunajimbulusha tunapotokea...mfano Jembe letu JPM anaongea Kisukuma ili wapate kura za wasukuma wote
 
Jiulize ni kwanini jimbo la Bwege na mengine ya upinzani yanaonekana “mzigo”, tafakari kwa undani usiitazame taswira ya juu juu ukajenga hoja potofu.

Sera ya majimbo inakwenda kujenga hulka ya watu kujitambulisha kwa maeneo wanayotoka, jambo ambalo ni bata sana linaloua moyo wa utaifa.

..kama hiyo ndiyo hofu yako basi tulitakiwa tusiwe na mikoa, wilaya, na hata vijiji.

..mbona mataifa yenye mfumo wa majimbo wananchi wake ni wazalendo na wana moyo wa utaifa?

..Uzalendo ktk nchi yoyote ile unafifishwa na ukosefu wa haki na matumaini kwa wananchi
 
Upinzani wetu ni ule wa kutoka bungeni wakati wa mijadala muhimu ya kitaifa.

Ni upinzani mzigo kwa walipa kodi.

Mfano jimbo la kawe lina hazina ya rasilimali watu ya kutosha lakini mbunge wetu Halima kwa miaka kumi hata mara moja hajawahi kuonekana bunju A wala B yeye muda wote ni kuzozana na watu Twitter.

Hajawahi kushughulika na shida za Kawe, na huo ni mfano mmoja tu.
Halima sio kazi yake kuleta maendeleo kawe hilo ni jukumu la mkusanya kodi
 
..kama hiyo ndiyo hofu yako basi tulitakiwa tusiwe na mikoa, wilaya, na hata vijiji.

..mbona mataifa yenye mfumo wa majimbo wananchi wake ni wazalendo na wana moyo wa utaifa?

..Uzalendo ktk nchi yoyote ile unafifishwa na ukosefu wa haki na matumaini kwa wananchi
Serikali za majimbo zitayanyanyapaa baadhi ya majimbo na kuyapandisha hadhi mengine.

Asikudanganye mtu kwamba eti majimbo yatakuwa na uwezo wa kujisimamia na kujiletea maendeleo.
 
Serikali za majimbo zitayanyanyapaa baadhi ya majimbo na kuyapandisha hadhi mengine.

Asikudanganye mtu kwamba eti majimbo yatakuwa na uwezo wa kujisimamia na kujiletea maendeleo.

..mbona sasa hivi kuna mikoa na wilaya?

..Je, kuna mkoa au wilaya unanyanyapaa mkoa au wilaya nyingine?

..Kwa mfano, wilaya ya Kinondoni imewahi kunyanyapaa wilaya ya Ilala?

..Au mkoa wa Geita umewahi kunyanyapaa mkoa wa Shinyanga, au Simiyu?

..hata wakati wa mkoloni na mara baada ya uhuru majimbo hayakuwa na matatizo.

..wananchi waliweza kutoka jimbo moja kwenda lingine kutafuta fursa.

..pia wapo watumishi wa serikali walikuwa wakihamishwa toka jimbo moja kwenda lingine.
 
Back
Top Bottom