Uchaguzi 2020 Lissu anaongelea tu Serikali za Majimbo kujiamulia mambo ila haelezi gharama za uendeshaji zitatoka wapi

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
36,908
51,906
Lissu anaongelea tu majimbo kujiamulia mambo ila haelezi gharama za uendeshaji jimbo litatoa wapi.

Anaeleza kijanja janja huku akificha kuwa uendeshaji jimbo unatakiwa uendeshwe kwa pesa za ndani ya jimbo ikiwemo miradi ya maendeleo.

Chukulia Singida tegemeo lake kuu la uchumi ni kuuza vidumu vya mafuta ya alizeti. Hivyo vyaweza jenga barabara za lami? Kilomita moja tu ya lami inasoma Gharama ya bilioni moja. Hivyo vidumu vya alizeti vyaweza jenga barabara na kulipa mishahara ya wafayakazi wa jimbo?

Afafanue pia kuhusu gharama za kuendesha jimbo asilaghai tu ohh mujiamulie wenyewe.

Ukimsikiliza uaona kabisa mlaghai kwenye gharama za uendeshaji na za miradi ya maendeleo zitakako toka hagusi anahamia hoja nyingine mbio.
 
Usilazimishe Kutokuelewa Kwa Maksudi, unazidi kuudhihirisha ujuha wako.

Je, unayajua Majimbo yatakavyokua na mikoa itakayoyaunda hayo majimbo?

Hiyo singida uisemayo itakua katika jimbo la kati litakalojumuisha mikoa ya MOROGORO, DODOMA SINGIDA NA TABORA. haya hapo umasikini unatokea wapi ikiwa kuna vyanzo vingi vya mapato katk mikoa hiyo.

Mnakera hata kama mnalipwa, wengi ni mambumbumbu. Yaani weupe vichwani.
 
Sera ya majimbo msingi wake ni ubinafsi, ukabila na roho ya uchoyo.

Ni sera ambayo imechukuliwa kutoka nje pasipo kuangalia msingi wa utaifa wetu.

Msingi wa utaifa wa Marekani ni tofauti na ule wa Russia ni tofauti na ule wa Zambia ni tofauti na ule ww Afrika ya Kusini.

Ni sera ambayo ukiitazama kwa juu juu unaweza kudanganyika.
 
Chukulia Singida tegemeo lake kuu la uchuimi ni kuuza vidumu vya mafuta ya alizeti.
Ipo hivi kutakuwa na serikali kuu,serikali ya mkoa na serikali ya jimbo na serikali ya vijiji. Rasilimali ya mkoa mfano kama Arusha utalii na madini hivi chini ya serikali ya mkoa, kodi serikali ya jimbo, usimamizi wa maendeleo serikali za vijiji.


Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
Sera ya majimbo msingi wake ni ubinafsi, ukabila na roho ya uchoyo.

Ni sera ambayo imechukuliwa kutoka nje pasipo kuangalia msingi wa utaifa wetu.

Msingi wa utaifa wa Marekani ni tofauti na ule wa Russia ni tofauti na ule wa Zambia ni tofauti na ule ww Afrika ya Kusini.

Ni sera ambayo ukiitazama kwa juu juu unaweza kudanganyika.
Uchoyo utatoka wapi?

Mbona nyie kwa mfumo wa sasa ndo mnafanya uchoyo na ubaguzi? Kwa nini Magufuli alisema hawezi kujenga stand jimboni kwa mbunge Bwege kwa sababu ni mpinzani?

Kwa ini Magufuli amesema wazi mchana kweupe kwenye kampeni zake kuwa hawezi peleka maendeleo sehemu watakazochagua wapinzani?
 
Mkuu Yehodaya, sera ya kunadi serikali za majimbo ni hatua ya awali kabisa ya kutaka kurudisha mamlaka ya kusimamia vyama na kwa ufanisi rasilimali na mapato kwa wanachi badala ya kuhodhiwa na viongozi wachache waliopo serikali kuu. Sera hii ina mfanano na ile ya Mwl. Nyerere ya madaraka mikoani, isipokuwa hii mipango yote ya mapato na matumizi itasimamiwa na bunge la jimbo husika.

Gharama za uendeshaji wake utakuwa ni sawa kabisa na kama inavyoendeshwa hivi sasa na serikali kuu. Na vyema ikaeleweka ya kuwa, kwa uwepo wa serikali za majimbo, itakuwa si kwamba fedha zote zipatikanazo kutoka ktk jimbo husika zitatumika zote hapi hapo tu. La hasha! Kwa yale majimbo yenye mapato zaidi sehemu ya fedha zake zitapelekwa serikali kuu kwa ajili ya uendeshaji wa shughuli zake, na pia kuyapiga jeki majimbo mengine yenye changamoto zaidi za kifedha.
 
Uchoyo utatoka wapi?

Mbona nyie kwa mfumo wa sasa ndo mnafanya uchoyo na ubaguzi? Kwa nini magufuli alisema hawezi kujenga stand jimboni kwa mbunge Bwege kwa sababu ni mpinzani?
Jiulize ni kwanini jimbo la Bwege na mengine ya upinzani yanaonekana “mzigo”, tafakari kwa undani usiitazame taswira ya juu juu ukajenga hoja potofu.

