Rashda Zunde
JF-Expert Member
- May 28, 2022
- 297
- 285
Naandika mimi Rashda Zunde✍️
Tupo katika Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu, awamu ambayo ni tulivu, huru na demokrasia imetawala na mpaka dunia inatambua kwamba sasa Tanzania Mama anafanikisha, izidi kusonga mbele.
Rais Samia Suluhu hana shida na ni muumini wa demokrasia ndio maana aliirejesha mikutano ya hadhara iendelee akiamini kwamba wapinzani pia wanachangia yeye kutekeleza majukumu yake kama Rais wa nchi hii, Rais wa wananchi wote.
Sasa mikutano imerudishwa na kila mtu anafanya kwa kufata utaraibu unaofahamika, lakini cha ajabu ni kwamba Lissu ameanza kuturudisha sobibo, anaturudisha sehemu ambayo tulishatoka muda sana na Rais Samia alishatufuta machozi sasa tunasonga mbele.
Jana akiwa kijiji cha Ilolangulu wilaya ya Mbogwe mkoa wa Geita alikosa watu wakumsikiliza jambo lililosababisha watu wamcheke na hivyo aliamua kuhairisha mkutanao akaondoka lakini wote tunajua sababu ya kwanini watu hawakwenda (acha kutusi viongozi wa nchi, wananchi hawapendi).
Kwa kuona aibu, usiku Lissu na kundi lake wakaamua wachome gari lao la matangazo halafu wanasema ni vijana wa CCM. Ebu acheni siasa za ajabu, mnataka muonewe huruma kisa? Mnataka mturudishe sobibo kisa? Na mnasema gari limechomwa na vijana wa CCM, je, mliwaona? Walikuja wamevaa nguo za chama? walibeba kadi zao ndio mkawatambua au ni mihemko yenu tu?
Suala la kukosa watu kukusikiliza upuuzi wako ni jambo la kawaida lakini ndio utambue kwamba watu hawapendi siasa zako za hovyo, yani wewe Lissu kila ukipanda stejini ni kumtusi Rais tu huna hoja nyingine?
Sasa basi kama mnasema vijana wa CCM ndio wamewachomea gari, mtafuteni Comrade Kawaida, mwambieni vijana wake wamefanya nini, maana si mnawatambua? Lakini kama mmeropoka tu basi TANPOL wakiwachukulia hatua kwa kusema uongo na kusingizia watu bila sababu za msigi msilalamike.
Tanzania tupo salama, Lissu na wenzako acheni siasa za zamani, tayari tumeshatoka huko.