Lishe ya mgonjwa wa vidonda vya tumbo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lishe ya mgonjwa wa vidonda vya tumbo

Discussion in 'JF Doctor' started by jamadari, Mar 3, 2010.

 1. jamadari

  jamadari JF-Expert Member

  #1
  Mar 3, 2010
  Joined: Feb 13, 2010
  Messages: 295
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Ili kupunguza makali au kujiepusha kabisa na ugonjwa wa vidonda vya tumbo, unapaswa kujiepusha na tabia ya kula na kushiba kupita kiasi, kwa sababu kushiba sana huchochea uzalishaji wa asidi nyingi wakati wa usagaji chakula tumboni.

  Mbali na hilo, vyakula vyenye mafuta na sukari nyingi na vyenye kiwango kidogo sana cha kamba lishe, imethibitika kuwa husababisha madhara mengi tumboni. Katika makala ya leo, tutaangalia aina ya vyakula anavyopaswa kula au kuviepuka mgonjwa ili kupata nafuu na kuishi bila kusumbuliwa nao:

  VYAKULA VYENYE VIUNGO VINGI
  Epuka ulaji wa vyakula vilivyopikwa na kuungwa viungo vingi vya aina mbalimbali, kama vile pilipili kali za aina zote na viungo vingine vyenye ladha ya ukali ambavyo hutiwa ndani ya mboga ama chakula ili kuongeza ladha.

  POMBE NA KAHAWA
  Pombe na kahawa au vinywaji vingine vyenye ‘caffeine’, vinaweza kuleta matatizo kwa mtu mwenye vidonda vya tumbo na kwa mtu asiye navyo anaweza kupatwa na tatizo, hivyo ni vyema kuepuka au kutumia kwa kiasi kidogo vinywaji hivi. Kimsingi vinywaji hivi huongeza asidi tumboni na hivyo vinaweza kusababisha vidonda au kuzidisha maumivu kwa anayeumwa.
  ULAJI CHUMVI
  Utafiti uliowahi kufanywa nchini Marekani umeonesha kuwepo kwa uhusiano kati ya ulaji chumvi na vidonda vya tumbo. Mgonjwa anashauriwa kuepuka ulaji wa vyakula vyenye chumvi nyingi, hususan vyakula vya kusindika ambavyo huwekwa chumvi nyingi ili visiharibike haraka. Pia jiepushe na kuongeza chumvi kwenye sahani wakati wa kula.

  MAFUTA YA SAMAKI
  Baadhi ya utafiti unashauri wagonjwa wa vidonda vya tumbo wale mafuta yatokanayo na samaki (Omega-3 fats) ambayo yameonekana kutoa ahueni kwa wagonjwa. Na kwa mtu ambaye si mgonjwa atakuwa anajiwekea kinga dhidi ya vidonda vya tumbo na magonjwa mengine ya tumbo.

  VITAMINI NA MADINI
  Ulaji wa vyakula vyenye madini na vitamini kwa wingi husaidia sana kuleta ahueni kwa mgonjwa wa vidonda vya tumbo na kutoa kinga kwa wale ambao hawajaathirika. Wataalamu wa lishe wanashauri kupenda kula matunda na mboga za majani kama vile karoti, juisi ya kabeji, ndizi mbivu, na matunda mengine yenye vitamin C, halikadhalika maziwa ya mbuzi, jibini na cream za maziwa huleta ahueni.
  STAILI YA MAISHA NA VIDONDA VYA TUMBO
  Licha ya kusabisha Saratani, uvutaji sigara pia huongeza hatari ya mtu kupatwa na ugonjwa wa vidonda vya tumbo, hivyo ni sababu tosha ya kuacha uvutaji sigareti. Japo msongo wa mawazo unaweza kuwa vigumu kuuhusisha moja kwa moja na vidonda vya tumbo, lakini maisha ya wasiwasi, ukichangaya na ulaji mbovu, huweza kusababisha ugonjwa huu, hivyo kama unataka kujiepusha au kupunguza makali ya ugonjwa huu, ni muhimu kuzingatia ulaji sahihi na kuishi maisha ya furaha.
   
 2. Rubi

  Rubi JF-Expert Member

  #2
  Mar 3, 2010
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 1,623
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  uko sawa.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...