Sera ya majimbo inakwenda kujenga hulka ya watu kujitambulisha kwa maeneo wanayotoka, jambo ambalo ni bata sana linaloua moyo wa utaifa.
 
Jiulize ni kwanini jimbo la Bwege na mengine ya upinzani yanaonekana “mzigo”, tafakari kwa undani usiitazame taswira ya juu juu ukajenga hoja potofu.

Sera ya majimbo inakwenda kujenga hulka ya watu kujitambulisha kwa maeneo wanayotoka, jambo ambalo ni bata sana linaloua moyo wa utaifa.
Nijibu swali langu usilete tantalila
 
Mkuu Yehodaya, sera ya kunadi serikali za majimbo ni hatua ya awali kabisa ya kutaka kurudisha mamlaka ya kusimamia vyama na kwa ufanisi rasilimali na mapato kwa wanachi badala ya kuhodhiwa na viongozi wachache waliopo serikali kuu. Sera hii ina mfanano na ile ya Mwl. Nyerere ya madaraka mikoani, isipokuwa hii mipango yote ya mapato na matumizi itasimamiwa na bunge la jimbo husika...

Nigeria inabebwa na wingi wa watu wa ndani na wa nje, lakini utaifa wake upo hoi, sababu ni hiyo ya kujitambulisha kimajimbo.

Nchi nyingi zenye sera hii zinakuwa na vuguvugu jingi sana la ubaguzi wa ndani haswa masuala ya ukabila.
 
Sera ya majimbo msingi wake ni ubinafsi, ukabila na roho ya uchoyo.

Ni sera ambayo imechukuliwa kutoka nje pasipo kuangalia msingi wa utaifa wetu...
Hivi mnadhani kwa kuwa chama tawala nyie mna hatimiliki ya akili za Watanzania?

Kwamba sisi hatuelewi tunachoambiwa kuhusu majimbo yanayosemwa na kwamba tutapelekwa tu halutakuwa na vikao vya kuamua namna gani hayo majimbo yaendeshwe? Faida mojawapo ya majimbo tumeelezwa ni kuongozwa na Magavana wa kuchaguliwa, sasa hivi Wakuu wa mikoa na wilaya hawana tofauti na viongozi wa Kikoloni (Area commissioners) waliokuwa wanqogopwa kwa kukamata wananchi na kuwaweka ndani hata kwa makosa yasiyotajwa kwenye sheria.

Mmemsilkia Magufuli mwenyewe akisema wazi hata vitambulisho vya Machinga watu hawakupaswa kulazimishwa, lakini uliza mikoani Wakuu wa Wilaya ambao ni wateule wa Rais na Makada wa CCM wamewatendea nini Wananchi? Ni watumishi wangapi wamekamatwa kwa amri ya maDc kwa kosa la kuchelewa kikao cha mkubwa, huku sheria ikimtaka DC kukamata na kuweka ndani masaa 24 kwa makosa ya jinai na uvunjifu wa amani pekee na si makosa ya Nidhamu? Tumechoshwa na umyanyasaji wa "Wakoloni" wenu weusi.
 
Usilazimishe Kutokuelewa Kwa Maksudi, unazidi kuudhihirisha Ujuha Wako.

Je Unayajua Majimbo yatakavyokua na mikoa itakayoyaunda hayo majimbo?

Hiyo singida uisemayo itakua katika jimbo la kati litakalojumuisha mikoa ya MOROGORO, DODOMA SINGIDA NA TABORA. haya hapo umasikini unatokea wapi ikiwa kuna vyanzo vingi vya mapato katk mikoa hiyo.

Mnakera hata kama mnalipwa, wengi ni mambumbumbu.! Yaani Weupe vichwani.
Concept ya majinbo ,ni kutolaliana kuwa mnachangia gharama za uendeshaji jimbo kwa mgawanyo sawa na hakuna eneo linamlalia mwenzie chake.

Jimbo hugawanywa kwa mikoa lakini kila mkoa chake chake sio kuwa singida ataponea pesa zitazoingizwa morogoro hata kama wako jimbo moja isipokuwa kwa ile miradi ya pamoja.

Ukiunda jimbo ni kuwa mfano umeunda jimbo lenye mikoa miwili wa singida na kilimanjaro usidhani hapo kuwa pesa za utalii za kilimanjaro zitaenda singida .Haiwezekani .kodi kila mkoa unakusanya zake asilimia fulani ndio wanapeleka mfuko wa jimbo hawapeleki zote kwa ajili ya kugharimia gharama za uendeshaji wa jimbo. Lakini hakuna mkoa ambao utabeba mkoa mwingine kwa pesa zake kila mmoja anajibeba mweyewe.
 
Nijibu swali langu usilete tantalila

Upinzani wetu ni ule wa kutoka bungeni wakati wa mijadala muhimu ya kitaifa.

Ni upinzani mzigo kwa walipa kodi.

Mfano jimbo la kawe lina hazina ya rasilimali watu ya kutosha lakini mbunge wetu Halima kwa miaka kumi hata mara moja hajawahi kuonekana bunju A wala B yeye muda wote ni kuzozana na watu Twitter.

Hajawahi kushughulika na shida za Kawe, na huo ni mfano mmoja tu.
 
Back
Top Bottom