Lissu aibukia Mahakama Kuu, atangaza mgomo wa kula hadi apewe dhamana

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,278
25,846
Mbunge wa Singida Mashariki na Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA,Tundu Lissu amewasilisha maombi ya dhamana katika Mahakama Kuu ya Tanzania baada ya kukataliwa dhamana na polisi

Maombi hayo yamewasilishwa na Lissu kupitia Wakili wake Peter Kibatala. Kibatala amesema kuwa Polisi walikuwa na muda wa kutosha kufanya uchunguzi wao,mwezi mmoja,na hawana sababu ya kukataa kumpa dhamana Lissu

Chanzo: Mwananchi
================

Tundu Lissu ameendelea kushikiliwa na Polisi bila kufikishwa mahakamani. Hajafunguliwa mashtaka yeyote hadi sasa na Polisi wameendelea kumkatalia dhamana. Unyanyasaji huu dhidi wa Wawakilishi wa Wananchi na viongozi wengine wa Chama unatia doa kubwa demokrasia katika nchi yetu.

Baada ya mashauriano na Mhe Lissu na familia yake, chama kimeridhia na kimeafiki Mhe. Lissu kuanza rasmi mgomo wa kula chochote (hunger strike) hadi hapo atakapofikishwa mahakamani na kufunguliwa mashtaka rasmi.

Tuendelee kumuombea Mhe. Lissu pamoja na kuijaza faraja familia yake pamoja na viongozi wetu mbalimbali wanaopambana na Utawala huu wenye kila kiashiria cha Kidikteta.
 
Mhe Lissu ameendelea kushikiliwa na Polisi bila kufikishwa mahakamani. Hajafunguliwa mashtaka yeyote hadi sasa na Polisi wameendelea kumkatalia dhamana. Unyanyasaji huu dhidi wa Wawakilishi wa Wananchi na viongozi wengine wa Chama unatia doa kubwa demokrasia katika nchi yetu.

Back
Top Bottom